Tuliopitia maisha ya "Saidia Fundi" tukutane hapa

Ile kazi ni ngumu mkuu, sema inategemeana na speed ya fundi mwenyewe,
Kingine utaiona rahisi Kama huna malengo mengine ya kimaisha
Ugum sikatai.ilaukisema kwamba kama huna malengo mengine utaiona rahisi naona.kama sio sawa mkuu watu wanaingia kule kwakuwa wanaona nikazi yamwisho nawatu wanaingia kule kwamalengo tofauti wanaoingia kule kutafuta pesa ndohutoka namajibu haya lakini wanaoingia kutafuta ujuzi huwaongezea bidii yakufikia malengo yao lakini pia sio vizuli kunawatu wanaapa kutokurudia huko au mtu anasema asingependa kuona mwanae akifanya kazi hiyo mliofanikiwa kimaisha nasasa mko maofisini mnaweza kusema vyovyote lakini tulio nje ya ajira lasimi niwambie kazi hii haipatikani kirahisi tena waliopata matatizo kwenye ajira zao wanajua nachoongea .ivi unakuta kijana amemaliza chuo amekosa ajira mwisho anaona ajiue bora nn
 

Hapo kwenye kuibiwa baiskeli hapo[emoji23][emoji23] naelewa mziki wake man ukirudi home msala wake ni kama umedondosha BMW X6 kwenye daraja.
 
Hapo kwenye kuibiwa baiskeli hapo[emoji23][emoji23] naelewa mziki wake man ukirudi home msala wake ni kama umedondosha BMW X6 kwenye daraja.
Acha tu baba'ke icho kipigo nilichopewa na mzeebaba na hata p*ssy ya yule manzi sikuikumbuka tena[emoji3][emoji3][emoji3] ila kesho yake nikaikumbuka.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi nilipitia huko mwaka 2002,baada ya kumaliza o' level. Bahati nzuri wakatinipo shule jirani na bweni kulikuwa na gym,kwahiyo asubuhi gym jioni baada ya masomo tunakwenda kucheza mpira.

Kimwili nilikuwa fit kinoma nimejengeka haswa! Siku ya kwanza jamaa jirani yangu baada ya kuniona niponipo tu sina ramani ,akanichukua nikamsaidie fundi.

Kazi niliyoikuta ilikuwa ni kumwaga zege " jamvi".niliwakimbiza wazoefu hadi walishangaa.mazoezi yalinisaidia.

Niliendelea na kazi na hiyo timu ya ujenzi kwa miezi kadhaa,matokeo yakatoka nikawa nimefeli.

Sikujali kwasababu tayari nilishaanza kushika hela,nikaona kama mambo ya shule yatanipotezea muda.

Baada ya miaka mitatu nikawa fundi kamili,naweza kazi zote za ujenzi mpaka kuweka tiles.

Hapo sasa ndio nikakumbuka shule,nikajiunga masomo ya A level private. Yale masomo ya jioni kwenye vibanda umiza,nikawa nawahi kutoka job naenda kusoma,nikafanikiwa kumaliza,nikafeli tena.

Sikukata tamaa,nikaenda VETA kuongeza ujuzi wa hii fani ya ujenzi ,nikafaulu vizuri, nikaomba nafasi ya masomo chuo cha ardhi.

Nikahitimu ,nikarudi tena kwenye ujenzi.safari hii nikiwa foremen.

Miradi mikubwa niliyowahi kushiriki.Msamvu Terminal, new SUA hostels, PPF tower

Usimamizi wa miradi ya ujenzi binafsi ni mingi tu nimefanya.

Najivunia,kujenga nyumba ya mama yangu,na za wadogo zangu kwa mkono wangu mwenyewe bila usaidizi wa mtu mwingine,na nyumba zangu nimejenga mwenyewe,hivyo gharama za ufundi kwa familia zilikuwa free.


Nisichojivunia.sikutegemea kama hii ndio ingekuwa ajira yangu.ndoto zangu zilikuwa kuwa daktari wa mifugo wa JWTZ.nilipenda sana kuwa mwanajeshi mwenye fani ya udaktari.
Nashukuru Mungu kwa yote,maisha yanakwenda murua kabisa.

Yule jamaa aliyeniingiza kwenye saidia fundi miaka ya baadae nilimuoa dada yake.kwahiyo ni shemeji yangu . Namshukuru sana.
 
Hongera mkuu hata mm.imenisaidia kuna watu wanailani kazi hii
 
Hongera mkuu hata mm.imenisaidia kuna watu wanailani kazi hii
Sasa hiyo mimi saidia fundi ilikuwa 2002.sasa hivi kupata kazi saidia fundi ni connetion pia.mwambie mtu ambae anaidharau hii kazi afanye majaribio kuitafuta tu kama ataipata. Wapo wahitimu wa ualimu na degree zao wanawasaidia mafundi ambao hata hiyo darasa la saba wamemaliza kwa tabu.maisha yamebadilika sana sasa hivi.
 
