Tuliowahi kukutwa na ushamba mara baada ya kununua gari kwa mara kwanza tukutane hapa

Tuliowahi kukutwa na ushamba mara baada ya kununua gari kwa mara kwanza tukutane hapa

Siku Moja niliomba bei ya gari hizi kwenye showroom za dar es salaam.
1.IST.
2. Vts.
3. Volvo
4. Carina TI.
5. Volts.
6. Suzuki.
7. Nadia.
8. Balloon 4pistons.
9. Gx100
10. Corona old model.
11.Allexes.
12. Premio old model.
13. Wish.
14. Verosa.
15.Juke
16.altezza
17. Alfaaard
18. Volkswagen toleo la sasa.
19. Allions

Naomba Msaada
Mbona gari yangu pendwa honda crosroad haipo kwenye hii list wala wadau hawaizungumzi kabisa, hii ndoa katoliki bila shaka.
 
Baby lock.mafundi magari ni sawa na mafundi electronics wanapiga hela za bure kutokana na watu wengi kutokuwa na ABC za vitu husika.
Tungeyajulia wapi haya mabebiloki kama sio JF, leteni uhondo wadau.
 
Ilikuwa mwaka 2010 nina siku mbili tangu kupokea toka bandarini gari RAV 4 Old model. Kabla ya hapo nilikuwa namiliki corora box body manual. Ilikuwa asubuhi najiandaa kwenda ofisini. Nimeitoa kwenye packing na kisha nikaizima na kwenda kumalizia kujiandaa. Kumbe wakati natoka nilitwist steering ikajipiga lock steering. Wakati nataka kuwasha kila nikinyonga ufunguo naona kuna ugumu haijipigi. Hata switch on hakuna. Pigia fundi moja na kumwelezea akasema hiyo steering imejilock ili kuondoa lock twist steering huku ukiweka switch on. Aisee ilikuwa ni sekunde tu nilijiona mshamba sana. Kuja kukutana na fundi akanambia kuna jamaa alishawahi acha gari bar asubuhi akaenda na fundi kumbe steering lock.
 
Kuna siku nilizima gari bila kuweka parking gear, nikahangaika kutoa funguo hadi jasho likanitoka. Kwa kuwa nilikuwa nyumbani niliacha gari na ufunguo nikalala hadi asubuhi. Nilivyojaribu tena kuutoa ufungua ndio nikagundua gari iko kwenye gear.

Ushamba/ujinga ni kitu cha kawaida kwa binafamu.
 
Aisee ki IST kiligoma kuwaka kumbe kilikuwa kwenye gia hahhahaah... Nikampigia fundi nikiwa na wazo betri limechuja.... Lahaula kusukuma sukuma gear lever nawasha ngoma ipo hewani..... Nilizima simu kwanza fundi asinidai ya boda boda
[emoji23][emoji23]Hii ilimsumbua Anko wangu mmoja baada ya kununua Nadia,yupo wilayani akaenda misele mtaani akazima gari akaacha kwenye gia kila akijaribu kuwasha haiwaki akahisi mafuta yameisha akaita dogo mmoja aende kununua kwenye kidumu analetewa anajaza,akijaribu haiwaki anaagiza tena,kaagiza kama mara nne hivi ngoma haiwaki,mpaka yule jamaa wa sheli akashtuka

Bahati nzuri Madogo wa home walikuwa wanapita maeneo hayo na gari wakamkuta ndio akawaambia Mjomba hii gari imegoma kabisa kuwaka naona mafuta yatakua bado yapo chini,chukueni dumu mkaongeze,walipocheki wakaona ipo kwenye gia wakatoa na kuiwasha kucheki gauge ya mafuta mshale upo Full,walicheka sana,wakati wanaijaribu wakaenda chemba ili wanyonye mafuta,kuingiza mrija wakakuta tank la mafuta lina chujio,bila hivyo wangeyanyonya[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Ilikuwa mwaka 2010 nina siku mbili tangu kupokea toka bandarini gari RAV 4 Old model. Kabla ya hapo nilikuwa namiliki corora box body manual. Ilikuwa asubuhi najiandaa kwenda ofisini. Nimeitoa kwenye packing na kisha nikaizima na kwenda kumalizia kujiandaa. Kumbe wakati natoka nilitwist steering ikajipiga lock steering. Wakati nataka kuwasha kila nikinyonga ufunguo naona kuna ugumu haijipigi. Hata switch on hakuna. Pigia fundi moja na kumwelezea akasema hiyo steering imejilock ili kuondoa lock twist steering huku ukiweka switch on. Aisee ilikuwa ni sekunde tu nilijiona mshamba sana. Kuja kukutana na fundi akanambia kuna jamaa alishawahi acha gari bar asubuhi akaenda na fundi kumbe steering lock.
Hahahaa ilishanikuta hii jasho lilinitoka

Sent from my CPH2015 using JamiiForums mobile app
 
Daah nakumbuka nilishindwa kufungua boot la Crown mpka nikaita fundi
Duh! Ya kwangu button yake mlangoni imekufa bila kujua siku nimepata pancha sijui nafunguaje. Niliokuwa nao hawajui pia. Nikachukua jeki na spana kwa mtu nikafungua tairi nikapeleka likazibwa nikarudishia. Kesho kwa fundi kurekebisha button na nikamsimulia kilichonikuta jana akanionesha wapi kitundu cha kufungua manually na ufunguo. Kimefichwa sana nacho!
 
Nimejifunza kuwa tunatakiwa kukubali kwamba vitu ambavyo hatujavitengeneza sisi lazima kuna wakati vinatutoa ushamba kwahiyo tukubali kujifunza na kuomba ushauri kwa wenye uzoefu navyo.

Unaweza ukaharibu gari kizembe kisa hutaki kukubali kutolewa ushamba au kuongia gharama zisizo na maana
 
Nimezoea toyota, mwaka 2018 nimeazima gar la jamaa ni benz nikapitia kituo cha mafuta kuongeza mafuta nikafika naanza kutafuta pakufungulia mfuniko wa mafuta google ilinitoa ushamba hata handbreak yake ilibidi nigoogle
 
Back
Top Bottom