Tuliopitia Vita Na Chuki Makazini Tushirikishane Hapa

Habari za muda huu

Haya yalinikuta kwenye kazi yangu ya kwanza nilipokuwa bado sijafunzwa na Ulimwengu

1. Chuki ya kwanza nilijisababishia mwenyewe baada ya kutongoza wafanyakazi watatu kwa nyakati tofauti wote walichomoa na kumbe walihadithiana ndipo nikaanza kupitia sarakasi na vitimbi hadi nikaona Ofisi Ni chungu.

2. Chuki ya pili nilikuwa na mshkaji alikuwa anapenda kunitembelea, siku moja alikuta kifaa kinachofanana sana na cha Mradi wa Taasisi, akauliza tu friendly umekitoa wapi, nikamjibu nilinunua dukani. Kumbe alienda kumuambia boss kuwa nimeiba kifaa Cha Mradi! Boss na yeye mwanamke, badala ya kuniita na kunihoji, akachukua uamuzi wa kunipunguzia 75% ya majukumu ikwemo ya site kwa hoja ya kwamba nimekosa uaminifu(japo hakuniamba directly, ila aliongea kwa mafumbo).

3. Nilifiwa, wakateuliwa wawakilishi wa taasisi wanisindikize msibani, baada ya msiba wakarudi kuhadithiana Hali ngumu ya kijijini kwetu. Niliposikia kuwa wamehadithia, nikachukua uamuzi wa kumpiga makofi yule dada. Kumbe ilikuwa ni Mali ya Boss, boss akazidisha vitimbi Hadi nikaona nikubali yaishe nikaacha kazi.

Namshukuru Mungu nilipata kazi Nyingine ambayo Ndiyo naifanya Hadi Sasa. Jambo la Msingi nililojifunza ni PRIVACY& CONFIDENTIALITY Ni muhimu Sana wakati wa kujumuika na workmates. Lingine ni KUTOKUMUAMINI YEYOTE KWA WAKATI WOWOTE kwani sehemu kubwa ya Chuki na vita makazini husababishwa na mtu kuwa na DETAILS zako.

Karibuni tushirikishane matukio ya Chuki na Vita tulivyowahi kupitia kazini.
Kazini kuwa time taker, cheka na kila mtu, mpende kila mtu ila usimwamini mtu.
Workmates wakifahamu kuna hatua ya kimaendeleo unapiga chuki zitaanza , hapo jiandae kurogwa
 
Habari za muda huu

Haya yalinikuta kwenye kazi yangu ya kwanza nilipokuwa bado sijafunzwa na Ulimwengu

1. Chuki ya kwanza nilijisababishia mwenyewe baada ya kutongoza wafanyakazi watatu kwa nyakati tofauti wote walichomoa na kumbe walihadithiana ndipo nikaanza kupitia sarakasi na vitimbi hadi nikaona Ofisi Ni chungu.

2. Chuki ya pili nilikuwa na mshkaji alikuwa anapenda kunitembelea, siku moja alikuta kifaa kinachofanana sana na cha Mradi wa Taasisi, akauliza tu friendly umekitoa wapi, nikamjibu nilinunua dukani. Kumbe alienda kumuambia boss kuwa nimeiba kifaa Cha Mradi! Boss na yeye mwanamke, badala ya kuniita na kunihoji, akachukua uamuzi wa kunipunguzia 75% ya majukumu ikwemo ya site kwa hoja ya kwamba nimekosa uaminifu(japo hakuniamba directly, ila aliongea kwa mafumbo).

3. Nilifiwa, wakateuliwa wawakilishi wa taasisi wanisindikize msibani, baada ya msiba wakarudi kuhadithiana Hali ngumu ya kijijini kwetu. Niliposikia kuwa wamehadithia, nikachukua uamuzi wa kumpiga makofi yule dada. Kumbe ilikuwa ni Mali ya Boss, boss akazidisha vitimbi Hadi nikaona nikubali yaishe nikaacha kazi.

