Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Mkuu kwani si kuna kuna kufunga mikataba ? Mbona kampuni za nje ziki dhurumiwa na Serikali zina ishtaki serikali na serikali inalipa gharama zote, sasa inakuwaje kampuni za wazawa zina shindwa kuishtaki serikali ?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Kuna shida katika uendeshaji wa local company, kuna kipindi mtu ana sign mkataba tu ili apate kazi hata kama haoni kitu mbeleni.. badae yanatokea mazingira kama hayo na ndio mwisho wa company. Jiulize kwanini local company nyingi zinakufa
 
mikopo nomaz mimi hadi leo kuna bank inanidai 16mil nasijui ntawalipaje wameshikilia hati ya nyumba yangu ya pekee niliyoujenga jaw jesho sijengi sanaaa .
Mkuu mimi Mzazi wangu kakopa pesa Banki lakini kwa marejesho ya banki kukata kwenye pensheni yake sasa pensheni yake Azina hawaja muingizia benki miezi 4 imefika sasa Afisa mikopo wa Banki ana tusumbua sisi watoto tumpeleke mzee wetu Azina akahakikiwe, Mimi nimekataa simpeleke kwasababu pesa alivyokopa haja tugaiya kaitumia peke yake, sasa hatujui afisa mikopo wa benki atazipataje pesa zaidi ya Milioni 10

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Si hatuvunji December maana hakikuanza December
Ndo kwanzaaaa tuna miez kadhaa
Pole,inabidi upambane tu,

Nilikopa laki 6 aisee nilishasema silipi maana mambo ni mseto na nimekuja shtuka tulipewa wiki 2 turejeshe juzi j,pili nimehesabiwa hisa zangu nilichomoka na 24000 tu[emoji16]

nafikiria hapa niingie tena au[emoji706]
 
Pole,inabidi upambane tu,

Nilikopa laki 6 aisee nilishasema silipi maana mambo ni mseto na nimekuja shtuka tulipewa wiki 2 turejeshe juzi j,pili nimehesabiwa hisa zangu nilichomoka na 24000 tu[emoji16]

nafikiria hapa niingie tena au[emoji706]
Ingia tena vinasaidia mnoo
Me nkiwa na shida ya laki kadhaa hadi milioni ndo naibukia huko pananitoa sana
 
Aisee hii mikopo iko nzuri na mibaya, nilishawai kuchukuwa M10 za mkopo hapo sikujua namna ya kurejesha maana ilikuwa haraka haraka siku yule jamaa ananipa utaratibu wa kurejesha niliishiwa nguvu, maana nilitakiwa nilipe jumla ya M16 kwa miezi sita, cha kustaajabu hela yote niliijengea, nyumba nikaiuza nikageuka mpangaji kwenye hiyo nyumba, alienunua hiyo nyumba nae akanipa notisi niachie nyumba yake.
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ilikuwa mwaka 2011 mwezi wa 7 mara yangu ya kwanza kuchukua mkopo benki, Tsh 3m. Ule mkopo niliufanyia biashara vizuri na nikarejesha bila changamoto kubwa ndani ya miezi 6. Wale maafisa mikopo wakafurahia na kunishauri nichukue mwingine wa Tsh 5m. Nikafikiria na baada ya mwezi nikachukua mkopo mwingine. Ikawa kama bahati wakati nachukua mkopo nikawa nimepata tenda ya kushona uniform za shule flani. Nikaona hili ni dili zuri na kwa bahati wateja wangu wakanilipa pesa za advance zaidi ya 90%. Kilichofuata nikaamua nitafute mafundi wazuri Nairobi wanishonee uniform zote. HAPA NDO BALAA LILIPOANZA. Niliingia choo cha kike. Mkenya niliyempa kazi kumbe ni mshenzi mno... kadhulumu watu wengi sana. Ni kweli ofisi anayo na mafundi anao ila kwa bahati mbaya huwa hatimizi makubaliano. Ujinga mwingine niliofanya ni kumlipa karibu hela zake zote.

Hadi shule zinafunguliwa Januari sikuwa nimepeleka nguo yoyote kwa mteja. Basi presha ikaanza kutoka kwa mteja wangu ambaye pia alikuwa anawashiwa moto na wanafunzi + wazazi. Baada ya kusumbuana na mzabuni wangu nikaona isiwe ishu nichukue hela za kwenye biashara yangu niliyoombea mkopo wa 5m ili kupambana na tatizo ambalo lilikuwa limefikia pabaya. Kwa maana nitafute fundi mwingine nitengenezee kwake huku nikiendelea kupambana na huyu wa mwanzo. Changamoto iliyojitokeza tena ikawa kwa muda ule wauza uniform wengine wana kazi zingine nyingi na bei zao zimeshaenda juu. Gharama za nauli nenda rudi Ars - Nrb nazo zikawa zinanipiga kama ngoma.

Hadi kuja kufanikiwa kupeleka nguo angalau kwa 70% tayari kiuchumi nilishayumba hivyo marejesho yakawa yanasuasua. Ninachokumbuka ule mkopo niliotakiwa niwe nimemaliza kulipa kabla hata ya August nilimaliza December kwa mafaini kibao huku nikiwa nimefilisika. Wale maafisa mikopo walijua kuniwashia moto.

Pamoja na yote hayo nilijipanga upya na baada ya miaka kama mitatu nilirudi tena benki na kuchukua mkopo. Ninamshukuru Mungu kwamba ninakopesheka na ninaendelea kuchukua mkopo. Somo kubwa ni kwamba usichukue mkopo kuanzisha biashara.
Usichukue Mkopo kuanzisha Biashara.
🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom