Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Hapo uliposema usichukue mkopo kuanzisha biashara umetumia vigezo vya wewe kukwama wakati mmoja tu. Sisi tunataka mikopo tuweke mabiashara
Ilikuwa mwaka 2011 mwezi wa 7 mara yangu ya kwanza kuchukua mkopo benki, Tsh 3m. Ule mkopo niliufanyia biashara vizuri na nikarejesha bila changamoto kubwa ndani ya miezi 6. Wale maafisa mikopo wakafurahia na kunishauri nichukue mwingine wa Tsh 5m. Nikafikiria na baada ya mwezi nikachukua mkopo mwingine. Ikawa kama bahati wakati nachukua mkopo nikawa nimepata tenda ya kushona uniform za shule flani.

Nikaona hili ni dili zuri na kwa bahati wateja wangu wakanilipa pesa za advance zaidi ya 90%. Kilichofuata nikaamua nitafute mafundi wazuri Nairobi wanishonee uniform zote. HAPA NDO BALAA LILIPOANZA. Niliingia choo cha kike. Mkenya niliyempa kazi kumbe ni mshenzi mno... kadhulumu watu wengi sana. Ni kweli ofisi anayo na mafundi anao ila kwa bahati mbaya huwa hatimizi makubaliano. Ujinga mwingine niliofanya ni kumlipa karibu hela zake zote.

Hadi shule zinafunguliwa Januari sikuwa nimepeleka nguo yoyote kwa mteja. Basi presha ikaanza kutoka kwa mteja wangu ambaye pia alikuwa anawashiwa moto na wanafunzi + wazazi. Baada ya kusumbuana na mzabuni wangu nikaona isiwe ishu nichukue hela za kwenye biashara yangu niliyoombea mkopo wa 5m ili kupambana na tatizo ambalo lilikuwa limefikia pabaya.

Kwa maana nitafute fundi mwingine nitengenezee kwake huku nikiendelea kupambana na huyu wa mwanzo. Changamoto iliyojitokeza tena ikawa kwa muda ule wauza uniform wengine wana kazi zingine nyingi na bei zao zimeshaenda juu. Gharama za nauli nenda rudi Ars - Nrb nazo zikawa zinanipiga kama ngoma.

Hadi kuja kufanikiwa kupeleka nguo angalau kwa 70% tayari kiuchumi nilishayumba hivyo marejesho yakawa yanasuasua. Ninachokumbuka ule mkopo niliotakiwa niwe nimemaliza kulipa kabla hata ya August nilimaliza December kwa mafaini kibao huku nikiwa nimefilisika. Wale maafisa mikopo walijua kuniwashia moto.

Pamoja na yote hayo nilijipanga upya na baada ya miaka kama mitatu nilirudi tena benki na kuchukua mkopo. Ninamshukuru Mungu kwamba ninakopesheka na ninaendelea kuchukua mkopo. Somo kubwa ni kwamba usichukue mkopo kuanzisha biashara.
a
 
Mikopo inaleta fedheha hasa kausha damu ukishndwa kurudisha wanakuja
kubeba hadi chupi nilishudia kwa mdada mmoja iv.
Yaani mikopo si mizuri wallah, nina best yangu kakopana kwenue vicoba sijui black sijui wapi yaani na hana alichokifanya, sasa ni kazi ya mume kumlipia mkewe madeni.
 
Hahaha nina kamkopo kangu ka laki Tano hapa nashangaa mbona hakaishi, hapo nilikuwa natest nilitaka nichukue milioni Moja nikaona hapana embu nitest laki Tano dah nashangaa akaishi bana na mwisho wake ni Jumatatu ijayo doh
[emoji23][emoji23][emoji23],utapata presha[emoji23][emoji23]
 
Dadangu anafosi nimwandikie barua ya mkopo,
Anakopea kiwanja cha urithi, hii ni mali yetu mimi na yeye....hii pesa nina wasiwasi hatarudisha.
Naandika kesho kuepuka lawama ila najua ili deni nitalipa mimi dadeki.
Vizuri unajua kabisa utalipa mwenyewe hapo haina shida....
 
