Tuliokuwa tunamponda Magufuli akiwa hai, sasa tutamtetea akiwa Amekufa!

Si lazima duniani uelewe vyote, vikikushinda vingine unakaa kimya.
 
Hao viongozi waliowaheshimu, kuwasikiliza na kuwatii walifanya nini kipindi chote cha uhuru wa TZ kabla ya JPM kukamata madaraka ya Urais 2015?

Ngozi nyeusi ni ngumu sana kuipeleka kilelemama lelemama, ndiyomaana tunaendelea kuwa maskini tukipumbazwa na democracy ilihali maisha yetu ni ya kipumbavu sana.

Nature yetu ngozi nyeusi ni kupata maendeleo kwa njia fupi tu za dili ilihali namna ya kudumisha hayo maendeleo ni 0.

JPM alikuwa anaujua sana udhaifu wa wafanyakazi wengi serikalini na taasisi binafsi hasa ikiwa alishakaa katika uongozi wa ubunge na uwaziri zaidi ya miaka 20 kabla ya kuwa Rais wa TZ.

Kwa namna hiyo utamdanganya nini sasa kuhusu kuinyoosha hii nchi kiuongozi?
 
Mzanzibar kaongea. πŸ˜… anamzungumzia magufuli kwa mfano wa hitler πŸ˜†πŸ˜† ama kweli akili ni mali. Unazungumzia ukali wa mbwa kwa kutolea mfano wa chui.
 
Kama lile bwawa lililokula mamia ya mamilioni juzi tu hapa. πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ushasema Alikua na mabaya yake mengi Sana, usipoukemea ubaya wake atakuja kuibuka mwingine akifuata nyayo zake akijua ndio wengi wanapenda rais anaetafuta kiki kuliko usawa wa haki.
Huyu wa sasa hana mabaya? Au mnasubiri afe ndo mkemee πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ni kweli mkuu magufuli alifanikiwa kirahisi kabisa kuwadanganya watu wajinga ambao kwa Tanzania ndio wengi kuwa alikua mtetezi wa wanyonge na mpaka leo wanaamini kuwa asingekufa mpaka leo nchi ingekuwa haina haya matatizo iliyo nayo kama kupanda kwa bei za mafuta,nauli nk
 
Na tozo zisingekuwepo. Mafuta gharama isingekuwa kubwa kuliko wanaopitishia bandarini kwetu, waziri mdogo angekuwa hatembelei helicopta
 
Hakuna kupumzika, JPM lazima anangwe tu na Mtanzania anayeipenda Nchi yake. Yule baradhuli alikuwa anatuharibia nchi vibaya sana. Tushukuru Mungu tu aliiingilia kati akamchukua kumpeleka jehanam
Na atakuchukua na wewe kukupeleka huko huko. Yeye amepumzika unajichosha tu na mikelele yako.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Unafiki ndio Siasa za Waafrika
Aliyepo hawaoni km anakosea sehemu, ye sa hv ni malaika. Au wanasubiri awe marehemu ndo wamuamshie oooh alimkalisha flan rumande miezi kadhaa, mara alishindwa kutupa tenda ya kushuti royal tour n.k
 
Chama tawala wameamua kucheza ngoma ya wapinzani bila kujua, taratibu wanapoteza wafuasi wao (pro Magufuli). Kwa maana nyingine chama tawala wanashambuliana wenyewe kwa wenyewe, wakisaidiwa na wapinzani.

Kama jina lile lisingekuwa na nguvu, wasingesimama kujitetea kila siku kuwa watamaliza miradi iliyoachwa. Kama jina lisingekuwa na nguvu wasingekusanyika chart kuazimisha. The best choice ni kukaa kimya.
 
Chuki ni chukizo. [emoji16] hata lile la kusema fagilia simba siyo jema? Huyu aliyepo hebu nae mmwambie mabaya yake mapema ili baadae tukwepe kuwatuhumu marehemu
Hapa tunaongelea Jiwe habari za wengine hizo fungulia uzi wake.
Jiwe hakuna alichokifanya chenye neema kwa watanzani.
 
Na tozo zisingekuwepo. Mafuta gharama isingekuwa kubwa kuliko wanaopitishia bandarini kwetu, waziri mdogo angekuwa hatembelei helicopta
Huu ni wivu wa kijinga kabisa
 
Hapa tunaongelea Jiwe habari za wengine hizo fungulia uzi wake.
Jiwe hakuna alichokifanya chenye neema kwa watanzani.
Unafiki na uzandiki tu ndo umewajaa. πŸ˜’πŸ˜’
 
Ukisikia mtu anakwmabia historia itakuhukumu ndio hivyo.

Mambo ndivyo yalivyo. Wewe uliyetendewa mazuri ila hujali watu walioumizwa hongera.
 
Alitutisha tusimseme akiwa hai, sasa hayupo, acha asemwe, asiyetaka kumsema pia akae kimya, ni uamuzi wake.

Magufuli ndio kaweka historia yake ya kusemwa au kutosemwa ama kwa mazuri au kwa mabaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…