Tuliowahi kukutwa na ushamba mara baada ya kununua gari kwa mara kwanza tukutane hapa

Baby lock, mafundi magari ni sawa na mafundi electronics wanapiga hela za bure kutokana na watu wengi kutokuwa na ABC za vitu husika.
 
Mara ya kwanza, kabisa nipo zangu na Corola yangu, siku ya tatu tu, toka nimeletewa toka DSM!

Nikawa nimekaa ndani, nimefunga door na window zote, nakula kiyoyozi! Sasa kuna jamaa ni mtani wangu, akachukua maji akiwa kwa nje, akamwaga pale kwenye wind screen, aiseee,nilikwepa kama vile yanaingia ndani! Jamaa alicheka sana, akasema kweli wewe hizi mambo ni ngeni kwako.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23]
 
Ile nimefika destination sijaweka parking nang'ang'ana kutoa ufunguo, aisee nilipambana weeee ngoma haitoki, ile nagundua sijaweka parking kijasho tayar!

Next time nimewasha taa ya kumulika ndani, sijaizima wala nini nikafunga gar nkaenda kuangalia mpira. About two hour ngoma inavuta betri tu.

Kisanga kingine namaliza kupak nimetoa ufunguo, ile nazungusha steering kidogo tu, ngoma inajilock. Hapa kwanza nilikaa nkatulia nkapata wazo la kuingia google. Case solved.

After those, ushamba wa gari wote ukaishia hapo.
 
Uwe na balance ya kama shiling ngapi ndio ununue gari au uwe na kipato cha shiling ngapi kwa mwezi na mwaka ndio ununue gari nijibu
 
Mimi na bro tuliiba gari ya mshua ilikua RAUM old model kipindi hiko ndio nyukwaaaa.... Tukawasha AC kali kufika kijitonyama play ground kuchungulia chini tunaona gari inavuja oil tukasema tumepasua sample.... Almanusura tuite fundi. Kumbe ni maji ya AC ndio yanatema. Bila kunusa yale maji tungeliwa na fundi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…