Tumalize Ubishi: Tundu Lissu nitajie IGA au BIT inayoeleza kutakuwa na HGA alafu bado inayoenesha kiwango cha uwekezaji na mgawanyo wa mapato?

Usihamishe magoli. Toa majibu acha longolongo
 
Rejea angalizo. Staking longolongo
 
Una tatizo la kupata elimu ya bure
 
Mwanasheria gani usiyejua kugusa pointi uende nayo straight..

Lissu umesoma nae......

Mambo aliyotoa ushauri Lissu..... wakati mwenzako ameshashinda kesi kibao mahakamani, wewe umewahi kushinda ngapi mpaka sasa?

Ooh IGA ni kama posa, sasa kama hiyo posa imeshakubaliwa, na mwarabu karuhusiwa kuchukua mke tangu October 2022 siku iliposainiwa, hiyo HGA yenu ina maana gani?

Halafu ulivyo hovyo kabisa, unaomba ruhusa kuchukua baadhi ya huu utumbo hapa, ili ukapandikize kwenye utumbo wako mwingine, mnatujazia bure server ya JF.
 
Mwanasheria gani usiyejua kugusa pointi uende nayo straight..

Lissu umesoma nae......

Mambo aliyotoa ushauri Lissu..... wakati mwenzako ameshashinda kesi kibao mahakamani, wewe umewahi kushinda ngapi mpaka sasa?
Sijawahi kupanda mahakamani!.
Ooh IGA ni kama posa, sasa kama hiyo posa imeshakubaliwa, na mwarabu karuhusiwa kuchukua mke tangu October 2022 siku iliposainiwa, hiyo HGA yenu ina maana gani?
IGA ni posa tuu, posa ikiisha kubaliwa, unapangiwa mahari (HGA), ukiisha lipa mahari, ndipo unakabidhiwa mke. Mwenye dada hakosi shemeji, IGA ni posa tu. Je, tuendelee kupiga kelele kuzozania posa, au tutulie tupange Mahari ya maana kwenye HGA?
Halafu ulivyo hovyo kabisa, unaomba ruhusa kuchukua baadhi ya huu utumbo hapa, ili ukapandikize kwenye utumbo wako mwingine, mnatujazia bure server ya JF.
Duh...!.
P
 
Kikubwa inatakiwa hizi hoja zijibiwe kwanza...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
1. Nionyeshe IGA au BIT yoyote ambayo inasainiwa na Kampuni badala ya state.
2. Nionyeshe IGA au BIT yoyote inayotaja miradi Phase 1, Phase 2 etc.
 

Hoja yako inafikirisha ati IGA ni kama "posa" na HGA ndio "mahari". Je, posa huwa na masharti kama yaliyomo kwenye IGA? Mkuu Paskali, kama mwanasheria, unajua uzito wa neno shall lilotumika kwenye baadhi ya vifungu.
 
Nina maswali kadhaa kwako ndugu mleta hoja;

1. Ndugu Lord denning, hivi Tanzania mpaka sasa tumeingia makubaliano ya mashirikiano (IGA)na Dubai pekee au zipo IGA za mashirikiano na nchi zingine pia kama Canada, Kenya, Uganda, USA nk nk?

2. Kama ziko IGA zingine, unadhani ni kwanini hii inapingwa na kuleta mjadala mkali unaotugawa kama taifa? Unadhani ni kwa sababu Rais Samia Suluhu Hassan ni muislam au Mzanzibari na kwa sababu hizi anafanyiwa mtima nyongo tu?

3. Je, unaweza kuleta IGA kati ya Tanzania na nchi nyingine yoyote mfano USA au Canada ili tujaribu kulinganisha na hii ya Dubai tuone shida iko wapi?




LA MWISHO NA LA MUHIMU ZAIDI NI HILI👇👇👇

4. Hii IGA inayoleta mjadala is very confusing. It's confusing because haiko specific and straight kiasi cha kuwaacha watu in dilemma Kwa kujiuliza kuwa hivi haya ni makubaliano ya mashirikiano ya kiuchumi na kijamii (interGovernmental Agreements - IGA) kati ya nchi na nchi au ni mkataba wa kibiashara (business contract) kati ya TPA na DP WORLD?..

Nakuuliza swali hili kwa sababu hata nyie watetezi wa hii kitu mnapata shida kueleweka kwa sababu haileweki mnatetea IGA au mkataba wa kibiashara kati ya Tanzania na DP world au nchi ya Dubai kiasi cha kujichanganya mara kwa mara. Hata Bunge la Dr Tulia asiyeweza kutulia mpaka sasa halijui lilipitisha mkataba au makubaliano..!!

Hata hivyo, maandishi hayo yanaonesha moja Kwa moja kuwa huo ni mkataba wa kibiashara kwa sababu unataja eneo specific ambalo DP world watakakalo deal nalo yaani UWEKEZAJI KATIKA BANDARI ZETU ZOTE..

Na kama ndiyo hivi, basi huu ni mkataba wa kibiashara na hivyo basi hoja na maswali ya tunaoukataa mkataba huo kuwa hauko sawa ni lazima yajibiwe ndani ya mkataba (kisheria tunasema mkataba sharti ujisemee na kujitetea wenyewe). Wewe Lord denning na wenzako hamwezi kutetea mkataba kama wenyewe hauwezi kujitetea....!!

Maswali yetu ni mengi. Lakini makubwa ni kama vile; hivi mwekezaji anakuja (wekeza kiasi gani?), ukomo wa mkataba, wajibu wa mwekezaji ni upi, na sisi kama nchi wajibu na haki zetu ni zipi, nini matarajio ya manufaa (ajira, mapato nk) tukayopata sisi kama nchi nk nk..

Lakini maswali ni mengi zaidi Kwa viongozi wetu. Mfano kama hili ni jambo zuri ikawaje kufanya kama Siri hadi mkataba huu ulipovujishwa tu na serikali kukurupuka kujifanya kupekeka bungeni? Ni wapi na lini tenda ya kukaribishwa wawekezaji kwenye bandari zetu ilitangazwa? Kampuni gani ziliomba? Kwanini ni bandari za upande mmoja tu wa muungano - Tanganyika wakati bandari ni suala la muungano? Kwanini mwekezaji apewe bandari zote za bahari na maziwa yetu??? Kwanini??

Mwisho, unahangaika bure ndugu Lord denning. Hii kitu iko very clear kwamba kuna shida mahali. Na shida kubwa ni rushwa Kwa viongozi wetu tuliowapa dhamana kutuongoza kwenda Kanaani, lakini cha ajabu hawa watu wametuongoza kututumbukiza kwenye shimo la uchafu..

Kama hutaki kuelewa, basi let's go to war na mwisho wa siku itajulikana mshindi ni nani. Je, ni hawa wajiitao viongozi wetu au ni wananchi wenye nchi yao. And just to remind you, NGUVU YA UMMA - WANANCHI haijawahi kushindwa..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…