Tuliokuwa tunamponda Magufuli akiwa hai, sasa tutamtetea akiwa Amekufa!

Bwana ROBERT HERIEL samahani sana sijawahi kukukosoa lakini leo ngoja nikukosoe kidogo.

Magufuli sio kwamba alipendwa na tabaka la chini kwa kuwahenyesha matajiri hapana.

Magufuli alipendwa na mtanzania yoyote mzalendo angalia usimamizi wa rasilimali kipindi cha magufuli mtu alikuwa akilipa kodi anajua kabisa kwamba kodi yangu inaenda kuleta matokeo na anayaona kweli mfano ujenzi wa bara bara na madaraja, ni tofauti sana na kipindi hiki mtu akitoa kodi hana amani ya moyo anajiuliza hii kodi natoa inaenda tumboni kwa mtu au inaenda kufanya nini.

Kingine wafanyakazi kipindi cha magufuli walikuwa wanajituma anajua mda wowote nikifanya uzembe sina kazi kwa kifupi nidhamu kazini ilikuwepo tofauti na kipindi hiki ambacho mfanyakazi anaweza akaenda kazini akasign kitabu basi akaamua kufanya mambo mengine.

Lakini tuseme tu ukweli watanzania bila kiongozi imara kazi haziendi.

Lakini pia jaribu kuangalia suala la uslama mfano majambazi huku mitaani kipindi cha magufuli lilipungua kabisa.

Kipindi cha magufuli ulisikia mnyama yoyote kasafirishwa kwenda ulaya?.

Kifupi Magufuli alipendwa sababu si kuwaonea tabaka la juu hapana jamaa alipendwa sababu ya ushapavu wa kulinda rasimali za nchi yake sasa katika harakati za kusimamia rasimali akajikuta anatengeneza uadui na hao wapi dili wa tabaka la juu.

 
Umasikini mbaya sana. Tena saaaaana. Kama ni hivi basi naachakusoma hii makala yako
 

Kitu kimoja unachoshindwa kuelewa ni kuwa, kwa sasa, watu si kuwa wanamsema Jiwe kama Jiwe, yeye sasa ni mifupa.
Wanasema aina yake ya uongozi mbovu, matendo yake mabovu na mabaya yote ili uongozi uliopo na ujao wasije kuyarudia.

Huwezi kuzuia hilo, hatukatai kuna mazuri pia alifanya na atapongezwa kwa hayo. Shida ni mzani wake ukoje? Kati ya mazuri yake na mabaya yake, hapo kila mtu ana jibu lake, kutegemea na alivyoguswa.
Tusifokeane na Tusipangiane.
 

Watanzania wanolipa Kodi ya moja Kwa moja ni wachache Mno Mkuu!
Wengi wetu hatulipi Kodi ya moja Kwa moja.

Fuatilia hapo mtaani kwenu ni wangapi wanalipa Kodi moja Kwa moja utaelewa nazungumzia nini. Kwenye kumi utaona anayelipa Kodi ni mmoja.

Wengi wetu ni wakwepaji wa Kodi Hali iñayopelekea hao wachache wanalipa Kodi ya moja Kwa moja kubanwa na kuhenyeshwa.
 
Hakuna jema alilofanya hapa duniani.
 
Tumegawanyika! Wale wa vyeti feki na wapigaji kamwe hawawezi kuwa pamoja na jpm, sisi wa huku bondeni tuko pamoja na jpm kwa miundombinu ya usafirishaji aliotuachia.. wezi andeleeni kumponda
 
Ubaya aliofanya hakuna mtu atasahau
 
Wakulima bei za mazao ziliteremka lazima ulikumbuke hilo
 
Nenda kazikwe naye Chato, huyo alikuwa muuwaji, fisadi, na dikteta kuliko Sani Abacha na Mobutu Sese Seko
 
Watumishi wa serikali hawakuongezwa mishahara wala kupanda madaraja pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…