Tuliowahi kufukuzwa kwa watu/kwa ndugu tukumbushiane ilikuwaje

Sec nilikuwaga nikifunga shule nikakaa kwa ndugu wa mama maana nisingeweza kwenda home kutokana na umbali, basi ikabidi likizo fupi niwe naenda huko.
Mm by nature napiga kazi zote za nyumbani bila msaada wa MTU, mama mdogo alikuwa anatuachia kazi Mimi na binti yake yeye anategea mm nazifanya mwenyewe.

Basi mama hiyo alinipenda sana binti yakee hicho kitendo cha mama yake kunipenda hakikumfurahisha.

Siku moja tumekaa tunapiga story na mama mdogo. Binti yake kamwambia hivi :
"mama unavyompenda luckyline akinya ma.vi kwenye sahani unaweza kuilia chakula bila kuiosha"

Jamani nilijisikia vibaya mpaka nikalia.

Nyingine nilikuwa nikifunga basis on kitoka chuo naenda kwa kaka ila WiFi yesu kwangu, kaka akisafiri tunakila ugali dagaa asubuhi na jion, na hapo mm nilikuwa sijazoea ugali bora hata sasa hivi naupenda, nilipata taabu sana. Ila.kaka akitoka safari tunakula kuku balaaa

Na kaka alikuwa na uwezo so alikuwa anaacha hela ya kutosha ila Wifi duh. Kwa sababu nilikuwa chuo na Nina pesa yangu Siku moja nikamwambia mm WiFi ugali asubuhi jioni siwezi nashindwa kwenda choo, Siku hiyo nikisema anaona aibu anatoa.Mchele.

Siku moja ugali ulishinda akasema Tule na jion, nilimwambia mm sili naenda hotelini, nikambeba mtoto wake tukaenda tukala tukarudi nikakuta kavuta mdomo.nikamwambia sirudi hapa wewe ndo unanipigia nije hapa nikija inanitesa wakati vyakula vipo sirudi tena. Akasema nisimwambie kaka. Sikurudiga tena.

Nilivyomuuliza mfanyakazi akasema ndugu wa mwanaume wakija ni ugali non stop.nfyuuuuuuuuuu natamani Siku moja aje kwangu nimpikie bonge LA msosi nimkomeshe.
 

so sad bro maelezo yako mafup ila yamenifanya nitoe choz mzee nna asthma naelewa hyo situation
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
mkuu sema unaonekana sura ako imeka kula vile vitu sana.ndo maana maza hausi akakutimua chumba cha mwanae
 
Hii siri wengi wameipita hata like moja hawajakupa.. Nakupa like 100 kwa mchango huu
 
Hahahaa, Uzi murua sana huu.

Mimi nilifukuzwa kwa Akili sana.
Ilikuwa nikwandugu angu Tena ni baba mdogo I mean mdogo wake na Father Mzazi wangu,Enzi hizo napiga Chuo kikuu hapo kwa makonda ,kilichonifanya kwanza nikae hapo kwa ndugu ni kwamba siku natoka kijjn kwetu naenda Chuo mwaka wa kwanza sem ya kwanza sikufikia chuo ila nikafikia kwa huyo ndugu, nilikaa kwa muda kama mwezi mmoja na hii ni kwasababu Chuo na hapo kwa ndugu ilikuwa ni mwendo w dkk 10 ushafika chuo so sikuwa na sababu ya kutosha kuchomoka hom nikapange, kuna muda ilifika nikamwambia mwenyeji wangu kuwa nataka nitafute chumba mtaani, akanizuia akisema chuo ni kalibu mno sasa unataka utoke uende wapi sehemu ingine iliyo kalibu zaidi ya hapa, nilikosa cha kujitetea ikabidi nitulize ndigiri zangu, trera lilienda likaenda ikaja kufikia kama miezi saba ivi badae nikawa naambiwa niwe najitahidi nakuja na chakula I mean kama mchele , Unga , mboga mboga n.k cha kuliwa na binadamu.
Hii haikuwa na maana kwamba Mzee hakujiweza kuhudumia family, hapana family kwanza ilikuwa ndogo sana na Mzee alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa sana, swala la chakula hapo kwake haikuwa issue hata kidogo, ila hali ilibadilika ikawa ivo natakiwa , angalau kwa wiki niwe nanunua chochote kile kuchangia msosi hapo home, sikumkatalia wala kuhoji chochote ila nilijumlisha na za kuzaliwa ikawa ivo na mm bumu nikipata naleta hapo homu tunakula, ikaenda ikaenda taktaka nyingi sana hapo katkt zilitokea, Mara Mzee anakuja amekunywa bia zake mbili huko kutafuta confidence ya kuja kunivuruga zaidi et mtu anarudi saa nane nightmare kanywa unakuta naww ushapiga mboji anagonga get unamfungulia ,anaanza kukupayukia Mara Maneno kibao Mara eti mpaka siku hiz mama yako kakonda anawaza family itakula nn ww upo tu, Maneno na taka taka nyingi bila sababu za msingi.
Nilichokifanyaga niliwasapliz kwa kuhama kimya kimya maana sikuwa na vitu vingi sana vya kuhamisha labda ni involvu kigali kunihamisha no ilikuwa simple tu, kimoja moja baada ya kingine tena kwa kutumia rusket ya mgongoni , nilivyomaliza niliwagaga kwa simu tu sikutagaka kuleta kelele sana, aliniasa sana kurudi but it was too late.

Note: kusema ukweli huwa naheshimu na kupiga salute kwa mtu yeyote yule ambae ashamake na kuwa na family yake yenye Furaha na Amani maana huwa natambua ni magumu mengi sana watu wanapitia mpaka kufika hapo walipo, Respect kwenu wadau mlio na Maisha.
I'm glad Mungu alinipambania na mm naenjoy maisha yangu , huwa napenda kutumia misemo kama "Binadamu hutesa kwa wakati, wakati pia utakuja nami Nitatesa na ikawa hivo" , Pia nilikuwa nikijisema mwenyewe kuwa "Mungu hajamuumbia binadamu shida siku zote, ipo tu siku atamsaidia na kumfanya ang'ae kama yalivyo mapenzi yake"

Nashukuru Mungu nilijifunza mengi, lkn niseme tu kuwa kwa wakati niliokaa pale sio tu mabaya yalinisibu Bali haya mema nayo yalikuwepo Mengi tu, nilijifunza japo sikujua kwa kipndi hicho ya kuwa hilo nalo lilikuwa ni darasa, lkn kwangu ile situation ilinifanya Niwe imara sana, Mungu aendelee kuijalia ile family ya huyo Mzee kwa kadri ya mapenzi yake.
 
Nimekuelewa sana nahisi tumeshabihiana sana. Hongera.
 
Haya mambo yanaumiza sana,KAMA HUJAWA TAYARI KUISHI NA MTU...BASI USIISHI NAYE MAANA UTAJILETEA LAANA ZA BURE. KUISHI NA MTU NA KUISHI KWA MTU NI VIPAJI.
 
Nilipokaa popote sijawahi kufukuzwa wala kuteswa zaidi nilikuwa mchapakazi na nilipendwa sana mpaka leo wananipgia simu mara kwa mara hata mimi nisipowakumbuka kuwapigia simu ila sio ndugu ni watu baki sijawahi kukaa kwa ndugu maana nishawahi kumwomba mmoja nikakae kwake kwa wiki 2 ili nijiandae na mtihani akanambia pamejaa na nafasi hakuna.
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] eti pamejaa hlf unajisifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…