Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ameni wengine wameokokaa kabisaa baada yakunusurikaa katika ajali. Ukutee hataa wewe ulikuwa mpiga zengwe ilaaa uchenjuajii ndo ukakufanyaa ukamjuaa MUNGUMimi leo nipo hai ni Mungu tu amependa niwepo hai, nimenusurika katika ajali mara mbili ndani ya mwaka mmoja. Ajali ya kwanza ya pkpk ya pili gari yangu aina ya Noah mpka leo gari iko juu ya mawe but mimi natembea nikiwa mzima na viungo vyangu vyote, isipokua nina makovu mawili matatu. Hakika ninamrudishia Mungu shukurani za moyo wangu na ninampa sifa na utukufu kwa ajii ya uzima wangu. NARUDIA TENA NI MUNGU BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO AMEPENDA MIMI NIENDELEE KUWA HAI....I glorify you The Most High God in the name of Jesus Christ!!!
Ajali njia ya MSATA bagamoyo karibia kabisa na geti la maliasili SAA NNE usiku, nikielekea Dar, kwenye zile daraja zisizo na kingo niliona kabisa daraja linahama na katika kulikwepa .......ne next moment nilijikuta chini ya daraja gari ikiwa imegeuka juu chini
Nilitoka mzima bila jeraha kutokana na aina ya gari niliyokuwa nayo... Ingekuwa mjep sijui kama ningesalimika
Ilikuwa 2013 siku masaa machache kabla ya IDD
Ni siku ambayo asubuhi yake kuna NOAH ilipata ajali njia hiyohiyo na kuondoka na roho nane hapohapo[/QUO
Menopause imekujia vibaya.Uzi wa kijinga huu Sijapatapo kuona.
Ajali badala kumshukuru Mungu upo salama nyie mnatangaza hapa.
Mnapeleka ujumbe upi kwa wale waliiondokewa na ndugu, jamaa, marafiki, watoto, wazee wao kwenye ajali?
Mnapeleka ujumbe upi kwa wale waliolemaa maisha kwa ajali?
Huu uzi ufutwe, ni upumbavu wa hali ya juu kuuwacha hapa.
Mungu mkubwa,mmh wewe si wa kawaida una maono!Ilikuwa mwaka 1997 tunasafirisha maiti toka Dar kwenda Iramba mkoani Singida tulifika salama Dada akaniambia tushukuru tumefika salama pale pale nikawa mnyonge sana nikajikuta namwambia ila wakati wa kurudi tutaanguka na gari sijui kwa nini nilisema hivyo Dada akanikataza nisiseme hivyo Mimi nikamjibu kweli Dada. Tukazika na kuanza safari ya kurudi ile tunaanza safari nikamwambia Dada laaaah tunakwenda kuanguka masikini sijui tufanye nini? Dada akaniambia usimsemee hivyo nikamwambia kweli. Kutoka Singida tukafika pale ambapo ukinyoosha unakwenda Arusha ukikata kulia unapitia Dodoma mkuu wa msafara akamwambia driver nyoosha tupite ya usandawe ilikuwa ni jioni Mimi nilikuwa kiti cha pili nyuma ya driver nikamwambia driver kwa sauti kata kulia pita ya Dodoma, driver akauliuliza nimsikilize nani? Nikamwambia Mimi, mkuu wa msafara akasema nyoosha halafu akaniuliza kwanini umesema hivyo ile sauti ya kufoka nikamjibu Barabara zote mbili tutaanguka hii ya Dodoma tutapata msaada hii ya usandawe nani atatusaidia? Kanijibu hoja dhaifu driver nyoosha, nikamwambia Dada naogopa ajali Mimi nalala nisione tunavyoanguka, Dada akasema usiseme hivyo mdogo wangu nikamwambia kweli dada, nikalala muda mrefu baadae nikastuka nikamuuliza Dada hatujaanguka? Akaniambia wewe, nikamuomba nikae upande wa dirishani aliponipisha nikamwambia nalala Mungu atunusuru jamani, nikalala kama saa tatu usiku hivi nikastuka usingizini gari inayumba vibaya sana mara tukaanguka ni kiza kinene, mvua inanyesha na tupo porini peke yetu watu wakatokea madirishani maana mlango upo kwa chini Mimi nikawa nimebanwa kidogo na kiti cha mbele yangu halafu na ule usingizi nikaamua nilale tu, kule nje wakagundua sipo ikabidi waanze kuniita kuchungulia Giza nikawaambia sitoki wakanibembeleza nikatoka nina hasira ile mbaya siongei na mtu. Mkuu wa msafara akamfuata driver anataka kumpiga Mimi nikamwambia nilikwambia tukiwa Singida ukanidharau hakuna msaada hapa nyanyueni gari tuondoke, ikabidi wafanye hivyo huku wanalalamika maumivu Bahati nzuri iliwaka tukaondoka kweli Mungu ni Mkubwa yaani ukiona hiyo gari huwezi Kuamini kama itatembea na haikuua Ila majeruhi, kufika Dodoma tukabadilishiwa usafiri. baada ya muda nikawa na maumivu ya mgongo, hizi zingine ambazo ni mbaya zaidi kwangu nazihifadhi Ila Mungu ni Mkubwa kisichokuwa kikupate hakikupati
Hapana mkuu ilitokea tuMungu mkubwa,mmh wewe si wa kawaida una maono!
Pole duh!Nilikuwa natoka Kigoma kwenda Dar, driving my RAV4 Old Model. Nikalala Singida. Kesho yake mchana nikaanza safari tena. Kucheki vile vibao vya barabarani naona 215km to Dodoma. Nikawaza hapa nikitambaa at least 120km/hr, ntapata lunch yangu Dodoma.
Katikati ya Ikungi na Isuna nilikula booonge la mzinga. Nakumbuka nilikuwa at 140km/hr. Taili la nyuma mkono wa kulia liliburst na kwa kutokuwa na uzoefu nikadhani nimegonga mtu. Kosa lilikuwa kupiga brake maana gari liliyumba mara tatu na kubiringita kwenda porini.
Namshukuru Mungu niliumia mguuni na kifuani tu japo niliambiwa nilizimia kwa karibu robo saa. Gari ilikuwa third party na written-off completely maana niliuza engine tu. Baada ya kuzinduka nilishuhudia watu wakiniibia vitu. Niliambulia kuokoa simu yangu moja, laptop na wallet yangu - thanks to some truck drivers walioona mchezo wote tangu ajali ilipoanza.Tangu siku hiyo I am no longer a fan of speeding. Nawapaga site wote wanaoomba kunipita. I really thank God kwa kuniponya kwenye ile ajali.
deep-----BEEPUnideep cm niliporwa na wenye nguvu
Mkuu mimi nina hofu ya Mungu hata kabla ya hizo ajali, labda niseme nimezidi kumpenda sanaaaa sanaaaa maana nimejua kuwa anapigana na wanaopigana nami usiku na mchana.Ameni wengine wameokokaa kabisaa baada yakunusurikaa katika ajali. Ukutee hataa wewe ulikuwa mpiga zengwe ilaaa uchenjuajii ndo ukakufanyaa ukamjuaa MUNGU
Sent from my Infinix NOTE 3 using JamiiForums mobile app
Huku ni JF lakini sio FBHuna kaz ya kufanya
Uko wapi huo Uzi niwajue vizuri ,maana unafikiria Maneno mengine mtu anacomenti unajiuliza ivi huyu ni binadamu Wa kawaida kweli!Kuna uzi humu unasema kuwa kuna member wa JF ambao ni majini.
Nadhani utakuwa unakuhusu.