Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Pole kwa waliokopa, wakabetia halafu wakaliwa na dhamana zao mwishoni zikauzwa kwa bei za kutupwa.
 
Hapo ulikosea kwa mkenya tu, hasa ulivyomlipa pesa yote, kwenye deal yoyote ya ivyo wewe nguvu yako iko kwenye pesa yako. Sasa kama umeshamlipa yote unabaki huna nguvu tena
Nilikosea sana mkuu. Sema yule Mkenya ilikuwa ndo tabia yake. Mungu amlaze anapostahili. Kadhulumu wengi sana
 
Aisee hii mikopo iko mizuri na mibaya, nilishawahi kuchukua M10 za mkopo hapo sikujua namna ya kurejesha maana ilikuwa haraka haraka siku yule jamaa ananipa utaratibu wa kurejesha niliishiwa nguvu, maana nilitakiwa nilipe jumla ya M16 kwa miezi sita, cha kustaajabu hela yote niliijengea, nyumba nikaiuza nikageuka mpangaji kwenye hiyo nyumba, alienunua hiyo nyumba nae akanipa notisi niachie nyumba yake.
Hii kali, kuna mikopo sio rafiki kabisa.
 
Acha tu hii kitu inaitwa mkopo. Mimi ilitaka kunikimbiza niache nchi. Maana kila nilichoshika kilikuwa kinateleza, ndoa huku mambo hayaendi, maana nilikuwa sihitaji hata kula mzigo. Nguvu ziliyeyuka mzigo hata ukiubusu unakataa.

Nashukuru nilipomaliza nilikuwa kama nimezaliwa upya. Hii kitu mkopo itabidi niiandikie kitabu vijana wangu waje kujua ilikuwaje maana nao waliteseka sana.
 
Hahaha nina kamkopo kangu ka laki Tano hapa nashangaa mbona hakaishi, hapo nilikuwa natest nilitaka nichukue milioni Moja nikaona hapana embu nitest laki Tano dah nashangaa akaishi bana na mwisho wake ni Jumatatu ijayo doh
 
Aisee hii mikopo iko mizuri na mibaya, nilishawahi kuchukua M10 za mkopo hapo sikujua namna ya kurejesha maana ilikuwa haraka haraka siku yule jamaa ananipa utaratibu wa kurejesha niliishiwa nguvu, maana nilitakiwa nilipe jumla ya M16 kwa miezi sita, cha kustaajabu hela yote niliijengea, nyumba nikaiuza nikageuka mpangaji kwenye hiyo nyumba, alienunua hiyo nyumba nae akanipa notisi niachie nyumba yake.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] daah ila watu kumbe wamekutana na masaibu mengi, ukikaa peke yako unaweza kuhisi kwamba hakuna aliyesuffer kama Mimi kumbe wapo. Good enough watu hawakati tamaa tunajifunza.
 
Kukopa kuzuri ni kule kunakotokana na kutathmini faida ya mkopo kwanza.
Yaani nakopa Tsh 10m, nakatwa jumla ya 12. hapo ukweli nimekopa 8m.
Hiyo 8m kuna biashara naenda kuifanya itakayo niingizia zaidi ya 21m kwa muda usiozidi japo miezi mitano.
Katika hiyo miezi mitano nalipa mkopo wao wa m13, na kubakiwa na m8 kama faida.
Hapo nitakuwa nimepata m8 yangu ya kuendeleza biashara yangu ya mtaji wa m8.
Unaandika kama motivation spika...kana kwamba mambo yote yamepangika.
 
Dadangu anafosi nimwandikie barua ya mkopo,
Anakopea kiwanja cha urithi, hii ni mali yetu mimi na yeye....hii pesa nina wasiwasi hatarudisha.
Naandika kesho kuepuka lawama ila najua ili deni nitalipa mimi dadeki.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] msaidie anakopa kwaajili ya nini mpe ideas ili wew usiingie kwenye shida, afanye marejesho mwenyewe.
 
Uko sahihi bila mkopo huwez fanya maendeleo lazima tu utahitaj mkopo otherwise utachelewa sana kwenye maisha
Hadi kina Bakhresa wanakopa Bank wanaendesha biashara zao. Kukopa muhimu sana ila make sure, narudia make sure Pesa unayokopa huli hata mia, teseka umalize mkopo ubaki na mtaji wako ndo uendelee kula maisha. Cha kurejesha ni Faida sio Mtaji.
 
Back
Top Bottom