Same kwangu. Nimefeli kabisa. Na huwa sipo comfortable kuwaambiwa watu maana nikiwaambia wanaanza kunielekeza na kunifanya nihisi nakosea jambo ambalo huwa linanikwaza sana.
Kuna jamaa nilikosana nae sababu ya kunielekeza namna ya kutumia mguu m'moja tukiwa barabara kubwa ilibakia nusu nimshushe ila malaika wa MUNGU walikuwa karibu wakanituliza hasira zangu.
Jamaa alikuwa tu si mtulivu, amekaa anaacha kuwa busy na mambo yake nashangaa ananiuliza, "unatumia miguu miwili kukanyaga pedals, hatari sana hiyo" akaongea kwa namna ya kuhamaki sana aisee hadi nikapanic kimya kimya ingawa sikumuonyesha hiyo hali ya kupanic nikajikaza.
Halafu anakazana kukulekeza dah nikajikuta namuuliza swali moja tu, kuwa mimi naendesha gari tokea 2003. Miaka yote hiyo gari zote nimekuwa nikiendesha kwa mtindo huu, hayo unayosema si yangeshatokea mbona sijawahi kujihisi nafanya jambo la hatari na jambo la zaidi ni kuwa ninakuaa na confidence zaidi nikitumia miguu miwili kuliko mguu m'moja?
Akanikazania, "sawa endelea kuwa mbishi, unaambiwa unakosea unabishana na wataalamu wa sheria za barabarani" dah nikajifeel vibaya sana yale maneno yalinikata stimu ila nikamindi zaidi kwa huyu mtu nimempa lift na mimi ndie mwenye mali why mtu anipangie. Nikavumilia nikajua huyu tunakorofishana tu nikiendelea na mjadala wacha nikae kimya upepo mchafu upite.
Kwahiyo hii kitu naona watu wengi hawajaifanyia tafiti kama vile miaka ya nyuma ilivyoaminika kuwa watu wote hutumia mkono wa kulia tu na sio wa kushoto. Kumbe tafiti zilipofanywa ikaja kuonekana kuna watu mikono ya kushoto ndio main na ya kulia sio.
Ila yote kwa yote huwa nachukia sana mtu anaeingia kwenye gari nakuanza kunilecture as if huwa ananiendesha yeye kila siku. Huwa nachukizwa sana na hii tabia. Maana hata mimi nikipanda gari ya mtu huwa natulia tuli na naongea mambo mengine ya kumfanya dereva awe comfortable kuendesha na kufurahia kuwa na aibiria ambaye wanashare story.