‘Tuma kwa namba hii’ wapatiwa muarubaini, mwisho wao umefika

‘Tuma kwa namba hii’ wapatiwa muarubaini, mwisho wao umefika

Kwa laini zilizosajiliwa baada ya kuanza kwa kanuni hii, utasemaje laini huitambui wakati uliweka finger print mwenyewe?! Kama ulimsajilia ndugu yako, tupeleke kwake!
Huijui Tanzania ndugu yangu....mfumo wa saivi ni wa fingerprint lakini watu wana swap Sim card za watu kama njugu ..
 
Agent-Principal Relationship Theory.

Watoa huduma za mitandao ya simu (Service Provider, SP) ambao Mawakala wao wamefanya Uhalifu huo wanapaswa kuwajibishwa na kuadhibiwa kwenye suala hili la wizi au utapeli wanaofanyiwa wananchi. Hii itakuwa fundisho kubwa sana kwao
Kwa kanuni hii mpya, wala hatutafika huko, maana watashindwa kusajili laini ziada, na tatizo ndio limeishia hapo.
 
Huijui Tanzania ndugu yangu....mfumo wa saivi ni wa fingerprint lakini watu wana swap Sim card za watu kama njugu ..
Sawa, ila alieswap si anajulikana, maana huwezi kurenew line bila kuweka fingerprint wewe muhusika. Na kama ikifanyika ndani ya ofisi basi jina la mfanyakazi litaonekana kwenye records. Mimi nazungumzia changamoto ya watu kusajilishwa laini za ziada ili kufanyia utapeli na mwishowe inakuwa haijulikani nani kafanya utapeli, hii kanuni mpya itazuia hayo mara moja!
 
Kuna watu wengi hawana NIDA, ukiwatumia hela majina yanatokea si yao. unakuta mtu anawasajilia namba ndugu, marafiki na mahawara zake. nusura nitoe kichapo kikali baada ya msajili laini mmoja kumsajilia mke wangu namba bila kuchukua alama zake za vidole wala nyaraka zingine
 
Sawa, ila alieswap si anajulikana? Mimi nazungumzia changamoto ya watu kusajilishwa laini za ziada ili kufanyia utapeli na mwishowe inakuwa haijulikani nani kafanya utapeli, hii kanuni mpya itazuia hayo mara moja!
Bado tuna safari ndefu hasa ya elimu kwa sababu kwa watu tulioko kwenye industry ya Security kamwe mwizi hazuiliki...always wana improvise...tunapaswa kuwafundisha watumiaji wa simu against phishing attacks na scamming defenses...chaajabu kwenye vyombo vya habari elimu kubwa inayotelwwa ni namna ya kupata hela kwa uraisi...kamari..kamari..michezo supa & e.t.c
 
Kuna watu wengi hawana NIDA, ukiwatumia hela majina yanatokea si yao. unakuta mtu anawasajilia namba ndugu, marafiki na mahawara zake. nusura nitoe kichapo kikali baada ya msajili laini mmoja kumsajilia mke wangu namba bila kuchukua alama zake za vidole wala nyaraka zingine
Ukimsajilia mtu line, na akafanya utapeli, sisi tunakufa na wewe mwenye NIDA, hadi utupeleke kwa hao ndugu zako waliofanya utapeli. Kwa kanuni hii mpya , namba zitasajiliwa kwa fingerprint ya NIDA tu!
 
Bado tuna safari ndefu hasa ya elimu kwa sababu kwa watu tulioko kwenye industry ya Security kamwe mwizi hazuiliki...always wana improvise...tunapaswa kuwafundisha watumiaji wa simu against phishing attacks na scamming defenses...chaajabu kwenye vyombo vya habari elimu kubwa inayotelwwa ni namna ya kupata hela kwa uraisi...kamari..kamari..michezo supa & e.t.c
Sawa. Ila kwa sasa kanuni hii mpya ni muarobaini.
 