Andaa full stori itakuwa poa sana
 
Subili na mimi niwape yangu ingawa ni ya tofauti lkn ni saidia fundi pia


Wakati nimemaliza form six pande za mbeya (old airport) nilikuwa npo nyumbani muda wote nikasema ivi siwez pata sehemu ya kushinda ili niweza kupata pesa ya kununuwa smartphone maana home walikataa kuninunulia adi matokeo yatoke ndo nitapewa, basi nikaongea na mama kuhusu kunitafutia kazi ya kufanya baada ya siku mbili iv kuna rafiki yake flani iv yeye ni fundi umeme basi nikapata connection so nikawa naenda kufanya KAZI lkn zilikuwa ni zile za kawaida yan kutengeza vifaa vya umeme siku zikaenda apo nikaanza kucheza na mchango kabisa pale soko la sido per day ilikuwa 2000 alafu tupo watu kama 145 baada ya week iv jamaa akapata site pande za Isyesye kulikuwa na mjengo unalimziwa kujengwa unavyumba kama 15 so ikabid tuchimbie kwanza alafu ndo tufanye kusuka umeme sasa ikabid mm ndo nipewe KAZI ya kuchimbia bomba/ Condut so kesho yake nikaanza KAZI apo vifaa kama vyote (nyundo, vishoka vidogo, tindo, na nyundo kubwa) aisee kufikia site kumbe mjengo ni wa tofali za block yan iyo ratio yake sio poa maana jamaa alikuwa na pesa hatari
So nikaanza kuchimba ukuta yan kila nikipiga ni cheche tuu zinatoka apo kila chumba kina chimbiwa njia ya soket ,switch pamoja na Tv soket yan nilichimba mpaka mkono ukawa unatetemeka daah apo ndo kwanza simaliza ata chumba kimoja kuna muda uchanga uliingua jichoni daah Ayo maumivu yake sio poa [emoji24][emoji24][emoji24][emoji856]
Baada ya masaa kama tisa nikawa nimemaliza chumba kimoja yan apo hoi daaha nikasema iv kwa nn najitesa ivyo si bora niache tuu [emoji119][emoji119][emoji119] kumbe nilikuwa nimejiweka kwenye mkataba ambao nisingeweza kuacha ile KAZI maana nilikuwa na cheza mchango so jina langu kulikuwa la 136 out 147 alafu icho kipindi ndo tupo jina la 89 but kwa siku wanatoka watu wawili aisee kwaiyo nikiacha tuu pesa yangu imekwenda na maji [emoji856][emoji856][emoji856] daaha ikabid nikomae tuu kuchimbia yan kuna siku nilikata moto maana nilikuwa napanda ngazi alafu kishoka nimekiweka juu ya ngazi sasa wakati na panda kikashuka yani kilinipiga kichwani pale pale nilianguka but baada ya masaa iv nilizinduka na akuna aliye jua maana nilikuwepo mm mwenyewe tuu so ikanibid nilud nyumbani but fundi alivyo kuuliza vipi leo umefanya vyumba vingapi ikabid nimwambie viwili then akasema Sana dog komaa ili tukabidhi mjengo wa watu kumbe mwenzie ata kimoja sijagusa
Ikapita kama week iv akaja yule boss mwenye mjengo pamoja na watoto wake kumbe mtoto wake mmoja wa kike tulimaliza nae form six daah alishangaa Sana kunikuta kwenye ile hali adi machozi yalimlenga maana nilikuwa mchafu hatari ukiongeza na vumbi la block yan ilikuwa sio poa so akasema jaman Mariki umekosa nini adi unafanya kazi kama izo nikabaki na jiumauma tuu then akatokea baba yake akasema vp mnafamiana akasema ndio ndo akanitambulisha lkn mshua wake alishangaa Sana then akasema unalipwa shingapi per day nikasema 5000 akaguna akaniambia nitakuwa nakuongezea 10000 lkn naomba ufanye kazi yangu vizuli so siku zikaenda maisha yakawa mazuli lkn kazi kazi ilifika kipindi Abdala kichwa wazi alikuwa asimami maana sio kwa kuchoka Kule
Nilikuja kupokea mchango wangu yan moja kwa Moja nilienda kwa Mtawa pale ilomba nikanunua simu ili kuwa Tecno Boom J8 kwa shilingi 215000/=

NB
Akuna kitu kizuli kama kujiwekea malengo pia ukitumia kitu ambacho umekipata kwa jasho lako kina kuwa na thamani kubwa sana kwako
 
Mimi nilinunua philips savy. Simu flani ya kijanja kwa wakati wake,[emoji3][emoji3]
 
Mkuu hata mm nimeanza miaka hiyo huwa naishia kucheka tu mtaani hata humu utawasikia umeshindwa kupiga hata yazege kunamtu naelim yake anakuja sait mambo magum anaomba apate japo kibarua cha 5000 kuna wengine humu wamesoma babazao wanafanya kazi hizohizo
 
Kweli aisee...
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…