Namshukuru Mungu nilipata kazi Nyingine ambayo Ndiyo naifanya Hadi Sasa. Jambo la Msingi nililojifunza ni PRIVACY& CONFIDENTIALITY Ni muhimu Sana wakati wa kujumuika na workmates. Lingine ni KUTOKUMUAMINI YEYOTE KWA WAKATI WOWOTE kwani sehemu kubwa ya Chuki na vita makazini husababishwa na mtu kuwa na DETAILS zako.

Karibuni tushirikishane matukio ya Chuki na Vita tulivyowahi kupitia kazini.
Duh
 
Kila kazi ina changamoto zake kwa sababu Watanzania ni wale wale. Boda boda mnamchukia pia mwenzenu ambaye anapata wateja wengi mnaanza kusema ni mchawi, na nyie mnaanza kwenda kwa waganga. Basi inakuwa ni mwendo wa waganga tu! Hela yote inaishia huko kwa waganga halafu pikipiki ni ya hesabu.
Au Wana mchukia mwenye Boxer mpya wakati wao Wana pikipiki za zamani
 
Kiufupi waafrika hatupendani kuna ile story ya HR wa barrick gold mine kuwalipa pesa kiduchu wafanya kazi licha ya management kuidhinisha pesa kubwa ila HR alikataa akasema kama hawataki tutaleta wengine ndio utajua wabongo jinsi tulivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli tena ukute HR kutokea uko Kilimanjaro wanapenda kutetea wazungu kama ndugu zao, utakuta Mzungu kakubali kulipa pesa nyingi, HR ana mkataza husiwalipe hivi walipe hivi, Yani HR alitokea jamii ya kanda ya kaskazini tu ujue staff mme umia.
 
Ishi vizuri na hao maofisini. Toa lonja kwa Wana wageni hapo kazini. Siku moja moja hawawezi kukusahau kukutoa. Kumbuka maisha ni duara. Uaminifu na ustaarab ni kitu muhimu. Ukiweza kujiendeleza fanya hivyo.
Kuna jamaa alihadithia maskani kuwa kuna mwana alifukuzwa kazi kwa Faizar kiwanda Cha mikate Dar kisa kavaa sendo zile za 60,000 kama Mwarabu. Mwarab kumuona akakwambia kwa mshahara ninaokupa huwezi kuvaa sendo ya bei hii. Wewe unaniibia. Akamfuta kazi hapohapo. Hili ni funzo kuwa weka password ktk maendeleo yako kazini. Wengine si wazuri.
 
Supervisor wangu nimemzidi elimu, nimemzidi/tunafanana salary. Kwa miaka mi4 sasa tunaishi na ww3.

Mm sina urafiki na workmates, nipo busy na kazi then narudi home lakini tabu iko pale pale. (chuki zipo tu hata ufanye nn, trust me hata Mungu anachukiwa na baadhi ya watu).

I will never Quit, I will never resign. (Siwezi kukata tamaa na kurudi nyuma kwa sababu ya mtu mmoja).

Kila sehemu kuna changamoto zake, changamoto haziishi. Safisha nafsi, kuwa mtu mzuri na mtegemee Mungu katika kila hatua.
Safi sana piga kazi kiongozi
 
Habari za muda huu

Haya yalinikuta kwenye kazi yangu ya kwanza nilipokuwa bado sijafunzwa na Ulimwengu

1. Chuki ya kwanza nilijisababishia mwenyewe baada ya kutongoza wafanyakazi watatu kwa nyakati tofauti wote walichomoa na kumbe walihadithiana ndipo nikaanza kupitia sarakasi na vitimbi hadi nikaona Ofisi Ni chungu.

2. Chuki ya pili nilikuwa na mshkaji alikuwa anapenda kunitembelea, siku moja alikuta kifaa kinachofanana sana na cha Mradi wa Taasisi, akauliza tu friendly umekitoa wapi, nikamjibu nilinunua dukani. Kumbe alienda kumuambia boss kuwa nimeiba kifaa Cha Mradi! Boss na yeye mwanamke, badala ya kuniita na kunihoji, akachukua uamuzi wa kunipunguzia 75% ya majukumu ikwemo ya site kwa hoja ya kwamba nimekosa uaminifu(japo hakuniamba directly, ila aliongea kwa mafumbo).