Wewe jibu hoja. Kwa kanuni hii mpya, Mtu anaikataa vipi laini ya simu aliyosajili mwenyewe kwa kuweka fingerprint?!
Kwanza utujulishe, wewe binafsi una kiwango gani hasa cha elimu? Isije ikawa tunajadiliana na mtu ambaye ni 'half-mad' or completely illiterate and ignorant.
Kuambuka: "No research no right to speak." By Mao Zedong.
 
Mtu akiwa na laini moja ya simu kwa mwezi mmoja tu wa mwanzo, anakosaje mawasiliano?

Hii kusema mwezi ni extreme case tu, ila hata wakifanya laini moja kwa siku, itakuwa bado ni sawa tu, maana wakala tapeli hawezi kukusajilisha laini ya ziada kwa session moja..
Uhuru wa mawasiliano unajumuisha pia uchaguzi wa njia na namna ya kufanya mawasiliano hayo. Unapokandamiza njia ama namna ya mawasiliano unapiga kabali uhuru wa mawasiliano hayo. Ni sawa na wale walio na mawazo kuwa mitandao inaleta uchochezi kwa kuwa watu wanaongea mambo wasiyoyapenda, solution yake wakaanza kupendekeza tozo kwenye line za simu na kupandisha bei za vifurushi. civic space tayari inakuwa imebanwa sababu ya short sighted ya kutatua tatizo
 
Kwanza utujulishe, wewe binafsi una kiwango gani hasa cha elimu? Isije ikawa tunajadiliana na mtu ambaye ni 'half-mad' or completely illiterate and ignorant.
Kuambuka: "No research no right to speak." By Mao Zedong.
Onyesha madness , iliteracy na Ignorance yangu kwa kujibu hoja.
 
Uhuru wa mawasiliano unajumuisha pia uchaguzi wa njia na namna ya kufanya mawasiliano hayo. Unapokandamiza njia ama namna ya mawasiliano unapiga kabali uhuru wa mawasiliano hayo. Ni sawa na wale walio na mawazo kuwa mitandao inaleta uchochezi kwa kuwa watu wanaongea mambo wasiyoyapenda, solution yake wakaanza kupendekeza tozo kwenye line za simu na kupandisha bei za vifurushi. civic space tayari inakuwa imebanwa sababu ya short sighted ya kutatua tatizo
Kwani aliyezuia matumizi ya VPN si amefanya hivyo kwa mujibu wa sheria? Hata hili litafanyika kisheria kwa manufaa ya akina Marehemu mzee Ayo, au akina mzee Ayo hawana haki zinazopaswa kulindwa pia?

Tunaweza kuweka hata limit ya laini moja kwa siku, sio lazima kwa mwezi.
 
Wewe jibu hoja. Kwa kanuni hii mpya, Mtu anaikataa vipi laini ya simu aliyosajili mwenyewe kwa kuweka fingerprint?!
Siku hizi teknolojia imekuwa Sana, suala la fingerprints technology pia Sasa Lina muarabaini wake, kwa nchi za wenzetu walioendelea kiakili, kwa Sasa upo uwezekano wa mtu kuweza kurekebisha au kubadili kabisa fingerprints zake. Teknolojia hii tayari ipo, mwaka 2017 nikiwa kwenye nchi Fulani X, nilihudhuria mojawapo ya Mkutano wa Wataalamu kutoka UNESCO, ulikuwa Mkutano Maalumu kwa ajili ya kumpongeza na kumtambua Mgunduzi wa Teknolojia hiyo ya Mtu kuweza Kurekebisha na/au kubadili Fingerprints, Mgunduzi huyo wa teknolojia hiyo alikuwa kijana kabisa wa umri wa miaka 28 tu kwa wakati huo, ambaye pia alikuwa Mtafiti Mwanafunzi, na kwa kazi take hiyo kubwa ya Ugunduzi wa Teknolojia hiyo Mpya hapa duniani, pia aliweza kutunukiwa Uprofesa akiwa miongoni mwa watu ambao bado ni vijana wadogo zaidi hapa duniani kwa Karne hii ya 21. Jopo la Watqalamu wa UNESCO walitambua mchango wa Mgunduzi huyo kwa kazi yake hiyo.
 
