Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Taratibu aisee yaani umefanya moyo ulipuke puuuh..!

Yaani hawa platinum credit wataua raia huku....jamani msipende kuchoma mikuki ya moto rohoni yaani hata ni vigumu kuelezea

Hahahahahaa mimi walikuwa kila siku wananitumia majembe,siku nilipogundua walipoweka zile GPRS zao walifurahi,mpaka leo wananisaka na mkopo sijawahi kulipa.
 
-Usikope kuanzisha biashara
-Usikope kujenga

Nyinyi hivi vitu mnafanya kwa pesa ipi?

Tatizo mnashauri kwa jumla,nachojua sio kila mmoja ataishi bila kukopa labda huo ushauri wenu mnashauriana wafanyabiashara, mtumishi asipokopa ili kujenga akaibe? Maana vimishahara vyenyewe uchwara
Wakati mwingine usiwazingatie sana watu na comments zao humu.Mimi nilikopa na nikajenga na Sasa naishi.Nilikopa na nikaanzisha biashara miaka Saba iliyopita na Sasa inanitunza Mimi na familia.Mshahara ni chanzo kizuri mno Cha mtaji,kwakuwa hautateswa na rejesho la Kila mwezi kutoka kwenye biashara
 
Hahahahahaa mimi walikuwa kila siku wananitumia majembe,siku nilipogundua walipoweka zile GPRS zao walifurahi,mpaka leo wananisaka na mkopo sijawahi kulipa.
Duuh mm wananidai mwaka sana umeisha sijui ni watoroke aje
 
mazaa alikua akichukua mikopo kwa wale SEDA.. asee mambo yakaenda kombo akawa anawatoroka maana anajua siku zao za doria..

Wakaja kwa kushtukiza kwetu ni badland kule gari unaacha road upite chocho kadhaa ndo ufike..

Braza alikua anajua ile gari ya alivyoiona chap mbiombio akaja kumshtua maza, chap akazama uvunguni..

Wakafika cha kwanza..mama yuko wapi ? Braza kwaambia amesafiri kuna msiba kijjini alikua anajibu kwa wasiwasi..

Mmoja wao akanichukua nlikua ndo niko Darasa la kwanza haoo hadi dukani...Mangi mpe mtoto mzuri biskuti ilikia zile za choclate 500/=nakumbuka..

Woii nikachoma maza yupo uvunguni kule.. [emoji23][emoji23][emoji23] wakaenda kumchomoa, hela hamna wakasomba mazaga hapo sebleni

Ile kipigo nlipata walivyoondoka biskuti ilitokea puani...

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]dah hatari
 
Kuna kikampuni hapo dodoma kinakopesha kwa dhamana ya kiwanja, chombo cha moto, ama nyumba, muhimu uwe mmiriki halali, watafute hao, uwapige hela, ukishindwa kurudisha wanachukua chako kinakuwa chao, unakuwa kama umeuza mali na kupata pesa...THE DEAL DONE, hivyo ndivyo maharamia tulifanya biashara bila kuhangaika na wateja[emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hahahhahahah wewe jamaa
 
Pole sana mkuu. Kama bado uko na hizo shughuli za kushona tupeane connection DM. Mim pia ni fundi kama wewe
 
Ilikuwa mwaka 2011 mwezi wa 7 mara yangu ya kwanza kuchukua mkopo benki, Tsh 3m. Ule mkopo niliufanyia biashara vizuri na nikarejesha bila changamoto kubwa ndani ya miezi 6. Wale maafisa mikopo wakafurahia na kunishauri nichukue mwingine wa Tsh 5m. Nikafikiria na baada ya mwezi nikachukua mkopo mwingine. Ikawa kama bahati wakati nachukua mkopo nikawa nimepata tenda ya kushona uniform za shule flani.

Nikaona hili ni dili zuri na kwa bahati wateja wangu wakanilipa pesa za advance zaidi ya 90%. Kilichofuata nikaamua nitafute mafundi wazuri Nairobi wanishonee uniform zote. HAPA NDO BALAA LILIPOANZA. Niliingia choo cha kike. Mkenya niliyempa kazi kumbe ni mshenzi mno... kadhulumu watu wengi sana. Ni kweli ofisi anayo na mafundi anao ila kwa bahati mbaya huwa hatimizi makubaliano. Ujinga mwingine niliofanya ni kumlipa karibu hela zake zote.

Hadi shule zinafunguliwa Januari sikuwa nimepeleka nguo yoyote kwa mteja. Basi presha ikaanza kutoka kwa mteja wangu ambaye pia alikuwa anawashiwa moto na wanafunzi + wazazi. Baada ya kusumbuana na mzabuni wangu nikaona isiwe ishu nichukue hela za kwenye biashara yangu niliyoombea mkopo wa 5m ili kupambana na tatizo ambalo lilikuwa limefikia pabaya.

Kwa maana nitafute fundi mwingine nitengenezee kwake huku nikiendelea kupambana na huyu wa mwanzo. Changamoto iliyojitokeza tena ikawa kwa muda ule wauza uniform wengine wana kazi zingine nyingi na bei zao zimeshaenda juu. Gharama za nauli nenda rudi Ars - Nrb nazo zikawa zinanipiga kama ngoma.

Hadi kuja kufanikiwa kupeleka nguo angalau kwa 70% tayari kiuchumi nilishayumba hivyo marejesho yakawa yanasuasua. Ninachokumbuka ule mkopo niliotakiwa niwe nimemaliza kulipa kabla hata ya August nilimaliza December kwa mafaini kibao huku nikiwa nimefilisika. Wale maafisa mikopo walijua kuniwashia moto.

Pamoja na yote hayo nilijipanga upya na baada ya miaka kama mitatu nilirudi tena benki na kuchukua mkopo. Ninamshukuru Mungu kwamba ninakopesheka na ninaendelea kuchukua mkopo. Somo kubwa ni kwamba usichukue mkopo kuanzisha biashara.
Pole sana mkuu. Njoo DM tupeane connection za ufundi wa kushona
 
Muda huu naenda kukamata nyumba ya mtu na mnada juu, yule mama lazima aniroge yaani.analia anasema ninvumilie ana misiba mitatu, sijui nani kafa, lakini ashapewa notice muda mrefu sana na mnunuzi ninae tiyari na ninaambiwa ni mchawi.🤣
Mwingine lazima nimuondowe pale maana sio kwa kiburi kile hataki kutoka kwa hiari, mama yake ni mzee sana nilienda nikamuelezea kuhusu majanga ya mwanae, cha ajabu yule bibi ni mzeee sana ila ati alikuwa mganga juzi niliona kwenye ndoto wamenitumia nyota nyiiingi naziona kwenye kona ya chumba nikaanza kukemea. Moyo ulienda mbio nikasali sana

Hii mikopo hii kuuza lazima niuze.
Afisa mikopo utaua watu 😂😂
 
😂😂😂
Hawa watu hasa wa microfinance wanakwaza sana
Na siku ya mwishobwatakua wanachomwa kama hotdog wanaviringishwa ndani ya gogo af wanaunguzwa taratibu waahed kabisa.

Kuna mmoja alikuja kazini amechomekea mpka kwenye diaphram na hesima deebe ananidedesa nichukue mkopo kwao marejesho yao ni kidogo hayaumizi. Nkamwambia aende aniachie kipeperushi nitafakari. Alivoondoka nkakaa nkapiga hesabu vzuri kbsa taratibu, nkaja kushtukia kua naenda kupigwa riba ya almost 30% kisirisiri, nkachana kipeperushi nkatupa kwenye dustbin.

Jamaa hakuogopa akaenda kwa mlinzi wa ofisi akamseti, msukuma wa watu akajaa kingi akachukua mkopo kwa kuamini kua rejesho la elf 5 kwa wiki hawezi kosa. Baadae akaja nkampigia hesabu nkamfungulia dunia kama clouds fm, alichoka. Yuke mlinzi kila jembe analopiga ardhini anawatukana wale jamaa. Alifanikiwa kulipa lkn kwa uchungu sana.

Bora nikope kwenye vikundi vya hisa huko, yakinishinda wanachukua hisa zangu aibu inapungua.
😂😂😂 nimecheka sana hiyo kuchomekea mpaka kwenye diaphragm
 
Mkuu kwani si kuna kuna kufunga mikataba ? Mbona kampuni za nje ziki dhurumiwa na Serikali zina ishtaki serikali na serikali inalipa gharama zote, sasa inakuwaje kampuni za wazawa zina shindwa kuishtaki serikali ?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Huwezi ishtaki serikali wakati uhai wa kampuni yako unategemea tenda kutoka kwao
 
Aisee hii mikopo iko mizuri na mibaya, nilishawahi kuchukua M10 za mkopo hapo sikujua namna ya kurejesha maana ilikuwa haraka haraka siku yule jamaa ananipa utaratibu wa kurejesha niliishiwa nguvu, maana nilitakiwa nilipe jumla ya M16 kwa miezi sita, cha kustaajabu hela yote niliijengea, nyumba nikaiuza nikageuka mpangaji kwenye hiyo nyumba, alienunua hiyo nyumba nae akanipa notisi niachie nyumba yake.
Nimecheka asee
 
Project za Serikali ni pasua kichwa sana, shift ya kutoka kwa JK to JPM imefanya makandarasi wengi kuwa maskini. Kukopea hela mradi wa Serikali pasua kichwa, labda uingie ubia na bank katika mradi husika inaweza pona pona yako.
Shida pesa ikija kama huna pesa nyingine wanakata chao juu kwa juu
 
Back
Top Bottom