Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Niliwahi kuzichanga huko nyuma, nikafungua grocery! Kwa kuwa nami nilikuwa mwanachama, mwanzoni nilikuwa na wateja wazuri na waaminifu. Baada ya muda mikopo ikaanza. Mteja akikopa na deni likiwa kubwa, anahama kijiwe.

Nakumbuka mara ya mwisho nilifungia crate tupu kwani hata chupa walishakopa zikiwa na pombe ndani. My Take: Biashara ya pombe kama na wewe mmiliki ni mnywaji, usinywee pale, ni hatari kwa usalama wa grocery yako.
Hayo ndio yanayo nikost Mimi na mume WANGU... FUNGA, fungua kila siku ela z uku zinaend kununua vinywaj kwa wiki yeye peke yake anakunyw kret 3 had 4 maana anajua n MARAFIKI na si mchoyo....nimeongea NIMECHOKA NIMEAMUA nikae kimya na mm sinywi pombe lakin mwenzangu Muhaya huyu anakoga sio kunywa
 
Pole sana mkuu, hii thread yako inanikumbusha ndugu na jamaa waliofilisika, nami kupitia wao nimejifunza vitu vingi sana katika maisha, kwanza nnaamini hakuna ajuaye kesho yake, pili kufilisika haina kesho, tatu usijivune ukiwa navyo(usiwadharau wengine), nne kuwa na nidhamu ya pesa(kimatumizi), tano epuka kukopa kiwango kikubwa cha mkopo na pia usiwe mwepesi kukopesha na n.k
Kunywa soda hii sentesi ya mwisho
 
nilipata 5.5 M kutoka abroad kwa ndg angu mmoja hivi kama ada then nikawa nikanunua kitanda na godoro kama 350k nikanunua sim 400k laptop ya 400k nikalipa kodi 500k nikawa nimetumia kama 1.55M hii nyingine iliyobaki sikuelewa imeenda wapi zaidi ya kununua nguo na kupigia ruti ikakata niliishi kama mbwa koko tena wale watembea jalalani kuchakura mabaki at last laptop niliyokua nayo ikabidi niisukume nikapata kama 350k ingawa ningeweza uza zaidi manake ilikua chuma na mimi niliinunua kwa mtu mwenye shida

Slowly nikawa nanunua kuku nasukuma huku faida ikipatikana nanunua beberu wadogo nawahasi nawafuga time hii niko mwanza naonekana kama mwanachuo mzururaji ambaye alikua anaenda nzega na kurudi mara kwa mara japokua mambo yalianza kunyooka.....aisee biashara ya kuku ilikuja kudidimia baada kuibuka ugonjwa wa Kuku hasara ilikua kubwa sijakaa saa niko mwanza naambiwa mbuzi wameugua kimeta wanakufa tu maisha yakarudi kua magumu hapo nimekula sehemu ya ada na hapo naunga unga tu muhimu nilikua nimelipa kodi whole year na nyumba hazikua ghali sana

Mara ya pili nikapata 4M hii ndio ilikua mbaya nilikua kichaa
Aisee nilikua nakula bata sio kawaida nimekula totoz za kila aina na kwakua Mimi sio mlevi aisee nimekula totoz ikafikia time nikawa naona mwili umechoka kiuno hoi na mgongo unaita na nilikua napiga show kama vile nnaemkula ananilipa kws lengo na kumkomoa kumbe bwana malaya hakomolewi wengine wakaniganda mpaka leo hata nikimuona rafiki ake status nikaulizia namba hatokaa anipe zaidi ya kusema nimgegede Yeye

Within 2½ months nikawa nimekata pesa ATM yaani mpunga ukakata ...siku nimegundua mpunga umekata ni liposoma balance kwenye risit nikakuta 56000 aroooo[emoji23][emoji23] nilitafakari pale atm kwa kina sana nikajikuta nimeanza kusali bila kujua

This time around sitaki wanawake tena nikijua nimuuzaji nampotezea kabisa yani kuna namna siwahisi.....yaani sina hisia nao kabisa kwa sasa

Aisee
Wanawake ni catalyst ya mtu kumaliza pesa
Ukiendekeza mambo ya kula uroda unaishia kumaliza kila kitu

This time around mambo sio mabaya sana japokua nashukuru hizo moments zimenipa nidhamu ya pesa ninaheshimu pesa kwa sasa aisee hua nikiamka lazima niisalimie kwanza ndio niendelee na mambo mengine

Si siku nyingi mtonyo utaingia baada ya muda mrefu huu wenyewe ni kwa ajili ya maisha tu ila nimeupangia makubwa sio kawaida
Walikuwa wanakutumia Kwa njia gani
 
Namaliza chuo tu napta kazi. Inalipa mbaya nakodisha apartment. Nikifunga hesabu ya mwezi haina kwere nawatafuta washkaji tunasherehekea. Madem hawakauki kwangu full kujiachia ndani ya self contained. Luxury life. Sina saving. Siku nivofanyiwa auditing nakubaini madudu kazi ikaisha.

Nilipagawa nikarudi kwa baba na mama. Nikapatwa na maradhi ya watu wazima mapresha wakati niko kijana mbichii. Washkaji walinitenga. Mpaka leo sijapata kazi ya mana nahangaika kwa wahindi kazi mlima mshahara kichuguu. Nawazaga Sana'a.
Ngoma au gono
 
Huu uzi unanisuta mm. Enzi hizo kila club unayoijua hapa mjini nilikuwa napewa hashima na mameneja. Nimemtajirisha sana mbowe pale bills. Meza yangu ilikuwa haipungui watu 5. Nikaja nikaishiwa hata mia sina, ninachohukuru nilijenga nyumba ya maana. Jamaa zangu wote wakanikimbia. Inafika hatua uko nyumni kwenye jumba zuri hata mia huna. Unaanzaje kwenda kukopa kwa mangi wkt jamii inakuona mdosi!!!! Hajahahaha maisha haya. Msoto mkali miaka 3 mfululizo. Baada ya hapo nikaanza kupata vidili vya kuinhiza 2mil kwa week. Nafanya kazi lkn hela inaishia wapi sijui

Baada ya kutafakali sana nikaona niache kunywa c/lite. Hahahaha sasa nimeona nianze kunywa chibuku. Hata niwe na milion mfukoni nanunua kopo zangu tatu kwa shs 3000 tu natinga home nameza zangu chibuka. Namshukuru wife alinivumilia kipindi kile.

Bila kufulia huwezi jua dunia ikoje
Deal gani ulipata
 
Ukiwa nazo za kukinga.

Rafiki yako mkubwa ATM. Ukiingia pale una bofya tu. Mpunga unatoka. Zingine mpyaaaa. Alafu zina ubaridi ubaridi wa air condition. Ngoja siku ziishe. ATM utaipitia kwa mbaaali. Uingie ukafanye nini?

Nimeyamiss haya maisha kwa kweli.
Juzi naingia ATM inatema ubaridi wa AC naangalia tuuu
 
Hayo ndio yanayo nikost Mimi na mume WANGU... FUNGA, fungua kila siku ela z uku zinaend kununua vinywaj kwa wiki yeye peke yake anakunyw kret 3 had 4 maana anajua n MARAFIKI na si mchoyo....nimeongea NIMECHOKA NIMEAMUA nikae kimya na mm sinywi pombe lakin mwenzangu Muhaya huyu anakoga sio kunywa
Du
 
Back
Top Bottom