kuna watoto wa buza,kinondoni,msasani,mbezi nk ukiwaambia unaweza nunua sururu mpya kufika mchana ikabaki nusu hawakuelewi.
hii ndio ilinitokea siku moja nilikuwa mwaminifu sana halfu najali muda mno,akaja fundi mmoja mgeni toka wilaya nyingine kaletwa na boss mwenye nyumba,akapewa saidia mimi hapa.
tukaenda site,kufika nikaandaa mazingira akakata ramani,kisha nashangaa ananiuliza huu msingi kuchimba utachimbwa kwa shingapi??nikiwa nimeduwaa nikaropoka 250k,akazama mfukoni akatoa kibunda 190k,nyingine akanambia mpaka arudi akute maendeleo ya kazi.sikuwahi kushika hela nyingi kiasi hicho kwa kipindi kile.
nikarudi na kuzoa wanangu kibao ambao huwa tunakomaa nao,nikajisemea hapa lazima niwe mjanja,nikawaambia aisee hapa tunachimba hela mpaka fundi aje,wakakubali.ardhi ilikuwa ngumu mpaka nikawa natafakari kama watanielewa nikiwaambia nimetaja 250.tukapiga futi 1.5 kitu usawa wa goti[emoji28][emoji28].tukamsubiri fundi alipokuja wenzangu wakamvaa aongeze pesa bila kusema wamepewa kiasi gani.akaongeza 50 kwenye ile 60 iliyobaki,wao wakajua kazi yote niliomba 110k tu.
hawakuwahi kushtuka.
nilikuja kuachana na hii kazi kuna siku nifungua chokaa vibaya ikaingia puani,niliugua mafua mabaya sana,bahati nikapata ramani nyingine.