Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Mi kila nikikumbuka ajali zote inabidi nilie tu, maana nashindwa hata kueleza[emoji30] [emoji31] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]
 
Ameni wengine wameokokaa kabisaa baada yakunusurikaa katika ajali. Ukutee hataa wewe ulikuwa mpiga zengwe ilaaa uchenjuajii ndo ukakufanyaa ukamjuaa MUNGU

Sent from my Infinix NOTE 3 using JamiiForums mobile app
 
Mungu mkubwa,Pole naamini ukipita hapo huwa unakumbuka hiyo ajali.
 
Mimi nakumbuka mwaka 2010 natokea Tanga naelekea Dodoma nafika Moro basi kagoma break tukaenda kulivamia fusso nakumbuka kilichonisaidia ni mkanda lakini watu wengi walipasuka uso na kung'oka meno. Wengi safari yao ikaishia moro wakapelekwa hosp sisi tuliopona tukaendelea na safari.
 
Nilikuwa natoka Mkoani kwenda Dar. Nikalala Singida. Kesho yake mchana nikaanza safari tena. Kucheki vile vibao vya barabarani naona 215km to Dodoma. Nikawaza hapa nikitambaa at least 120km/hr, ntapata lunch yangu Dodoma.

Katikati ya Ikungi na Isuna nilikula booonge la mzinga. Nakumbuka nilikuwa at 140km/hr. Taili la nyuma mkono wa kulia liliburst na kwa kutokuwa na uzoefu nikadhani nimegonga mtu. Kosa lilikuwa kupiga brake maana gari liliyumba mara tatu na kubiringita kwenda porini.

Namshukuru Mungu niliumia mguuni na kifuani tu japo niliambiwa nilizimia kwa karibu robo saa. Gari ilikuwa third party na written-off completely maana niliuza engine tu. Baada ya kuzinduka nilishuhudia watu wakiniibia vitu. Niliambulia kuokoa simu yangu moja, laptop na wallet yangu - thanks to some truck drivers walioona mchezo wote tangu ajali ilipoanza.Tangu siku hiyo I am no longer a fan of speeding. Nawapaga site wote wanaoomba kunipita. I really thank God kwa kuniponya kwenye ile ajali.
 
Menopause imekujia vibaya.
Em kakae na zilipendwa wenzako huko
 
Mungu mkubwa,mmh wewe si wa kawaida una maono!
 
ajali nyingine mwaka huu january natokea Mwanza naelekea Moro katikati ya mapori hukohuko Morogoro gari likaanza kutoka moshi na baadae cheche za moto zikaanza kuwaka.. nakumbuka tuliruka kabla hata gari halikusimama vizuri ilibaki kidogo tu gari lingewaka moto ila ni kwa neema tu ya Mungu. tulilala humohumo porini hadi kesho yake basi likafanyiwa matengenezo tukaendelea na safari.
 
Pole duh!
 
mwaka 2013 nlipata ajali sitasahau nlikuwa coma kwa Sikh tatu Gari ilianguka n lucky enough mi mwenyewe ndo nlisurvive nikipitaga hilo eneo hadi leo nasisimka
 
Ameni wengine wameokokaa kabisaa baada yakunusurikaa katika ajali. Ukutee hataa wewe ulikuwa mpiga zengwe ilaaa uchenjuajii ndo ukakufanyaa ukamjuaa MUNGU

Sent from my Infinix NOTE 3 using JamiiForums mobile app
Mkuu mimi nina hofu ya Mungu hata kabla ya hizo ajali, labda niseme nimezidi kumpenda sanaaaa sanaaaa maana nimejua kuwa anapigana na wanaopigana nami usiku na mchana.
 
Nakumbuka mwaka 2007 nikiwa Mwanza nilikua naendesha Mark 11 nikiwa na wapambe wananichochea nionge mwendo sikujua nini kiliendelea gari iligonga ukuta wa nyumba na ikageuka ikaangalia ilikotoka gari iliaribika sana bosi hakunielewa zaidi alitaka gari yake itengenezwe na muda gari ikiwa gereji natakiwa nimlipe elfu 15 kila siku maana ilikua tax basi nikaona isiwe tabu nikakimbia Mwanza kwenda Dar mpaka leo nakala maisha

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 
Uzi huu niutumie pia kumshukuru Mungu aliniokoa nilipopiga mweleka nikiwa na pickup (speed 160km/hr). Ilikuwa ni baada tu ya kumuonya dereva wangu kuwa barabara ile ina kona nyingi. Gari ilipinduka tukiwa wote tumefunga mikanda wala hatukuumia. Nadhani pale Mungu alituokoa kwa namna ya ajabu.
 
Kuna uzi humu unasema kuwa kuna member wa JF ambao ni majini.
Nadhani utakuwa unakuhusu.
Uko wapi huo Uzi niwajue vizuri ,maana unafikiria Maneno mengine mtu anacomenti unajiuliza ivi huyu ni binadamu Wa kawaida kweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…