Tuliowahi kukimbia mimba, karibuni

Tuliowahi kukimbia mimba, karibuni

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,957
Sitasahau kisa hiki, kipindi hicho nimemaliza shule ya msingi na kubaki mkulima tu kijijini kwetu, nikaanza kutembea na mtoto wa shule, hamadiii!! akapata mimba.

Siku hiyo mida ya jioni naona wazee wameongozana na yule binti, wakagonga hodi baba katoka, nikajua msala huu, nikapitia dirishani na kupotea, kesho yake nikatimkia kijiji cha jirani kwa mjomba wangu.

Nilikaa huko takribani miaka 3 ndo nikarudi nyumbani nikakuta nina katoto kabinti kazuri. Najutia kosa hili.

Karibuni wenzangu tuliowahi kukututwa na mkasa huu, ilikuwaje siku hiyo na kwa nini ukimbie? M

imi niliogopa kufungwa wakati huo sheria ilikuwa kali sana.
 
Kwahyo una binti mkubwa sasa,naomba umuwekezee kwenye elimu na umtimizie mahitaji
yake ili isije kumkuta kama yaliyomkuta mama yake.

safi sana kwa kumwambia hivi hapo akuna haja tena ya Kuendelea na comment umemaliza.
 
Hongera ila,
Kumkimbia mama mwenye mimba is such a crime aisee.... Yani sio fair kabisa apitie hicho kipindi peke ake!
 
Sitasahau kisa hiki, kipindi hicho nimemaliza shule ya msingi na kubaki mkulima tu kijijini kwetu, nikaanza kutembea na mtoto wa shule, hamadiii!! akapata mimba, siku hiyo mida ya jioni naona wazee wameongozana na yule binti, wakagonga hodi baba katoka, nikajua msala huu, nikapitia dirishani na kupotea, kesho yake nikatimkia kijiji cha jirani kwa mjomba wangu, nilikaa huko takribani miaka 3 ndo nikarudi nyumbani nikakuta nina katoto kabinti kazuuuriii. Najutia kosa hili. Karibuni wenzangu tuliowahi kukututwa na mkasa huu, ilikuwaje siku hiyo na kwa nini ukimbie? Mimi niliogopa kufungwa wakati huo sheria ilikuwa kali sana.

Wanaume wakweli huwa tunaukimbia umasikini tu,. Hatukimbii watoto!!!
 
Kukimbia mimba hodari!ndo nyie mwisho wa siku mtoto kawa na mafanikio hamkawii kujisogeza na kujitambulisha kuwa wee ndo baba yake!nina chukia sana wanaume wanaokimbia mimba.
 
mtunze mwanao kwa upendo mkubwa sana kwa maana mama yake alipitia magumu wakati wa ujauzito ulipomtelekeza...

tna umwombe na mwanao msamaha kwa kumtelekeza
 
dada yangu, si ndo nimeomba msamaha na kujutia kosa hili jamaniiiii.
 
mtunze mwanao kwa upendo mkubwa sana kwa maana mama yake alipitia magumu wakati wa ujauzito ulipomtelekeza...

tna umwombe na mwanao msamaha kwa kumtelekeza

nitaufanyia kazi ushauri wako dada yangu.
 
Hongera ila,
Kumkimbia mama mwenye mimba is such a crime aisee.... Yani sio fair kabisa apitie hicho kipindi peke ake!

Naomba nisamehewe wajameni.
 
Kwahyo una binti mkubwa sasa,naomba umuwekezee kwenye elimu na umtimizie mahitaji
yake ili isije kumkuta kama yaliyomkuta mama yake.

kweli mkuu, sifanyi kosa tena, asante sana kwa ushauri wako.
 
Back
Top Bottom