‘Tuma kwa namba hii’ wapatiwa muarubaini, mwisho wao umefika

‘Tuma kwa namba hii’ wapatiwa muarubaini, mwisho wao umefika

Waweke tuu mfumo wa kuhakiki line za simu Kila baada ya miezi mitatu,kama line yako Ina issue wakudake moja kwa moja
 
Mfano mtu akifa Huwa anaondoka vipi kwenye data base ,ni nani anamfuta kwenye system?
 
Huwezi kufanya hivyo kwa sababu watu wana clone namba za simu. Hujawahi kuambiwa wat wanapata messege toka namba yako wakiomba helana wewe hujatuma hizo mesjesi? Sasa huoni utafungia watu NIDA wasio na hatia? Kwa hiyo pendekezo lako ni null and void, asante hata hivyo kwa kujaribu
Huyo ana uelewa mdogo Sana kwenye masuala haya aliyoleta hapa.

Utapeli wa "Phone Spoofing" ni janga kubwa sana kwa hapa Tanzania. Watu wamekuwa wakighushi Namba za simu za Watu wengine na kisha wanatuma meseji feki za kutaka kuwatapeli watu fedha. Mleta mada hajui kuhusu suala hili.
 
Tatizo sio kwa watu tatizo liko kwa serikali. Serikali ya Tanzania kuanzia kipindi cha Magufuli mpaka sasa utapeli umekuwa mwingi sana.
Wanaokopesha mikopo feki zaidi ya mia
Wanaotoa ajira fake zaidi ya mia
Utapeli ni biashara inayolipa sana Tanzania
Police na mahakama ni miongoni mwa taasisi za umma zenye watumishi wanaolipwa pesa ndogo sana.
Tapeli mmoja alifanya attempt ya kunitapeli nikamwambia nitakufunga akaniambia tunashikwa kila siku tunatoa pesa tunaachiwa.
Mahakamani tunatoa pesa kesi inapotea.
Akasema kuwa wao (matapeli) wana pesa.
Ungetoa mwarobaini wa kudhibiti wizi wa dawa kwenye hospital za umma, wizi wa fedha kwenye miradi ya umma , ungekemea pia tabia za viongozi kuchukua check za misaada na kugeanya pesa.
Kuna workmate wangu hapa job account yake ndani ya wiki 2 mafisadi wameitumia kupitishia karibu bilion . Yeye anapata jumbe tu pesa imeingia, pesa imetoka
 
IMG_2106.jpeg
 
Siku hizi teknolojia imekuwa Sana, suala la fingerprints technology pia Sasa Lina muarabaini wake, kwa nchi za wenzetu walioendelea kiakili, kwa Sasa upo uwezekano wa mtu kuweza kurekebisha au kubadili kabisa fingerprints zake. Teknolojia hii tayari ipo, mwaka 2017 nikiwa kwenye nchi Fulani X, nilihudhuria mojawapo ya Mkutano wa Wataalamu kutoka UNESCO, ulikuwa Mkutano Maalumu kwa ajili ya kumpongeza na kumtambua Mgunduzi wa Teknolojia hiyo ya Mtu kuweza Kurekebisha na/au kubadili Fingerprints, Mgunduzi huyo wa teknolojia hiyo alikuwa kijana kabisa wa umri wa miaka 28 tu kwa wakati huo, ambaye pia alikuwa Mtafiti Mwanafunzi, na kwa kazi take hiyo kubwa ya Ugunduzi wa Teknolojia hiyo Mpya hapa duniani, pia aliweza kutunukiwa Uprofesa akiwa miongoni mwa watu ambao bado ni vijana wadogo zaidi hapa duniani kwa Karne hii ya 21. Jopo la Watqalamu wa UNESCO walitambua mchango wa Mgunduzi huyo kwa kazi yake hiyo.
Sasa ukibadilisha fingerprint yako si itakataa kusomana na ile iliyopo NIDA? Utasajili vipi laini sasa?
 
Usajili wa line mpya za simu haujathibitiwa. Vijana wengi mno mitaani wasion hata na ofisi zijulikanazo hufanya shughuli hii. Ndio maana sio ajabu kitambulisho kimoja cha NIDA kinaweza kutumika kutoa line za ziada za simu pasipo mwenye line kujua - wanajifanya mashine haikusoma mara ya kwanza.

Usability uwe sio kiholela ilivyo sasa.
Kwa kutumia kanuni hii mpya, hayo yote yatakomeshwa!
 
Hiyo akili iliyozuia vpn ndio akili hiyohiyo unaiendeleza hapa, na ungekuwa na sauti jf ungeshinikiza kusajili users wa jf kwa majina halisi bila kujua haki ya anonymity ni uhuru binafsi. Mzee Ayo Kuibiwa ni suala moja kubana uhuru wa kujieleza na mawasiliano ni suala jingine.
Hakuna uhuru wowote wa mawasialiano unaobanwa kwa mtu kusajilishwa laini moja kwa siku…, kwani ukisajili leo laini moja, halafu kesho nyingine kwa ajili ya usalama wako, kuna tatizo gani?
 
Akili za hovyo hizi. Kama namba inasajiliwa kwa nida na wanashindwa kuwapata wahusika wataweza lipi?
Huwa wanashindwa kuwapata wagusika sababu watu husajilishwa laini za ziada bila wao kujua, hivyo zikifanya utapeli hiwezi kujua ni nani kafanya. Ila kwa kanuni hii mpya hili litafika mwisho!
 