Usajili wa line mpya za simu haujathibitiwa. Vijana wengi mno mitaani wasion hata na ofisi zijulikanazo hufanya shughuli hii. Ndio maana sio ajabu kitambulisho kimoja cha NIDA kinaweza kutumika kutoa line za ziada za simu pasipo mwenye line kujua - wanajifanya mashine haikusoma mara ya kwanza.

Usability uwe sio kiholela ilivyo sasa.
 
Kwani aliyezuia matumizi ya VPN si amefanya hivyo kwa mujibu wa sheria? Hata hili litafanyika kisheria kwa manufaa ya akina Marehemu mzee Ayo, au akina mzee Ayo hawana haki zinazopaswa kulindwa pia?

Tunaweza kuweka hata limit ya laini moja kwa siku, sio lazima kwa mwezi.
Hiyo akili iliyozuia vpn ndio akili hiyohiyo unaiendeleza hapa, na ungekuwa na sauti jf ungeshinikiza kusajili users wa jf kwa majina halisi bila kujua haki ya anonymity ni uhuru binafsi. Mzee Ayo Kuibiwa ni suala moja kubana uhuru wa kujieleza na mawasiliano ni suala jingine.
 
Hawa jamaa wanajuaje mtu kama unafanya muamala aisee
Screenshot_20241026-133502~2.png
 
Napendekeza kanuni mpya!

Kanuni mpya ni kwamba, NIDA moja hairuhusiwi kusajili zaidi ya namba moja kwa mwezi.

Sasa mtu NIDA yake ikitumika kufsnys utapeli kwa laini iliyosajiliwa baada ya kuanza kanuni hii mpya atatueleza, wakala alimsajilisha vipi namba ya ziada? Maana yake mwenye NIDA ndio tapeli. Na namba zote zaNIDA yake zitafungiwa hadi atoke shimoni akatoe maelezo polisi yeye mwenyewe, wala hatutamtafuta.

NB: haya ni mapendekezo yangu binafsi.
Akili za hovyo hizi. Kama namba inasajiliwa kwa nida na wanashindwa kuwapata wahusika wataweza lipi?
 
Kwanini? Utasemaje laini huitambui wakati uliweka finger print mwenyew?!
Kusajili line za simu kunafanyika kienyeji sana. Huwezi kutoa idhini kwa ''vishoka'' mtaani kuchukuwa fingerprints na data za wananchi halafu ukabaki salama. Haya mambo yalitakiwa kufanywa na organs kama polisi au sehemu maalum kukiwa na level ya juu ya utaalam. Nikija kwenye mada yako, tatizo kubwa la Tanzania ni kutokuwa na database ya taifa yenye orodha ya watanzania wote na wakazi wanaoishi Tanzania. Sizungumzii hivi vitambulisho vya NIDA, nazungumzia database ambayo inakuwa updated kila siku. Jambo la kwanza ilikuwa na kuchukuwa data za raia na wakazi wote na kuziweka kwenye database. (msiniambie ni jambo gumu kwa sababu teknolojia siku hizi imekua sana na fedha zipo plus nguvu kazi ya vijana wengi waliomaliza vyuo vikuu). Ukishakuwa na database kazi inakuwa rahisi kabisa, i.e ku-update kwa kuingiza vifo na waliozaliwa. Wanaotoka na kuingia ndani ya nchi systeam za mipakani zinafanya kazi. Zitungwe sheria kuwa bila jina lako kuwa kwenye database huwezi kupata huduma yoyote bila kibali maalum. Baada ya hapo database ndiyo inawezesha mambo mengine yote kama vitambulisho, leseni za magari, kupiga kura na kusajili mambo kama line za simu. Yaani ukitaka kitambulisho kwa mfano unakwenda na kukuta data zako tayari zipo unalipia na kupewa. Wakati wa kupiga kura wanajua automatically raia wenye sifa za kupiga kura ni wangapi na wanapelekewa reminders za kujisajili au wanapelekewa kadi za kupiga kura na siku ya kura wanakwenda wakiwa na kitambulisho na ile kadi. Ukitaka passport unakwenda na kitambulisho na kupewa bila kulazimika kujaza ma-fomu kibao
 
