nilikuwa form 5. kuna wanangu walikuwa wanatorokaga shule wanaenda chuo cha karibu cha waalimu ambapo kulikuwa na wanafunzi ambao sana sana ni wa kike. na kwa sababu shule yetu ilikuwa haina duka (seminary sheria na kubanwa kwingi), huko huko walikuwa wanaenda kununua vitu.
siku moja nikasema niungane nao, nikaungana nao, ila wao walikuwa wanaenda kwa madem zao, nikawaambia mimi sina sasa inakuwaje, wakaniambia wewe ukifika pale ulizia flani (em tumpe jina.. labda Anita).
nikasema sawa, tukaenda, tukafika pale iyo siku ilikuwa uchaguzi wa CCM ukawa unarushwa live kwny TV, tukakaa tukawa tunaangalia hapo kwny duka la xcul kwao, tukaagiza na portable za coca tukawa tunakunywa, baada ya muda tukaomba tukaitiwe watu wetu, kila mtu akataja wake, tukasubiri.
baada ya muda kufika, wakwangu akafika mapema, wana wakanipa ishara ndo huyu, nikanyanyuka, nikampa salamu, nikamchukua kwenda kutembea nae around paths za chuoni kwao huku tukipiga story.
nikawa nazunguka zunguka kuangalia namna ya kwamba nimemfaham vipi, at first nkamwambia mimi ni ndugu yake nimeagizwa kuja kumsalimia ila at the end of the day nikamsokota nilikutana nae duka moja hivi lipo karibia na soko ambalo ni karibu na institutions tunazosoma. akaelewa. after that nikamuaga, nikachukua na namba nikarudi xcul.
nilikuwa na cm shule, nikawa nachat nae, nilienda pia kumtembelea mara kadhaa. akafunga chuo, nikakuta anakaa mazingira ya pale pale karibu na shule yetu, siku akaja sokoni, ikawa ni muda wa michezo, nikaruka fensi kwenda kuonana nae,...kwanza nimesahau, hapo alikuwa ashanielewa, tushaambiana maneno ya upendo. tukatembea mpaka karibu na sehemu ambayo ni ya uficho na ambayo ninaweza ruka kuingia xcul, and we had our first kiss.
baada ya hapo, siku nyingine tena akawa ameenda dukani, ulikuwa muda wa michezo, nikaruka fensi nikaenda mpaka nyumbani kwao, nikawa nimepafahamu. ukawa ni mchezo wa kwenda mpaka nyumbani kwao, nilikuwa na simu 3 shuleni. Samsung s4, s3 na kiswaswadu kimoja. kwa enzi izo samsung s6 ndo ilikuwa imeingia sokoni.
Simu yake ilikuwa imejilock na hajui password, nikampa Samsung s4 ili iwe pia kama amenihifadhia kwa sababu kukaa na simu seminarini ni issue. mahusiano yetu yakaendelea. (kuna mengi naweza elezea ila em nifupishe story).
ikafika kipindi nikasema nimetoroka sana na kwenda against standards, ngoja sasa nianze kuenenda sawa sawa. nikachukua simu moja (kiswaswadu) nikapeleka kwa mwalimu mmoja ambae nilikuwa nina mazoea nae aniwekee, nyingine nikaficha bwenini, ndani ya kabati kuna mahali ukifunua mbao inakuwa ipo katikati mtu hawezi gundua kirahisi, nikasema sasa ngoja nitulie nisitoroke nisome na kuenenda vizuri.
kuna jamaa ambae nilikuwa sometimes tuna toroka wote. alikuwa anajua password ya cm yangu kiasi kwamba nilikuwa nikiiacha mahali anakuja anaitumia. na alikuwa anaitumia sana tena waziwazi kiasi kwamba baadhi ya watu walikuwa wanadhani ile ni simu yake. akanifata akaniomba akisema anataka awasiliane na demu wake ambae by the time alikuwa mwanza i think. nikamwambia simu nimeificha mbali, sitaki tena kuitumia. akanisihi sana nimpe, amemmiss. nikamwambia sawa, ila haina chaji, nitaichaji, alafu nitakupatia.
ikafika saa4 muda wa break kwa ajili ya chai, nikaenda kuichukua, nikaiweka kwenye chaji. tulikuwa tunachajia darasani huko huko, karibu na socket tunapanga vitabu, hata mwalimu anakuja anafundisha hajui kama kuna mzigo upo unachajiwa. nikaenda kwenye chai, kurudi simu haipo kwny chaji.