Napendekeza kanuni mpya!

Kanuni mpya ni kwamba, NIDA moja hairuhusiwi kusajili zaidi ya namba moja kwa mwezi.

Sasa mtu NIDA yake ikitumika kufsnys utapeli kwa laini iliyosajiliwa baada ya kuanza kanuni hii mpya atatueleza, wakala alimsajilisha vipi namba ya ziada? Maana yake mwenye NIDA ndio tapeli. Na namba zote zaNIDA yake zitafungiwa hadi atoke shimoni akatoe maelezo polisi yeye mwenyewe, wala hatutamtafuta.

NB: haya ni mapendekezo yangu binafsi.
Napenda kukwambia tu,uhalifu hauwezi kuisha hata uweke sheria kutoka china au north korea za kupiga au kuchinja hadharani.

Hata ukipiga marufuku kusajili mwisho line moja tu watu watapigwa kama kawaida...wahalifu "wanabinwu mbwinu" mpya kila siku.
 
Kuna kitu natamani kuandika kuishauri serikali yangu juu ya hili jambo Nina njia ya kudhibiti.
Hila ni maelezo marefu sana yanaitaji kufungulia thread kabisa nikitulia najua inakuwaje mana nishawai piga u _freelancer najua vijana wanafanyaje kupiga mshindo wa camishen na matobo ya mitandao ya simu yanavyowapa mianya vijana.
 
Hakuna uhuru wowote wa mawasialiano unaobanwa kwa mtu kusajilishwa laini moja kwa siku…, kwani ukisajili leo laini moja, halafu kesho nyingine kwa ajili ya usalama wako, kuna tatizo gani?
Usivyovijua kubali kushindwa, hujui unachoongelea kwa misingi ya kanuni za haki za kiraia. Na ndio sababu unabadilika badilika umeanza na mwezi, nikakupa scenario ya mwaka ama miaka kumi, umerudi na siku.
 
Naungana na mtoa hoja💯 Kwa maboresho ya hoja napendekeza.
Iwe marufuku kuwa na lakini zaidi ya Moja Kwa mtandao Mmoja ikilazimika Kwa matumizi ya data hizi laini zisirusiwe kupiga simu au kutuma message (kampuni au wafanya biashara wanaweza kupewa utaratibu maalumu kanuni inaweza bana biashara kirahisi kama zitatukuka siyo.

Iwe ni wajibu wa msajiri kutunza viambatanisho vya msajiriwa, lengo ni kuwasumbua Hawa mawakala wezi wanaowasajiri vibaka wenzao. Ikijulikana tu namba iliyofanya utapeli ilisajiriwa kwako you are in for it.

TCRA Kwa sababu wanauwezo kusoma message zetu wakipenda, na Siku hizi watu mambo yao ya Siri hawatumii message bali Whatsapp na Telegram basi waweke system inayo chakata kila msg taking advantage ya AI aka Akili Mnemba(yule robot wa Nape sijui anaitwa nani) ndio sehemu zake Sasa hizi itumike to analyze and block the numbers with fraudulent contents/intention. Same hiyo number ya nida inakuwa shared Kwa taasisi nyingine zinaiblock kwenye mitandao yote ya simu, mabank, bima ya afya, leseni, taasisi za elimu, kote huko anapigwa pini. Baada ya hapo watapungua na kuisha.

Pia iwe agenda kwenye mkutano ya wanasiasa hasa tupoelekea uchaguzi mkuu kutoa elimu ya kuzuia na kuzibiti utapeli wa mtandao.
 
Napenda kukwambia tu,uhalifu hauwezi kuisha hata uweke sheria kutoka china au north korea za kupiga au kuchinja hadharani.

Hata ukipiga marufuku kusajili mwisho line moja tu watu watapigwa kama kawaida...wahalifu "wanabinwu mbwinu" mpya kila siku.
Sawa, wacha wabuni mbinu mpya. Ila kwa mbinu za sasa, huu ndio muarobaini.
 
Usivyovijua kubali kushindwa, hujui unachoongelea kwa misingi ya kanuni za haki za kiraia. Na ndio sababu unabadilika badilika umeanza na mwezi, nikakupa scenario ya mwaka ama miaka kumi, umerudi na siku.
Nilisema toka awali, mwezi ni extreme case niliyotolea mfano, na nikasema hata ikawa laini moja kwa siku bado ni sawa tu, sababu hataweza kukusajilisha laini za ziada bila wewe kujua..

Sasa kuna tatizo au ubaya gani mtu akasajili laini moja kwa siku?
 
Kubabake namaliza kusoma nyuzi..tu Kuna huyu fala nae kajileta wemtoa Uzi mchawi nini..
 

Attachments

  • Screenshot_2024-10-27-14-24-14-04.png
    Screenshot_2024-10-27-14-24-14-04.png
    159.9 KB · Views: 2
Ila huu ujinga unalelewa tu mkuu. Mfano, wangesema kila ambae nida yake imetumika katika namba asiyoijua basi awasilishe hiyo namba na wakala atafutwe ajibu tuhuma hizo lasivyo wakala husika anafungiwa usajili hii na kifungo juu basi michezo ingepungua kwa kiwango kikubwa.

Sema taifa letu na namna za viongozi wetu ni vichekesho.
Exactly 💯
 
Back
Top Bottom