Heri mtu ukope ujue deni ni lako.....wengine tunaumizwa na kudhamini watu, kukopesha aisee mtu hupati hata usingizi

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Hii imenikuta mie na nimeapia sitomkopea mtu katu,labda mama yangu.

Yaani nilimkopea best yangu kwa jina langu so tarehe ya marejesho ilikuwa 19/12 mwezi huu, sasa ananiambia hana hela[emoji23]

Kiukweli nilijifungia ndani siku kama mbili hivi hata kula siwezi na nguvu sina, na mama sikumuambiaga kama nilimkopea mtu[emoji23],

Home niliwaambia tu kuwa naumwa,

J,pili ikapita na sikwenda niliagiza tu pesa ya hisa,

Nilivyoona yataniua,nilimwambia mama aisee,ikabidi anipe kiasi na nyingine akaniambia nitajua mwenyewe,na,

Na j,pili ya juzi ilikuwa ni siku ya mwisho kukabidhi pesa mezani aisee malengo yangu yote yameyeyuka maana nimekatwa hisa zangu na pesa za maafa,

Na kama kunilipa atanilipa lkn si kwa mwaka huu tena,

Najuta na sitorudia tena.
 
Na mimi nataka kukopa lakini sina biashara bali nina nyumba yenye HATI safi Dodoma, sasa kama kuna Mfanyabiashara anayekopesheka anahitaji kukopa Bank lakini hana dhamana mimi ninayo aje inbox tuyajenge, Nyumba ipo Dodoma Mjini, thamani ya Nyumba ni zaidi ya Milioni 50 na ni Nyumba mpya, karibuni.
Nikupe pole in advance kabla hao wabia unaowatafuta hawajaja
 
Pol
Hii imenikuta mie na nimeapia sitomkopea mtu katu,labda mama yangu.

Yaani nilimkopea best yangu kwa jina langu so tarehe ya marejesho ilikuwa 19/12 mwezi huu, sasa ananiambia hana hela[emoji23]

Kiukweli nilijifungia ndani siku kama mbili hivi hata kula siwezi na nguvu sina, na mama sikumuambiaga kama nilimkopea mtu[emoji23],

Home niliwaambia tu kuwa naumwa,

J,pili ikapita na sikwenda niliagiza tu pesa ya hisa,

Nilivyoona yataniua,nilimwambia mama aisee,ikabidi anipe kiasi na nyingine akaniambia nitajua mwenyewe,na,

Na j,pili ya juzi ilikuwa ni siku ya mwisho kukabidhi pesa mezani aisee malengo yangu yote yameyeyuka maana nimekatwa hisa zangu na pesa za maafa,

Na kama kunilipa atanilipa lkn si kwa mwaka huu tena,

Najuta na sitorudia tena.
Pole ni shngp ulimkopea
 
Yaani mikopo si mizuri wallah, nina best yangu kakopana kwenue vicoba sijui black sijui wapi yaani na hana alichokifanya, sasa ni kazi ya mume kumlipia mkewe madeni.
Yani unakuta ameachiwa hela ya matumiz anapeleka rejesho mwisho wa siku anaomba omba ili apate ya chakula...kweli kazi ipo
 
Yani unakuta ameachiwa hela ya matumiz anapeleka rejesho mwisho wa siku anaomba omba ili apate ya chakula...kweli kazi ipo
Yaani,kula kuvaa analetewa tu mahitaji no pesa, kila akipewa mtaji haudumu maana marejesho ni mengi,

Mumewa alikuwa anamkabidhi bajeti ya mwezi ya chakula lkn anunui mahitaji analisha ugali dagaa mwezi mzima, mume kwasasa ananunua kila kitu mwenyewe,

Sema tu huyu ni tamaa tu.
 
Poleni sana...maisha yamegeuka
Yamegeukaje apa wife material ukimwachia pesa unakuta kanunua kila kitu chenye pesa uliomwachia lkn mke unaweza sikute kitu chochote na pesa umemwachia isipokua Utaambiwa njoo na chakula chako au chips pesa yote imepelekwa kwenye vikoba na marejesho 🤣🤣
 
Back
Top Bottom