Tuliowahi kuvamiwa, kuibiwa au kutekwa na majambazi tujikumbushe

Mimi nakumbuka miaka ya nyuma nimemaliza kidato cha sita, nimetoka kwenye mishe zangu usiku saa tisa, halafu napita eneo la makaburini. Ghafla kwa mbali nikawa nasikia harufu ya moshi wa sigara mchanganyiko na bangi, kucheki naona kundi la watu wanapuliza wamekaa juu ya makaburi. Kipindi hicho watu walikuwa wanapigwa sana na nondo, na wiki kadhaa nyuma kuna jirani yetu aliuawawa. Kurudi nilikotoka njia ni ndefu mno, na kwenda mbele lazima yale manjemba yangenifanya kitu mbaya.

Ile akili sijui hata ilitoka wapi, sijui ni mihadarati. Nilichofanya ni kuvua nguo zote na kuzishika kwa nyuma halafu nikaanza kuelekea usawa wao, niko uchi wa mnyama. Uzuri kulikuwa na mbalamwezi. Jamaa walivyoniona wakaanza kuuliza kwa mbali, wee nani. Mimi kimya nasonga mbele tu, ile kunisogelea na marungu yao na kuniona vizuri kuwa niko uchi, jamaa walipigwa na ganzi. Kilichofuata ni kutukana na kuanza kukimbia vibaya mno kila mtu njia yake.

Kila nikikumbuka huwa najionea sana huruma na kuwaza endapo kama yale manjemba yasingekimbia.
Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.......
 
Wangekutatua marinda mkuu... Usirudie tena kuvua nguo mbele ya wanaume.
 
Umetisha Mkuu[emoji1787]
 
2013 mbona juzi tu we kweli dogo, acha kudanganya watu mwaka huo hakukuwa na mambo ya fatuma. Tafuta uwongo mwingine.
 
2013 mbona juzi tu we kweli dogo, acha kudanganya watu mwaka huo hakukuwa na mambo ya fatuma. Tafuta uwongo mwingine.
Usichokijua hukijui tu,arusha mpaka sasa hivi fatuma bado zipo wanalibeba kwenye kanga kama mtoto mdogo mgongoni,alafu mimi ni dogo kwa umri ila kwa akili ya maisha ni zaidi ya babu
 
 
Yan mi skutaka kuwauliza wamelibebaje...ni za kichwa tu

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
L
Eeeeh pole sana man.....mim walitakaga kunivamia nipo maskani peke nyeke kina maza wamekwenda mkoa acha kabisa klichonisaidia lile geti dogo la mlangoni lilikua imara hapo ndani nishajikojolea nishalia nishaomba Mungu nampgia maza cm hata hapokei
Kuna jirani yetu mmja alikua ni tajiri mtaa mzima alisikia kelele basi bn alipiga risasi mbili sijui ni baruti zile uwanjani kwake wahuni wote wakatoka mkuku
Baada ya muda ndio majirani wanasogea hapo nishalia kama zombie wakaja majirani wengine kurekebisha rekebisha getini wakabaki wawili mmja wa kike mwingine brother hivi akalala na panga hapo ndani

Ya pili ilitokea nikiwa na sister angu yani milango ya home kwetu nahisi ni ya mkoloni miguu balaa
Tumelala usiku sa tisa mara tunasikia mlango wa sebuleni na mlango wa jikoni unagongwa kwa nguvu na kutikiswa sister angu akaniamsha vaa suruali nkavaa a buti chini yani wakiingia ndani nashawaza kabisa hapo ntakimbia kama chizi hadi nyumbani kwa Diwani basi sister angu alikua na Bwana ake mwarabu mmja mgumu kinoma kwanza anaendesha Subaru yule msela akatoka ndani na wenzie kama kumi na usher nilijiuliza sana hawa waarabu hapo ndani wanalala vip maan sio kwa idadi hyo.........Mwizi mmja alikamatwa walichomfanya wakaenda mchomea moto katikati ya barabara polisi tunawapgia simu wanasema ety mmalizieni kabisa walikuja kubeba nyama choma
 
Haha kwamba ndani ya dakika 5 wamekuja waarabu 10 [emoji23][emoji23][emoji23] pole kwa huyo mwizi aiseee

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Ni hatari poleni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…