Tuliopitia Vita Na Chuki Makazini Tushirikishane Hapa

Hiyo unayofanya wewe ni kibarua sio kazi haiwezekani kuwe Kuna kundi kubwa la watu duni hivyo
 
Ukwel ni kwamba ukishapata kazi usimwamini yoyte yule usiwe mchochezi, na usiluhusu mtu kuwa lafiki Yako wakati WA kazi pia usip nde kukaa kimakundi uwapo kazini
 
Hizi habari za kuzoeana ni hatari achana nazo jiamini ni ushamba kufuatana nyumbani ,kilichokupeleka pale ni uwezo wako fanya wako then kwenu sijui kuna shughuli uwaleta mara hivi.

Jamaa alikuja hapa kwangu tena kwake hataki mtu akafika mara anaanza hoja za kijinga mbona kuzuri hapa ingiza mademu ,mara hivi umenunua sh ngapi ? ushamba mzigo nikamchana .

Kazini chuki ni lazima na swala la kutongoza basi ushajishusha maana hao washaambiana ofisi nzima inajua ni balaa.
 
Halafu hii tabia ya mtu kuuliza hii shngapi; hii shngapi inakera Sana aisee
 
Ukitoka ofisini,ishi maisha yako mengine kabisa nje ya ofisi,

Kua na marafiki wengine kabisa ambao sio wafanyakazi wenzako,muingiliano na wafanyakazi wenzako unatakiwa uishie pale unapotoka nje ya geti la ofisi,

Kuna ofisi zingine,wafanyakazi wanakua na hivi vigroup vya WhatsApp,sio kwa ajili ya info za kiofisi bali ni ujinga ujinga tu,achana na hivyo vigroup,trust no one,usiache watu wakujue sana au wakuzoee sana nje ya mambo yahusuyo kazi.
 
Naomba full picture ya umuhimu wa marafiki wa chini kabisaa
Mlinzi yupo masaa mengi kazini inshu zote anaziona. Ila hamwambii mtu isipokuwa mshkaji wake au mtu anayejua hawezi kusema kwingine. Kumbuka mtu anaouna vitu vingi anatamani aseme ila anaogopa consequences. Kama wewe ni mshkaji na siyo mmbea utajua jinsi ya kmtreat kila mtu kazini kwa kuwa una detail zao. Pia walinzi mara nyingi hawafuuzwi wote kazini utakuta anataarifa za hata miaka miwili na trend ya tabia za watu wa hapo kazini.
Mfagiaji ni kama mlinzi tu huwa wanadumu kazini na anaweza kukusanua taarifa fulani kwa kuwa hana competition na wewe.
 
Aisee..!
 
Sure kabisaa anaweza kukwambia nani mwema na nani mbaya hapo kazini.
Mkuu,unapoenda kufanya kazi kwenye ofisi yeyote ile,sikiliza tu maneno ya kuambiwa kua nani mbaya na nani mwema hapo kazini ila usichukulie serious au kumuhukumu mtu mpaka mtu huyo atakapokufanyia ubaya wewe au wema,sio rahisi kwa mtu kua mbaya kwa watu wote au kua mwema kwa watu wote,

Muhukumu mtu kwa jinsi atakavyo kutreat wewe kama wewe na sio kwa kusikia tu,mtu mbaya kwa wengine anaweza kua mwema kwako au mwema anaweza kua mbaya kwako,

Find the good in people and ignore the bad in them coz no one is perfect.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…