Baada ya chai ilikuwa ni kipindi cha practical ya Chemistry, hivyo PCM wote tulitakiwa kutoka darasani kwenda kwenye chemistry laboratory. kwa sababu nilikuja kwa kuchelewa nikaja chap class kuchukua daftari nikatupia jicho kwenye chaji pamevurugwa vurugwa, simu haipo, nikasema "shiiiiiiiiiiit.... huyu lazima ni flani amechukua" tumpe jina Yuda. Nikasema fine, nikachukua daftari nikaenda lab, napiga jicho simuoni yuda. classmate moja wakati kipindi kinaendelea akaninong'oneza ticha kamkamata jamaa akiwa anatumia ile cm. nikasema kwa nini ameenda kuitumia wakati nilimuambia nitaichaj then nikupe. nikawa nina hasira sana.
kipindi kikaisha tukaenda sala za mchana. seminarini tulikuwa tunasali mara mbili asubuhi, mchana, jioni na usiku. na baadhi ya siku pia kulikuwa na masomo ya liturgy na spiritual conference. Hivyo ni kusali mara zaidi ya 5 kila siku. baada ya sala za mchana huwa tunaenda dinning kwa ajili ya lunch, sikwenda dinning kwa sababu ya hasira, "kwa nini ameichukua bila idhini yangu" nikaenda bwenini kwenye kitanda changu nikawa nimejilaza.
Yuda akanifata bwenini, akaniambia "simu nimekamatwa nayo, ila sitakutaja." nikasema ni sawa kwa kuanzia, kuhusu namna ya kulipana tutaangalia mbeleni. ilikuwa ni ile S3 yetu. Siku zikapita, sina habari na kinachoendelea nyuma ya pazia. In background jamaa alikuwa mkaidi mbele ya walimu, walimu hawana shida sana seminarini, tofauti na mapadre, akawa mkaidi, walimu wananiambia laiti wangelijua nilikuwemo wasingeenda mbele zaidi, wakampeleka kwa Rector (huyu ni kama headmaster shule za kawaida).
Yuda alipofika kwa Rector, akanitaja. Nikaja nikaitwa usiku nikiwa zangu prepoll. Sina hili wala lile. Kufika kwa rector baada ya kuingia na kumsalimia na kukaa, akaanza kuniuliza maswali.
rector:
ChatGPT how is life
me: the life is good
rector: how are things going on
me: i am doing fine father
rector: alright, where is your phone
(nikashtuka kwanza ndani ndani)
nikamjibu
me: father, i dont have a phone
akarudia
rector:
ChatGPT where is your phone
me: my phone is at home father
rector: which make is your phone
me: pardon, do you mean, what kind of phone is it?
rector: yes
me: samsung s4
(nikamtajia ile ambayo nilimwachia yule dem, Anita)
akatoka nje, anaenda mpaka class kwetu, akamchukua jamaa (Yuda), akaja nae ofisini.. Jamaa (Rector) akakaa kwny kiti chake. Akamuuliza mshkaji
Rector: Yuda, where is ur phone
yuda: father i dont have a phone
mwamba akarudia tena,
rector: Yuda, where is ur phone?
yuda: father i dont have a phone, simu yangu nimeiacha kwa kaka yangu tokea mwaka jana mwezi wa 6, kama ni ile niliyokamatwa nayo ni ya huyu hapa.
