Kanuni mpya ni kwamba, NIDA moja hairuhusiwi kusajili zaidi ya namba moja kwa mwezi.
Sasa mtu NIDA yake ikitumika kufsnys utapeli kwa laini iliyosajiliwa baada ya kuanza kanuni hii mpya atatueleza, wakala alimsajilisha vipi namba ya ziada? Maana yake mwenye NIDA ndio tapeli. Na namba zote zaNIDA yake zitafungiwa hadi atoke shimoni akatoe maelezo polisi yeye mwenyewe, wala hatutamtafuta.
NB: haya ni mapendekezo yangu binafsi.
An argument from the short-sighted mind person.
Je, hilo ndiyo suluhisho sahihi la tatizo uliloeleza?
Je, umeshawahi kujiuliza ni kwa nini mtu ambaye siyo mmiliki wa akaunti yenye fedha kwenye benki yoyote ile hawezi kufanya muamala wa kutoa fedha kutoka kwa Mhasibu wa Benki bila ridhaa ya màandishi kutoka kwa mmiliki halali wa akaunti ya benki anayetambulika na benki husika? Umeshawahi kujiuliza swali hili?
Je, Hao matapeli wa mitandao ya simu huwa wanawezaje kutoa fedha kutoka kwa Namba ya simu iliyosajiliwa kwa utambulisho wa mtu mwingine bila ya kushitukiwa au bila ya kukamatwa? Is it possible?
Mbona kwenye benki wezi wa fedha zilizotolewa kwenye akaunti ya mtu huwa wanakua tracked na kuweza kukamatwa hata kama mwizi husika alifanya muamala wa wizi akiwa katika nchi nchi nyingine iliyopo mbali kwenye bara lingine hapa duniani? Kwa nini suala hili linashinsikana kwa upande wa mitandao ya simu hapa Tanzania??
Wewe binafsi bado unaamini kwamba hao wanaotakiwa kuzuia au kudhibiti tatizo hili la utapeli na wizi kwenye miamala ya mitandao ya simu hawahusiki kabisa kwenye kadhia hii??
Matahalani, kwenye miamala ya mabenki hapa duniani, kuna teknolojia zinazohusika na suala zima la miamala ya benki zilizopo ndani ya nchi fulani tu pekee na hata kuziunganisha na benki zingine zilizopo katika nchi zingine kwenye maeneo mbalimbali hapa duniani. Teknolojia hizi, kwa mfano teknolojia inayoitwa "SWIFT" kwa upande mwingine pia husaidia katika kuwatambua watu wanaofanya miamala ya benki kitaifa au kimataifa, na pia husaidia katika kuzuia uhalifu au hata kuwakamata wahalifu wa makosa yanayohusiana na miamala ya fedha kwenye mabenki au kwenye hizi taasisi za mitandao ya simu inayotoa huduma za ki-fedha (mobile money service providers). Je, suala Kama hili linashindikana vipi kufanyika hapa Tanzania?
Aidha, kwa kujibu wa taratibu za kimataifa za kuzuia au kudhibiti uhalifu wa fedha chafu au uhalifu wa utakatishaji wa fedha, taratibu ambazo zipo chini ya taasisi za Umoja wa Mataifa, yaani IMF, WB, WTO, n.k zinataka kwa LAZIMA kila nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa (UN) kuwa na taasisi maalumu itayokuwa inahusika na Usimamizi, Uzuiaji na/au Udhibiti wa Uhalifu wa Masuala ya ki-fedha, naamini kwamba Tanzania LAZIMA kuna taasisi ya namna hiyo Yaani "Financial Intelligence Unit (FIU)." Sasa; Je, hiyo FIU ya Tanzania kazi yake ni ipi Basi?? Kazi yake ni 'kusifu na kuabudu' watawala tu peke yake lakini siyo kuwabaini Wahalifu wa mitandao haramu ya fedha chafu???