Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Miaka 3 iliyopita nililima eka 40 za mpunga na 30 za mahindi nilipokuja kuuza mazao niliingiza faida ya mil 55 ukitoa na pesa ya mtaji.

Leo tar 1 nina laki moja tu, wanawake sio viumbe vya mchezo na kazi nimefukuzwa niliowasaidia wamenitupa. Nimejifunza mistake zote nilizofanya ila nikikumbuka naumia mno..kwa vile nina nguvu sina ulemavu naendelea kupambana.

Nimerudi home kwa wazazi maana hali ni tete ninaweza kuwa tahaira
 
Pole mkuu
 
Bora utajiri wa kuwekeza kuliko utajiri wa pesa,maana zikianza kupukutika utasema umerogwa
 
Kati ya watu usiotakiwa waamini na kuwasaidia, ni watu wanaokuwa karibu na wewe ukiwa na hela. Siku zikiisha watakusema na kukuona haufai.

Sidhani nitakuja saidia mtu maana wengi wao wanakugeuka na kukusema vibaya mambo yakienda ndivyo sivyo. Bora hiyo hela ukaipeleke kanisani kuliko kumpa ndugu mnafiki pale ukifuli

Hao unaocheka nao na kula nao raha ndio watakucheka baadae....
 
Pole sana mkuu,mimi mpaka leo sina rafiki hapa napofanyia kazi zangu maana nipo mbal na Nyumbani,urafiki na kazi yangu siutaki kabisa,kampani za kwenda kuzungusha bia baa siutaki,maana nashukuru nami si mtumiaji wa kilevi, nahitaji urafiki wa kimaslahi na siyo wa kinafiki, japo marafiki wa ukwel hawakosekani ila ni wawili tu na wapo mbali, nikiwa na shida tunasaidiana pamoja na huo umbali
 
Sure mkuu.... balaaa sana unaowasaidia wanageuka maadui kabisa...
 
Nimesoma michango ya watu huku nikajifariji kidogo kuwa sikuwa nyang'au mwenyewe...nilikuwa na raman yangu ya utalii Arusha kila kwa siku nikipiga dili haramu sikosi chini ya $500 nikageuka papaa na wapambe kibao na demu matata kwenda moshi ni tax au Karatu tunachukua Noah private ...siku za game za UEFA kinywaji ni Heineken kwa yeyote atakayejipendekeza ...siku za kawaida ni Jack Daniels home kwa maza sifiki ....namnyamazisha na kumwekea pesa pesa bank ...kitu mwanamke alinifanya sitakaa nisahau baada ya kuishiwa..alichukua kila kitu cha ndani na polisi akanipeleka ...kutoka kwenye JD nikarudi kwenye viroba.

Uzuri nilikuwa nashamba kubwa nikauza nikajirudisha kwenye raman japo mapicha picha kibao ya maden kwenye bar nilizokuwa na sign bill ..pesa ukiwa nayo na mwanamke na marafiki wa mteremko ni shida kubwa....nshawah tumia 1 m bar kwa siku moja na dem anachekelea tu.
 
duuh pole mkuu
 
Hapo kwenye ndugu mkuu pagumu kweli kitanzania, sijui mtu unajitoa vipi maana ndugu wengine ni wale wakaribu kabisa.
 
Mkuu naamini ukirudi kwenye kilimo utafanikiwa tena, jipange upya, mara nyingine hizo ni blessings in disguise.
 
Hapo kwenye ndugu mkuu pagumu kweli kitanzania, sijui mtu unajitoa vipi maana ndugu wengine ni wale wakaribu kabisa.
Inabidi tu mkuu maana maisha ni yako,ukiwa mchanga kwenye kutafuta hela ogopa sana ndugu.ndugu wanaweza kukufilisi kisha hao hao wakakucheka ila kama umeshajijenga vya kutosha unaweza kutoa msaada ili kuondoa lawama ila mtaji wako wa mill15 au 20 uanze kusaidia watu nakwambia utageuka kituko.
 
Kama nakufahamu hiv ,,si ulikuwa ukikuta malaya wa concord kwa anayekujua unamgawia elfu 10-20 ..ulikuwa unajiita jina flan hiv la dawa hedex kama sijakosea? Bora zilikuwa zako mana nilisikia ulifungwa kwa kuiba hela za ofis kumbe zilikuwa n zako na pikpik yako ilikuwa boxer nyeusi ,, mrefu ,mweusi mwembamba kiasi ,mkimya sana ! Tuanzie hapa nikukumbushe vingine
 
Ha ha ha,nilikua na kikazi kimoja kila siku hela ya maji ya kunywa 100,000 na kuendelea,
nakumbuka nimekula ulabu toka 2000-2010 non stop daily,

kweli pombe sio chai jameni,acheni nilime haya majaruba tu

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umenipa courage, sifikirii tena mpunga niliopoteza,kila cha moto nakiona
 
Pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…