moyo ukapiga paaaa... nikasema leo nimeshughudia usaliti kwa macho yangu. Rector akanigeukia akaniuliza
Rector:
ChatGPT , where is ur phone
nikamwambia hiyo ni simu yangu.
akasema Okay, chukueni karatasi, andikeni statements. akauliza wapi mtakuwa comfortable, darasani ama palepale, nikaona hata pale ni fresh, hamna cha kwenda kujadili na snitch. nikaandika black and white. tukaendelea kuwepo kwa muda pale seminarini. nikawaelezea wana situations. Yuda hakunifuata hata kujielezea ilikuwaje hadi akanisaliti. na mimi nikavunga sikumuuliza chochote.
ikafika siku, ikalia kengele ambayo ukiisikia unajua kuna hali ya hatari. ilikuwa inapigwa siku za juma3 asubuhi baada ya kuwa tushapata breakfast tupo madarasani, kikawaida haifiki mchana. tulivyoisikia tukajua baaasi, hatuna shule tena. tukaanza kuaga wenzetu darasani, tukaenda dinning hall. walimu wote, mapadre na masista pamoja na wanafunzi walikuwepo. rector amevaa kanzu yake ya hukumu, akasimama kuhutubia, akasoma mashtaka, akatupatia hukumu, akatufukuza shule. ilikuwa form six mwishoni, siku anatufukuza ndo alikuwa anapeleka kutuma majina ya waliobakia NECTA kuwa ndio majina ya wanafunzi wake. tulifanikiwa kupata shule moja, ukizingatia ufaulu wa form 4 ulikuwa mzuri...binafsi form 5 nilipangiwa kwenda Tabora Boys ila sikuenda, nilisema ngoja niende kwenye shule yangu ya ujana, mbona nilipata scores nzuri nikiwa nayo!
tulienda shule moja, tukawa tunakaa hostel moja, chumba kimoja, kuna mwenzetu nae alikuwa amefukuzwa kabla yetu tulikuwa nae pia...na kwa sababu wote ni PCM tukawa tunaenda shule na kurudi pamoja. nikawa ninaishi nae tu na kumwangalia kwamba mwamba amenisaliti na mpaka wakati ule hajaniomba hata msamaha. nikawa nimefukuzwa shule, wazazi waliumia sana. wakaanza kulipa ada na michango upya, kulipia hostel. nikawa nimekuja kwenye mazingira mapya, demu yule wa kule akanizingua akanitapeli na cm yangu Samsung S4, ile simu iliyokamatwa S3 rector akasema ile ni kama bangi ukikamatwa nayo hakurudishii (...mbali na hivyo alikuwa ana kinyongo na mimi,alikuwa hanitendeagi kama wanafunzi wengine...), kikawa ni kipindi kigum sana katika maisha yangu, ukiongezea na breakup ya huyo demu ambae nilidhani ananipenda sana, mahusiano yangu mimi nae kuvunjika labda nizingue mimi kwa kumuacha, f** her, akaniacha
Mungu akasaidia, nikamaliza ingawa sio kwa scores nzuri nikafanikiwa kwenda chuo kikuu fulani. kwa sababu scores hazikuwa zinang'aa sana nikapata course ambayo haikuwa ya ndoto yangu. nikamaliza chuo na sasa ninafanya kazi sehemu fulani kwa kutumia vitu nilivyojifunza chuoni. Kwa sababu kuna nafasi nyingi sana zikiwemo scholarships na paid international internships naona kesho yangu inayong'ara. nitasoma vitu ninavyovipenda kama masters na kuchanganya knowledge yake na nilivyovisoma na kuwa bora zaidi.
Kwenye maisha hauwi unayetaka kuwa. Kuna akina Yuda, akina Anita, wakubwa zetu ambao watafanya vitu ambavyo vitatuumiza ama kuharibu hali flani nzuri ambayo tulikuwa nayo, ila yote ni maisha. At the end pia Drake aliimba God's Plans: mapito yote tunapitia ili Mungu kudhihirisha ukuu wake maishani mwetu.
Ndefu sana ehhhh, nawasilisha.