Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Yote ni kushika pesa mikono yako haijazoea kushika

Mfano umezoea kuwa na laki to laki tatu ndo unaweza ibalance then unakuja shika milion kumi mara nyingi sana itaisha ikibaki laki ndo unapata akili

Nakumbuka nikiwa bado chuo sikuwa nimewah shika laki tano kasoro yangu kwa mkoa ule ambao bajet ya mtoto wa kiume milo mitatu ni 2500 kwa siku

Nikapiga zali moja nikapata 480k asee nilibadilika pesa mfukoni zipo nikabadil milo ..et siwezi kula wali nyama mkavu bila soda 😁 wakati mwanzo wali marage tupu daaa ..ile pesa sijui iliishaje
 
Nitatoa uzi mdaa sio mferu niliingia dsm kizembe na mtaji Wa 2 million baada tu ya Ku graduate, after 2 weeks sikua hata na mia mbovu na mzee kipindi ananipa huo mtaji alinipa husia kwa masaa 7 na kunambia tusijuane tena so pambana. Na Mimi baada ya mtaji kuisha hata sikurudi nyumbani 😁😁 kilichoniokoa ni ajira serikalini walitangaza nikaotea.
 
Huu uzi kweli kiboko! nilijua ni Mimi mwenyewe kumbe tupo wengi sana.
Nimemaliza chuo kikuu mwaka Jana Basi mzee akanipa M3, M1 nimsaidie kukarabati nyumba yake na zingine nione nafanyia nini, Sasa mimi kweli nyumba yake nikakarabati sasa hela iliyobaki nikawaza nijengee kijumba kwenye kiploti alichonipa nifanye masuala ya ujasiliamali hapo.

Mpaka sahizi lipo pagale lililoezekwa tu, na hela imekata sina ramani niponipo tu, lakini kila nikiangaliaga matofali yalivyopangika kwenye kijumba napata nguvu kwamba angalau sijaipoteza bure Kuna kitu nimefanya.
Hujafilisika ila umewekeza.
 
Ahsante Mkuu, Ila unapowasoma wahusika na matukio mbalimbali yaliyowatokea ni exprience nzuri kuliko mawazo ya mtu mmoja yaliyowekwa kwenye kitabu,Mwandishi anaweza asipate exprience tofauti tofauti kama Live exprience toka kwa wahusika, Hii inavutia sana na wasio na uwezo wa kununua vitabu wanajifunza kwa gharama nafuu na uhalisia sana, wengi wamekuwa sio wachoyo kwenye kufunguka.
Mimi hapa nishapata wazo,

UONGOZI WA JF,AU YEYOTE ANAYEWEZA AFANYE KUPRINT UZI HUU KTK NAKALA NGUMU.KILA PAGE 1 YA HUMU NA KULE INAKUWA NI KURASA MOJA AU ZAIDI.MWISHO ZINAPATIKANA KURASA ZAIDI YA 100 NA KINAKUWA NI KITABU KAMILI(JINA LINABAKI KAMA KICHWA CHA UZI KILIVYO)
TAFADHALI FANYENI KITU KWA AJILI YA VIJANA WAJAO!
 
Mwaka 2011 soko kuu mwanza nikiwa ninauza nafaka zikiwemo karanga, njugu, choroko,dengu,ufuta,ulezi,uwele,mtama,maharage na kunde.

Kamtaji kalivyokuwa nikawa naendea karanga tabora tani kadhaa nauza jumla. Nilipata pesa kwa njia hiyo. Basi kufkia December karanga zikawa chache Sokoni hivyo mwenye nazo alipiga pesa balaa.

January 2012 nikaingia poli kusaka karanga mpya ili niwahi bei sokoni. Basi nikapata kama gunia 30 (tani 3). Kufkisha Sokoni ziligombaniwa kama nyama. Nikaona pesa si hii apa. Nikazoa msingi wote around kama 22.8m. ili nikapige mkupuo mmoja nije nitulie.

Kuleta mzigo nafika Sokoni nakutana na fuso 6 zinashusha mzigo. Sasa kila mmoja ashajua ni dil acha bei ishuke. Nilijikuta karanga nimezinunua 2300 natakiwa niziuze 1600. Sasa nilipoharibu nikapiga mzigo stoo kwamba bei ikikaa sawa nitauza duh! Kumbe mzigo si haujakauka vizuri, nilikaa kama wiki nafungua stoo nakuta mzigo wote umevunda... Duh!
Hii ishu imemtokea jamaa yangu mwezi huu yani ni hatari.
 
Mimi binasfi cjawahi filisika lakin nakili wazi kabsa kma asingekuwa mke wangu kuniongoza vema kwenye mambo ya kheri mhhh bac mpaka sasa ningekuwa nishafilisika zamaaaaan!! Mwanamke wangu shujaa wangu hela natafuta mimi lakin matumiz napangiwa hela inayobaki tunafanyia jambo la maana kabsa ningekuwa mimi mwenyewe nicngeweza
 
Back
Top Bottom