Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Kukopa kuzuri ni kule kunakotokana na kutathmini faida ya mkopo kwanza.
Yaani nakopa Tsh 10m, nakatwa jumla ya 12. hapo ukweli nimekopa 8m.
Hiyo 8m kuna biashara naenda kuifanya itakayo niingizia zaidi ya 21m kwa muda usiozidi japo miezi mitano.
Katika hiyo miezi mitano nalipa mkopo wao wa m13, na kubakiwa na m8 kama faida.
Hapo nitakuwa nimepata m8 yangu ya kuendeleza biashara yangu ya mtaji wa m8.
Mambo kwa ground ni tofauti sana [emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Project za Serikali ni pasua kichwa sana, shift ya kutoka kwa JK to JPM imefanya makandarasi wengi kuwa maskini. Kukopea hela mradi wa Serikali pasua kichwa, labda uingie ubia na bank katika mradi husika inaweza pona pona yako.
Usifanye biashara na serikali hasa kama biashara Yako Haina mizizi utafilisika tu
 
Ni jambo linawezekana kabisa 100% hasa kama unataka kuekeza kwenye real estate cyo kila mkopo uendeleze biashara. Kukopa na kujenga kwa ajili ya biashara n nzur pia.
real etste inajengwa kwa profit generated sio mkopo...kwa sababu retune yake hadi uufikie profit margin ni mda mrefu labda zingekuwepo bank of investment hapa tz...zote ni commercial...hakuna itakayokupa grace period..ladba uchukue mkopo kumalizia real estate yako watu waingie uanze kupiga hela ila sio kujenga JARIBU UJE UTOE USHUHUDA HAPA.
 
Ni mwendo wa kuhamisha madeni, wa mwisho ama zake ama zangu..

Juzi kuna mshkaji wangu kaenda kuwashtaki taasisi iliyomkopesha ya kuwa wana mikopo kandamizi baada ya kuvutana, baada ya uchunguzi bahati ikawa kwake, akaambiwa alipe deni bila riba maana taasisi haikusajiliwa, na alishakaa na hela miezi 13.
Je hata hiyo ya bila riba alifanikiwa kulipa?

Maana ninavyojua, ukishafirisika hata uambiwe kulipa bila riba ni mtihani tu!

Ninawaona kina mama waliochukua pesa za Halmashauri zisizo na riba wanavyohaha namna ya kulipa marejesho tarehe zikifika!
 
Sure bro. Mambo yakigoma huwa ni balaa.
 
Ni mwendo wa kuhamisha madeni, wa mwisho ama zake ama zangu..

Juzi kuna mshkaji wangu kaenda kuwashtaki taasisi iliyomkopesha ya kuwa wana mikopo kandamizi baada ya kuvutana, baada ya uchunguzi bahati ikawa kwake, akaambiwa alipe deni bila riba maana taasisi haikusajiliwa, na alishakaa na hela miezi 13.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] tabia mbaya hiyo
 
Back
Top Bottom