An argument from the short-sighted mind person.
Je, hilo ndiyo suluhisho sahihi la tatizo uliloeleza?
Je, umeshawahi kujiuliza ni kwa nini mtu ambaye siyo mmiliki wa akaunti yenye fedha kwenye benki yoyote ile hawezi kufanya muamala wa kutoa fedha kutoka kwa Mhasibu wa Benki bila ridhaa ya màandishi kutoka kwa mmiliki halali wa akaunti ya benki anayetambulika na benki husika? Umeshawahi kujiuliza swali hili?

Je, Hao matapeli wa mitandao ya simu huwa wanawezaje kutoa fedha kutoka kwa Namba ya simu iliyosajiliwa kwa utambulisho wa mtu mwingine bila ya kushitukiwa au bila ya kukamatwa? Is it possible?
Mbona kwenye benki wezi wa fedha zilizotolewa kwenye akaunti ya mtu huwa wanakua tracked na kuweza kukamatwa hata kama mwizi husika alifanya muamala wa wizi akiwa katika nchi nchi nyingine iliyopo mbali kwenye bara lingine hapa duniani? Kwa nini suala hili linashinsikana kwa upande wa mitandao ya simu hapa Tanzania??
Wewe binafsi bado unaamini kwamba hao wanaotakiwa kuzuia au kudhibiti tatizo hili la utapeli na wizi kwenye miamala ya mitandao ya simu hawahusiki kabisa kwenye kadhia hii??

Matahalani, kwenye miamala ya mabenki hapa duniani, kuna teknolojia zinazohusika na suala zima la miamala ya benki zilizopo ndani ya nchi fulani tu pekee na hata kuziunganisha na benki zingine zilizopo katika nchi zingine kwenye maeneo mbalimbali hapa duniani. Teknolojia hizi, kwa mfano teknolojia inayoitwa "SWIFT" kwa upande mwingine pia husaidia katika kuwatambua watu wanaofanya miamala ya benki kitaifa au kimataifa, na pia husaidia katika kuzuia uhalifu au hata kuwakamata wahalifu wa makosa yanayohusiana na miamala ya fedha kwenye mabenki au kwenye hizi taasisi za mitandao ya simu inayotoa huduma za ki-fedha (mobile money service providers). Je, suala Kama hili linashindikana vipi kufanyika hapa Tanzania?

Aidha, kwa kujibu wa taratibu za kimataifa za kuzuia au kudhibiti uhalifu wa fedha chafu au uhalifu wa utakatishaji wa fedha, taratibu ambazo zipo chini ya taasisi za Umoja wa Mataifa, yaani IMF, WB, WTO, n.k zinataka kwa LAZIMA kila nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa (UN) kuwa na taasisi maalumu itayokuwa inahusika na Usimamizi, Uzuiaji na/au Udhibiti wa Uhalifu wa Masuala ya ki-fedha, naamini kwamba Tanzania LAZIMA kuna taasisi ya namna hiyo Yaani "Financial Intelligence Unit (FIU)." Sasa; Je, hiyo FIU ya Tanzania kazi yake ni ipi Basi?? Kazi yake ni 'kusifu na kuabudu' watawala tu peke yake lakini siyo kuwabaini Wahalifu wa mitandao haramu ya fedha chafu???
Alafu matapeli wengi wa tuma namba hii hutumia laini za TTCL
 
