Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

mimi ndo ngedere kabisa nilifanya kazi kwenye kampuni ya gas ndan ya miaka mi3 nilipata kama milion 10 nikanunua pikipki yakutembelea nikawa kazi yangu kuwafata mademu na kwenda kula bata beach demu nikimpata mtandaon hata awe anakaa kibaha namfata na pikipiki kiukwel sikuamin kama ile hela ingekuja kuisha nilikuwa naiona nyingisana kumbuka mii nmetokea familia ya kimasikin iv nnavyoandika hapa nmerud naish hom kwa baba na mama sina hata mia mfukon
Nimependa ulivyojiita ngedere[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kila nikionaga hii comment mi mbavu sina[emoji16][emoji16]

Mkuu unaendeleaje na biashara ya mbao?

@Dianaspencer Jah is by my side mambo yanaenda btw nakuja Pm kukuchokoza
tapatalk_1548247973869.jpeg
 
Duuh!

Mwanzoni mwa mwaka huu 2019 nikiwa sina muda mrefu sana kazini nilichukua mkopo wa 4,000,000/= kama staff. Mkopo huu ungekatwa kidogo kidogo kutoka kwenye mshahara wangu.

Mwanzoni nilijiaminisha sana kuwa nitafanyia biashara wazo nililokua nishaliulizia sana na kupata information za kuridhisha. Biashara hii kwa data nilizokusanya kwa wengi wanaoifanya ingenipatia angalau 15,000 - 20,000/= kila siku.

Nakumbuka nilikua nimeshamuambia jamaa mmoja ambae ameifanya biashara hiyo muda mrefu kuwa anitafutie wapi nitanunua vitetendea kazi kuna hela nitaipata hivi karibuni na akawa yupo standby. Kwakwel nilikua sitaki kupoteza muda sana kukaa na ile hela nilihofia itapotea. Plan zote nilishachora na nilikua najua kuwa vitu vikinyooka, baada ya kuulipa ule mkopo wote nitakua nishatengeneza faida kiasi gan. Kila kitu kilikuwa kimesetiwa kasoro account ya benk tu ndo ilikua haijasoma bado.

Mkopo ulipomaliza process ukawekwa kwenye account yangu. Asikuambie mtu, kuona zile sifuri sifuri tano, yani millioni na ushee kwenye balance yako ya benki kwa mara ya kwanza ni raha isiyoweza kuandikwa. Yani unajihisi tofauti. Ukiangalia balance unaona hii haiwezi kuisha nikitoa hapo 50k kununua kitu flani. Mdogo mdogo number zinaanza kushuka. Unasahau kabisa mipango yako. Nilikua naona iliyobaki mbona bado inatosha. Sina hofi natoa tu hela bila kuangalia balance

Kabla hata sijajinunulia kitu cha maana, wala kuwatumia wazazi wangu hela, nilimnunulia mpenzi wangu kitu flan cha gharama zaidi ya laki 4. Nilikua najiaminisha kuwa nampenda, na kusema kweli tabasamu lake pale ninapo mnunulia kitu huwa lilikua linanifanya nijione mimi ndo mwanaume haswa, siku hizi mwanaume pesa!

Zikaisha wiki kadhaa, hela ile ikawa imefika karbia nusu. Hapo nahitaj tena kulipa kodi, nikatoa na kodi humo humo, ikawa inazidi kupungua tu. Yule jamaa sikuwahi tena kumcheki kuhusu ile biashara na plan zote zikaota nyasi. Biashara sikuifanya wala kuiulizia tena tangia hicho kipindi. Wanaosema wakipata hela hawato filisika. Unaweza ukahisi unajijua vizuri wakati huna hela. Lakini ukiwa nazo unaweza ukawa mtu tofauti kabisa. Omba sana uwe na uwezi wa kujicontrol.

Ilifika muda sipendi hata kuangalia balance langu la ATM. Kila nikitoa pesa atm ni kama bahati nasibu, nikisiki pesa zinafanya priiiiiiiiiiiii nafurahi maana nilikua sina uhakika kama zitatoka. Kufilisika ni kubaya jamanj asikuambie mtu. Nimiezi kadhaa sasa imepita, hivi leo ile biashara ingenyooka ningekua nimeingia zaidi ya 1,500,000 lakini sasa hivi kila mwezi nakatwa zaidi ya laki 7 kama makato ya marehesho ya mikopo ambayo mengine imeongezeka kwa kua zilivyoanza kukatwa na hela tayr imeisha maisha yanakua magumu sana.

Ninavyoandika hapa, nataka nikope nipate hela ya kumalizia hii wiki nikisubiri mshahara mwengine. Maisha yamekuwa magumu mno. Najutia mengi sana, pesa yote imeyeyuka.

Nilichojifunza ni kuwa, tengeneza plan yako kabla hujapat pesa. Utakapo ipata tu! Anza muda muda huo huo kutekeleza kwanza plan zako, halaf kinachobakia tenga kidogo uienjoy. Yani usifikirie mara mbili. Ukianza tu kujifikiria ukiwa na hela, hapo hafikirii mtu yule yule ambae alikua hana, anafikiria mtu mwengine kabisa ambae ana pesa na wewe humjui huyu mtu kwahyo usimsikilize hata nusu. Fanya kwanza yenye faida.

Napia jambo jengine na la muhimu, hata kama ni mbaya vipi, angalia balance yako ya hela mara kwa mara. Unaweza jishtua mapema unatumia pesa vibaya.

M/Mungu nipe nguvu haya makosa nisiweze kurudia. Sijakata tamaa, Sasa hivi najua ukipata hela usipoiwekeza mapema kwa akili itaisha bila mpangilio. Na utaishi maisha magumu kuliko mwanzo.
 
Daah wee jamaa kama mm tu..semaa mm bahat nzuri nlikumbukaa kununua tuvitu tangible ambavyo tunanifarij hadi sasaa..kalaptop na kapikpik kidogo..vinamifarij..japo mm pia kuna biasharaa nilifunguaa ilaa ikafaa..shida usimamizi..bt vile vitu vya biasharaa bado vipo..asikwambie mtu kwa sisi ambao hatujazoea kushika ela nying..mkopo ukiingiaga mkubws tunachanganyikiws kweli yan..mimi nilisafir had mikoa ambay ckuwah fika yotee hyo jeuri ya fwezaa dah..leo hii.
 
Back
Top Bottom