Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Pole kwa waliokopa, wakabetia halafu wakaliwa na dhamana zao mwishoni zikauzwa kwa bei za kutupwa.
 
Hapo ulikosea kwa mkenya tu, hasa ulivyomlipa pesa yote, kwenye deal yoyote ya ivyo wewe nguvu yako iko kwenye pesa yako. Sasa kama umeshamlipa yote unabaki huna nguvu tena
Nilikosea sana mkuu. Sema yule Mkenya ilikuwa ndo tabia yake. Mungu amlaze anapostahili. Kadhulumu wengi sana
 
Hii kali, kuna mikopo sio rafiki kabisa.
 
Acha tu hii kitu inaitwa mkopo. Mimi ilitaka kunikimbiza niache nchi. Maana kila nilichoshika kilikuwa kinateleza, ndoa huku mambo hayaendi, maana nilikuwa sihitaji hata kula mzigo. Nguvu ziliyeyuka mzigo hata ukiubusu unakataa.

Nashukuru nilipomaliza nilikuwa kama nimezaliwa upya. Hii kitu mkopo itabidi niiandikie kitabu vijana wangu waje kujua ilikuwaje maana nao waliteseka sana.
 
Hahaha nina kamkopo kangu ka laki Tano hapa nashangaa mbona hakaishi, hapo nilikuwa natest nilitaka nichukue milioni Moja nikaona hapana embu nitest laki Tano dah nashangaa akaishi bana na mwisho wake ni Jumatatu ijayo doh
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] daah ila watu kumbe wamekutana na masaibu mengi, ukikaa peke yako unaweza kuhisi kwamba hakuna aliyesuffer kama Mimi kumbe wapo. Good enough watu hawakati tamaa tunajifunza.
 
Unaandika kama motivation spika...kana kwamba mambo yote yamepangika.
 
Dadangu anafosi nimwandikie barua ya mkopo,
Anakopea kiwanja cha urithi, hii ni mali yetu mimi na yeye....hii pesa nina wasiwasi hatarudisha.
Naandika kesho kuepuka lawama ila najua ili deni nitalipa mimi dadeki.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] msaidie anakopa kwaajili ya nini mpe ideas ili wew usiingie kwenye shida, afanye marejesho mwenyewe.
 
Uko sahihi bila mkopo huwez fanya maendeleo lazima tu utahitaj mkopo otherwise utachelewa sana kwenye maisha
Hadi kina Bakhresa wanakopa Bank wanaendesha biashara zao. Kukopa muhimu sana ila make sure, narudia make sure Pesa unayokopa huli hata mia, teseka umalize mkopo ubaki na mtaji wako ndo uendelee kula maisha. Cha kurejesha ni Faida sio Mtaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…