Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Ilikuwa mwaka 2011 mwezi wa 7 mara yangu ya kwanza kuchukua mkopo benki, Tsh 3m. Ule mkopo niliufanyia biashara vizuri na nikarejesha bila changamoto kubwa ndani ya miezi 6. Wale maafisa mikopo wakafurahia na kunishauri nichukue mwingine wa Tsh 5m. Nikafikiria na baada ya mwezi nikachukua mkopo mwingine. Ikawa kama bahati wakati nachukua mkopo nikawa nimepata tenda ya kushona uniform za shule flani.

Nikaona hili ni dili zuri na kwa bahati wateja wangu wakanilipa pesa za advance zaidi ya 90%. Kilichofuata nikaamua nitafute mafundi wazuri Nairobi wanishonee uniform zote. HAPA NDO BALAA LILIPOANZA. Niliingia choo cha kike. Mkenya niliyempa kazi kumbe ni mshenzi mno... kadhulumu watu wengi sana. Ni kweli ofisi anayo na mafundi anao ila kwa bahati mbaya huwa hatimizi makubaliano. Ujinga mwingine niliofanya ni kumlipa karibu hela zake zote.

Hadi shule zinafunguliwa Januari sikuwa nimepeleka nguo yoyote kwa mteja. Basi presha ikaanza kutoka kwa mteja wangu ambaye pia alikuwa anawashiwa moto na wanafunzi + wazazi. Baada ya kusumbuana na mzabuni wangu nikaona isiwe ishu nichukue hela za kwenye biashara yangu niliyoombea mkopo wa 5m ili kupambana na tatizo ambalo lilikuwa limefikia pabaya.

Kwa maana nitafute fundi mwingine nitengenezee kwake huku nikiendelea kupambana na huyu wa mwanzo. Changamoto iliyojitokeza tena ikawa kwa muda ule wauza uniform wengine wana kazi zingine nyingi na bei zao zimeshaenda juu. Gharama za nauli nenda rudi Ars - Nrb nazo zikawa zinanipiga kama ngoma.

Hadi kuja kufanikiwa kupeleka nguo angalau kwa 70% tayari kiuchumi nilishayumba hivyo marejesho yakawa yanasuasua. Ninachokumbuka ule mkopo niliotakiwa niwe nimemaliza kulipa kabla hata ya August nilimaliza December kwa mafaini kibao huku nikiwa nimefilisika. Wale maafisa mikopo walijua kuniwashia moto.

Pamoja na yote hayo nilijipanga upya na baada ya miaka kama mitatu nilirudi tena benki na kuchukua mkopo. Ninamshukuru Mungu kwamba ninakopesheka na ninaendelea kuchukua mkopo. Somo kubwa ni kwamba usichukue mkopo kuanzisha biashara.
Fact🙏
 
Mikopo inahitaji nidhamu na commitment

Nilikopa Mwaka Jana 35M, Mkopo wa miezi 12

Bahati mbaya biashara ilienda vibaya hivyo nikalazimika kutumia kipato changu kingine kurejesha Mkopo.

Nilifanikiwa kuurejesha Mkopo Kwa shida sana

Mapema Mwaka huu, nikachukua Mkopo mwingine
Kufikia weekend hii nitakuwa nimeulipa wote

Tukopeni Kwa malengo
 
Ushauri wako ni tukope
 
Duh hatari...mkopo ukazalishe ndio utaenjoy
 
Yaani mikopo si mizuri wallah, nina best yangu kakopana kwenue vicoba sijui black sijui wapi yaani na hana alichokifanya, sasa ni kazi ya mume kumlipia mkewe madeni.
Pumbafu mie ningekuwa mume ningemwambia kagegedwe mpaka ulipe mikopo ya watu. Shenz type
 
Mikopo, mikopo, mikopo, mikopo, mikopo, huwa naona na kusikia watu wanavyoteseka kuhusu mikopo, sitaki hata kujaribu.
 
Nimekopa 30m nikaingiza kwenye ujezi wa gest house, marejesho ni kila mwezi kwenye salary yangu kwa miaka 5. Pesa imekata na ipo kwenye hatua za mwisho.

Naiwazia hii miaka 4.5 iliyobaki ya mateso, kilio na kusaga meno maana sina chanzo chochote cha pesa zaidi ya kazi, na salary inayobaki baada ya makato hata mwisho wa mwezi hua haitoboi.

Sio tangazo ila kama kuna kiumbe kipo tayari kufanya biashara aje DM. alipe kodi tuingize kwenye finishing anze kupiga pesa, eneo ni zuri sana ndani ya DSM. maana atakua ameokoa jaazi ili nipambane na marejesho kwenye salary.

NAKARIBISHA NA WALE WANAOHUSIKA NA KAUSHA DAMU PIA TUYAJENGE KWA MAKUBALIANO MAALUMU.

"IF YOU DIE YOU DIE"
 
🤔Duh pole
 
Mikopo inahitaji nidhamu na commitment

Nilikopa Mwaka Jana 35M, Mkopo wa miezi 12

Bahati mbaya biashara ilienda vibaya hivyo nikalazimika kutumia kipato changu kingine kurejesha Mkopo.

Nilifanikiwa kuurejesha Mkopo Kwa shida sana

Mapema Mwaka huu, nikachukua Mkopo mwingine
Kufikia weekend hii nitakuwa nimeulipa wote

Tukopeni Kwa malengo
Hela ya mkopo wanasemaga tuziombee na tuzitolee sadaka hazifai
Yani huwa zinaishaga hujafanya cha maana
 
Back
Top Bottom