Kusajili line za simu kunafanyika kienyeji sana. Huwezi kutoa idhini kwa ''vishoka'' mtaani kuchukuwa fingerprints na data za wananchi halafu ukabaki salama. Haya mambo yalitakiwa kufanywa na organs kama polisi au sehemu maalum kukiwa na level ya juu ya utaalam. Nikija kwenye mada yako, tatizo kubwa la Tanzania ni kutokuwa na database ya taifa yenye orodha ya watanzania wote na wakazi wanaoishi Tanzania. Sizungumzii hivi vitambulisho vya NIDA, nazungumzia database ambayo inakuwa updated kila siku. Jambo la kwanza ilikuwa na kuchukuwa data za raia na wakazi wote na kuziweka kwenye database. (msiniambie ni jambo gumu kwa sababu teknolojia siku hizi imekua sana na fedha zipo plus nguvu kazi ya vijana wengi waliomaliza vyuo vikuu). Ukishakuwa na database kazi inakuwa rahisi kabisa, i.e ku-update kwa kuingiza vifo na waliozaliwa. Wanaotoka na kuingia ndani ya nchi systeam za mipakani zinafanya kazi. Zitungwe sheria kuwa bila jina lako kuwa kwenye database huwezi kupata huduma yoyote bila kibali maalum. Baada ya hapo database ndiyo inawezesha mambo mengine yote kama vitambulisho, leseni za magari, kupiga kura na kusajili mambo kama line za simu. Yaani ukitaka kitambulisho kwa mfano unakwenda na kukuta data zako tayari zipo unalipia na kupewa. Wakati wa kupiga kura wanajua automatically raia wenye sifa za kupiga kura ni wangapi na wanapelekewa reminders za kujisajili au wanapelekewa kadi za kupiga kura na siku ya kura wanakwenda wakiwa na kitambulisho na ile kadi. Ukitaka passport unakwenda na kitambulisho na kupewa bila kulazimika kujaza ma-fomu kibao
Hakuna Mifumo thabiti ya Utambuzi wa Watu kwenye hizi nchi zetu hizi za ki-Afrika. Suala hili limefanywa kwa makusudi na baadhi ya Watawala wahalifu ili kuweza kujinufaisha binafsi wao wenyewe wakiwa madarakani. Mathalani, watawala wamekuwa wakivuruga makusudi mifumo ya utambuzi wa Watu katika nchi zao kwa nia ovu ya kutaka kuiba kura nyakati za Uchaguzi wa siasa, ili kuendesha biashara haramu ya binadamu, magendo na uhalifu katika masuala ya utakatishaji fedha chafu, kufanikisha biashara zao za madawa ya kulevya, na kufanikisha biashara haramu za kumiliki na kuendesha Magenge ya Uhalifu. Mfano mzuri zaidi kwenye suala hili ni uendeshaji wa biashara haramu ya magenge ya Utekaji watu na kuomba "Kikombozi" kutoka kwa Wanandugu wa Mtekwaji (abductees that kept into hostage camps) inayofanywa na baadhi ya Watawala wahalifu nchini Nigeria kupitia kwa Magenge ya Wanamgambo wa Boko Haram.
NB: Nchi ya Nigeria ina idadi ya watu wapatao zaidi ya Milioni 200 ambao wanaishi nchini humo, lakini watu ambao wamesajiliwa rasmi kwenye database ya raia wakazi wa nchi hiyo hawafiki hata idadi ya watu Milioni 22 nchini kote. Aidha, hata SIM cards za simu zilizosajiliwa rasmi kwa utambulisho rasmi ulio halali hazifiki hata Milioni Kumi kwenye nchi hiyo yote kabisa.
That's why Nigeria kuna uhalifu mwingi Sana, na ni vigumu Sana kuwatambua wahalifu hao.
 
Back
Top Bottom