Maamuzi ya walio wengi yaheshimiwe. Wananchi ndio wametaka chama kimoja kitawale baada ya kugundua waliowaamini waliwageuka na kujali matumbo yao zaidi kuliko wao waliowachagua. Kwa mfano, ilifika mahali mbowe alijiona mungu mtu ndani ya CHADEMA ikifika kipindi kama hiki cha uchaguzi anajichagulia tu wanawake anawatumia kingono kama kigezo cha kuwapa viti maalum. Ruzuku ya chama alikua anaitafuna anavyotaka bila kuulizwa na mtu, ukihoji unaitwa msaliti unafukuzwa kwenye chama. Mpaka sasa chama hakijafanya jambo lolote la maendeleo kutokana na ruzuku waliyokua wanapokea. Sasa kiburi kitamuisha, hana ubunge, chama kimepoteza uwakilishi bungeni, ruzuku haipo tena au itapungua kwa kiasi kikubwa sana.Amewanyima tu hao wapinzani ajira ya ubunge, udiwani na hata huo Urais! Ila upinzani hauwezi kufa kamwe. Hata ndani ya hicho chama chake, upinzani na makundi yatendelea tu kushamiri.
Yaani tumerudishwa enzi za Mwalimu! Hovyo kabisa.
Halikadhalika wabunge wa upinzani, baada ya kuchaguliwa hakuna jambo walilokua wanawafanyia wananchi zaidi ya kujijenga kimaisha wao na familia zao. Wakiulizwa kuhusu maendeleo, wanadai hiyo ni kazi ya Serikali, lakini Serikali hiyo hiyo ikifanya wanaibeza. Wananchi walichoka huu ulaghai, wameamua kuwapa lesson. Ukitaka kujua kwamba haya ni maamuzi ya wananchi, utaona ngome nyingi za upinzani ambazo zimechukuliwa na CCM hakuna malalamiko wala wananchi kugomea matokeo ina maana wanajua walichokifanya.
Kwahiyo, walioturudisha nyuma ni Wapinzani wenyewe kwa kuwadharau wananchi waliowapa imani na kuwachagua.