3. Nilifiwa, wakateuliwa wawakilishi wa taasisi wanisindikize msibani, baada ya msiba wakarudi kuhadithiana Hali ngumu ya kijijini kwetu. Niliposikia kuwa wamehadithia, nikachukua uamuzi wa kumpiga makofi yule dada. Kumbe ilikuwa ni Mali ya Boss, boss akazidisha vitimbi Hadi nikaona nikubali yaishe nikaacha kazi.

Namshukuru Mungu nilipata kazi Nyingine ambayo Ndiyo naifanya Hadi Sasa. Jambo la Msingi nililojifunza ni PRIVACY& CONFIDENTIALITY Ni muhimu Sana wakati wa kujumuika na workmates. Lingine ni KUTOKUMUAMINI YEYOTE KWA WAKATI WOWOTE kwani sehemu kubwa ya Chuki na vita makazini husababishwa na mtu kuwa na DETAILS zako.

Karibuni tushirikishane matukio ya Chuki na Vita tulivyowahi kupitia kazini.
Ngoja nami niweke case yangu

Nliajiriwa taasisi flani ya elimu kubwa tu hapa Dar baada ya miezi mitatu tu mkuu wa taasisi akatokea kuniamini sana kutokana na ufanyaji wangu akaniita ofisini akanipiga brush ya maana juu ya kitengo kingine nyeti katika taasisi hiyo kabla ya kutoka ofisini akaniambia nipitie reception kuna barua nichukue. Kucheck kaniongezea majukumu mengine nyeti sana na wenye safari za kutosha nafika kwa boss wangu wa kitengo changu kashatumiwa ujumbe akaniweka kitimoto sema sana umekuja juzi tu unajifanya wewe ndo mfanyakazi bora sio tutaona. Bwana were

Picha linaanza naye akaniongezea majukumu ikawa nkiingia kazini asubuhi natoka saa nne usiku nkifika nyumbani sita usiku ikawa ni kawaida mwili ulikubali ila nlichakaa hatari. Nkarudi kwa mkuu kumwomba anitoe kwenye kitengo cha kwanza akaniambia nkikutoa huko hicho kitengo kitashindwa kuperfom aseee ile kazi ilinitesa nlishindwa kufanya mambo ya msingi ya kwangu binafsi ya maendeleo ndugu wakaniweka kando kwasababu muda wote ilikua ni kazi na mimi.

Baada ya miaka minne rasmi ikaanza vita ya kuniharibia aseee ombea hii kitu usiombe watu wakuamulue jambo nlipigwa vita ya kufa mtu ikawa ni mashtaka kila siku uzuri mkuu wa taasisi aliliona hilo akatuita akampa makavu boss wangu mbele yangu bwana weeeee ilitokea tu nkaanza kuichukia kazi mwenyewe nkawa siendi kazini sina sababu nkafatwa mpaka kwangu na mkuu wa taasisi akaniuluza kama kuna jambo haliko sawa nimweleze lakini sikuona tatizo lolote hatimaye nkaacha kazi mwenyewe ukiniuliza Leo kwanini nliacha sinaga sababu Ila sijawahi kujutia mpaka kesho huo uamuzi
 
Nilikuwa kwenye kampuni flani na wajinga flani mngoni na mfipa,wakapiga zenge kwa boss ili niondoke kibaruani.nikasema hawa hawanijui vizuri itakuwa.mbona tumepigwa wote termination letter,na hawakuwa wamejipanga na mtaa,wanaishi maisha ya hovyo kwelikweli.
 
Hahaaaaaa....
Walimwaga mboga ukatoboa sufuria hahaaa
Ulimwambiaje bosi hahaaa sipati picha yaani vile unaanza "...bosi ni kweli lakini na fulani na fulani'
Hahaaa
 
Nilikuwa kwenye kampuni flani na wajinga flani mngoni na mfipa,wakapiga zenge kwa boss ili niondoke kibaruani.nikasema hawa hawanijui vizuri itakuwa.mbona tumepigwa wote termination letter,na hawakuwa wamejipanga na mtaa,wanaishi maisha ya hovyo kwelikweli.
Ukamwaga mboga
Dadeki zao [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom