Tumalize Ubishi: Tundu Lissu nitajie IGA au BIT inayoeleza kutakuwa na HGA alafu bado inayoenesha kiwango cha uwekezaji na mgawanyo wa mapato?

Tumalize Ubishi: Tundu Lissu nitajie IGA au BIT inayoeleza kutakuwa na HGA alafu bado inayoenesha kiwango cha uwekezaji na mgawanyo wa mapato?

Bado huoni ujuha mkubwa unaokusumbua hapa?

Wewe katika akili zako unaliona hilo jambo kuwa ndilo pekee linalopigiwa kelele kuhusu huo Mkataba, ambao hata nyinyi wenyewe mliukana toka mwanzo kuwa siyo mkataba bali ni makubaliano tu?

Hiyo IGA, siyo 'binding'. Yaliyomo humo hayaathiri chochote kitakachokuwemo huko HGA?

Sikunyingine ukinikaribisha kwenye andiko lako, jitahidi sana liwe la kiwango kinachostahili kujadiliwa, siyo longolongo kama hii uliyoweka hapa.
Usihamishe magoli. Toa majibu acha longolongo
 
Unawaita wewe kama nani?
Ficha ujinga wako nyumbani kwako
Acha kusumbua watu
Najua sheria sijui mimi meanasheria unashindwa mambo madogo
Okay Dubai ndio wapi na ni mdudu gani?
Bandari waache tuiendeshe wenyewe kwa hasara 60yrs mpaka sasa tupo sawa tu…
Nini mbaya na wewe?
Rejea angalizo. Staking longolongo
 
Mkataba wa bomba la mafuta Uganda mpaka Tanga umepita bungeni.

Mikataba ya manunuzi ya ndege yote imepita bungeni.

Mkataba wa bandari umepita bungeni na umekwenda mbali zaidi unajadiliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja na jamii nzima.

Wewe ndiye huelewi unayedhani mkataba unapaswa uwekwe wazi, kumbuka kuna mengi yanayoandikwa kwenye mikataba ambayo kampuni moja haipendi yajulikane kwa washindani wao wa kibiashara.
Una tatizo la kupata elimu ya bure
 
Mkuu Lord denning , kwanza asante kwa bandiko hili, pili kwa ruhusa yako, naomba kulitumia bandiko lako kama mbegu ya kuoteshea bandiko langu fulani, na kuzitumia hoja zako za humu kama shamba darasa la kuwafundisha watu humu kuhusu hii IGA.

Mimi na Lissu.
Kwanza nimesoma na TL Ilboru, nikiwa nimemtangulia, mimi nikiwa A level, TL akiwa O Level, mahali pekee tulipokuwa tunakutana na TL ni kwenye School Debate, TL ni mzuri sana kwenye debate, na pia upstairs is bright and brilliant!, nasisitiza TL ni mzuri, bright and brilliant, sheria anazijua but he is not the best!.

Nikiwa mwandishi wa habari, nimemripoti sana TL akiwa Leat. Hapa kati tukappteana, tukaja kukutana Atlanta nchini Marekani, yeye akiwa na yake, na mimi nikiwa na yangu.

Tuliporejea nchini, tukawa tuna interacts kwenye siasa yeye akiwa mbunge na kiongozi wa Chadema, mimi nikiwa mwandishi wa habari wa kujitegemea.

Kwenye hili la DPW, naamini TL anaujua ukweli ila anapotosha kwa makusudi for political mileage!.

Mtu ukiujua ukweli, halafu unapotosha kwa makusudi, hii maana yake ni kuwafanya wengine wote ni wajinga!.

Kwa vile yeye ndiye mwanasheria Mkuu wa Chadema, Chadema waamtegemea sana, wana mwamini sana, na matokeo yake mara kibao, amewaingiza chaka na kuja kuigharimu sana Chadema!.

Kusomea sheria, LL.B, Kuwa na Uwezo Mkubwa wa Kujieleza, na Kuwa Mwanasheria Mzuri, ni vitu viwili tofauti!.

TL ni msomi mzuri wa sheria, ni mzoefu mwenye long experience ya uzoefu wa muda mrefu, mwenye uwezo mkubwa wa kujieleza, he is very assertive kwa kutumia hoja za nguvu, (kulazimisha) badala ya kutumia nguvu za hoja!.

Naomba niwape baadhi ya mifano michache ya jinsi TL alivyo toa ushauri mbaya wa kisheria kwa kuishauri Chadema kwenye issues za kisheria, ushauri ambao umeigharimu sana Chadema, kwa kujua au kutojua!.
  1. Issue ya Bunge la Katiba - Serikali ilipoleta muswada wa sheria ya kuanzisha mchakato wa katiba mpya, Chadema kama the main opposition party, kiiliupinga mchakato huo, kwa maneno, TL kama mnadhimu mkuu wa opposition Bungeni, badala ya kuwasisha pingamizi kuuzuia muswada huo usisonge mbele, TL aliwasilisha go ahead yenye tamko tunapinga!, hivyo kuwaingiza chaka Chadema!. Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele! that was a mistake
  2. Chadema ina katiba yake, katiba hiyo ilikuwa na kipengele cha ukomo wa uongozi ni vipindi viwili vya miaka 5, jumla ni miaka 10!, lakini mwaka 2006 ni TL na watu fulani ambao naomba nisiwataje walikinyofoa hicho kipengele, kinyemela bila kufuata utaratibu rasmi wowote wa mabadiliko ya katiba!, Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA
  3. katiba hiyo ina utaratibu wa nidhamu, msimamizi mkuu wa kuhakikisha Chadema inaeshwa kwa mujibu katiba ni TL, lakini yeye ndiye mtu wa mstari wa mbele kutowatendea haki wanachama wao ile 2013, ni TL ndiye aliyesimamia dhulma hii Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!
  4. Waraka wa Mabadiliko - kuna wengi wanadhani siasa ni blah blah tuu!, lakini ukweli ni kweli kuna siasa za blah blah, uongo, fitna na majungu, na kuna siasa za ukweli ambazo sio blah blah, bali siasa za Sayansi ya siasa, Political Science, ule waraka wa mabadiliko ni waraka wenye hoja za ukweli za siasa za ukweli, but very unfortunately Chadema are too blind to see!, wakaita ni usaliti, na kuwatimua Zitto, Prof. Kitila na Mwigamba, hivyo kumpoteza think tank wa Chadema.
  5. TL ndiye aliyeshadadia sana kumtimua Zitto, TL kama mwanasheria anajua kabisa CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya NKM, lakini Chadema ilimtimua tuu. Nikawapa angalizo Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!" ni kweli karma iliwashughukia!.
  6. Chadema ilijinasibu kuupinga udikiteta kwa kufanya maandamano na mikutano ya hadhara, hoja ya udikiteta sio hoja ya kisiasa ni hoja ya kisheria, hivyo solutions ya udikiteta sio mikutano ya hadhara na maandamano Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele!
  7. Kuna vitu vinafanywa kisheria, kikanuni na kiutaratibu, moja ya vitu hivyo ni chaguzi mbalimbali , kwenye uchaguzi wa Wabunge wa EALA, Chadema kilishindwa kufuata taratibu, TL akawashauri Chadema waende mahakamani kupinga uchaguzi ule!, ni mimi ndiye niliye waokoa kwa bandiko hili CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue, Serious Issue ya Katiba ni UKUTA!.
  8. Issue ya kina Halima Mdee, ni kama issue ya Zitto, kwa mujibu wa katiba ya Chadema, CC ya Chadema haina mamlaka ya kumtimua Mdee, lakini CC ya Chadema, ikakaa kama a kangaroo court na kuwatimua, kwa sasa kesi iko mahakamani, japo huko mahakamani watashindwa, The Voices From Within: "Mahakamani Watashindwa Tena!" Sababu ni Mawakili! Jee Tanzania Tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?Jitokezeni Kusaidia! cha moto cha karma ya dhulma hii, Chadema watakipata!.
  9. Kiongozi fulani wa Chadema, kafanya jinai, akahifadhiwa mahali , kesi ikaunguruma, Mahakama ikathibitisha uwepo wa prima facie!. Wakajitokeza kina Askofu Makarios wetu, kumuombea msamaha, TL akawagomea!. Tukamshauri Mama asamehe tu hata bila kuombwa msamaha, Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?
  10. Mama akasamehe na kuanza vikao vya maridhiano, wakakubaliana kugawana nusu mkate, TL hataki maridhiano, anataka confrontations!, Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?
Hivyo kwenye hili la hii IGA, ni kweli IGA inamatatizo ya kisheria kama walivyo ainisha wanasheria na watu mbalimbali, nikiwemo mimi, Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

IGA ni kama barua tuu ya posa, mahari ni HGA, kama mahari ni kumnunua binti, then bandari imeuzwa, lakini kama mahari ni consideration ya kumpata mke, hakuna hata milimita moja ya Bandari yetu iliyouzwa!. Tuyazungumze matatizo ya IGA bila upotoshaji na badala yake tufanye uendeshaji umma ili mwisho wa siku tupate HGA nzuri.
P
Mwanasheria gani usiyejua kugusa pointi uende nayo straight..

Lissu umesoma nae......

Mambo aliyotoa ushauri Lissu..... wakati mwenzako ameshashinda kesi kibao mahakamani, wewe umewahi kushinda ngapi mpaka sasa?

Ooh IGA ni kama posa, sasa kama hiyo posa imeshakubaliwa, na mwarabu karuhusiwa kuchukua mke tangu October 2022 siku iliposainiwa, hiyo HGA yenu ina maana gani?

Halafu ulivyo hovyo kabisa, unaomba ruhusa kuchukua baadhi ya huu utumbo hapa, ili ukapandikize kwenye utumbo wako mwingine, mnatujazia bure server ya JF.
 
Mwanasheria gani usiyejua kugusa pointi uende nayo straight..

Lissu umesoma nae......

Mambo aliyotoa ushauri Lissu..... wakati mwenzako ameshashinda kesi kibao mahakamani, wewe umewahi kushinda ngapi mpaka sasa?
Sijawahi kupanda mahakamani!.
Ooh IGA ni kama posa, sasa kama hiyo posa imeshakubaliwa, na mwarabu karuhusiwa kuchukua mke tangu October 2022 siku iliposainiwa, hiyo HGA yenu ina maana gani?
IGA ni posa tuu, posa ikiisha kubaliwa, unapangiwa mahari (HGA), ukiisha lipa mahari, ndipo unakabidhiwa mke. Mwenye dada hakosi shemeji, IGA ni posa tu. Je, tuendelee kupiga kelele kuzozania posa, au tutulie tupange Mahari ya maana kwenye HGA?
Halafu ulivyo hovyo kabisa, unaomba ruhusa kuchukua baadhi ya huu utumbo hapa, ili ukapandikize kwenye utumbo wako mwingine, mnatujazia bure server ya JF.
Duh...!.
P
 
Kikubwa inatakiwa hizi hoja zijibiwe kwanza...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Nimemsikia Lissu akiyasema makubaliano yetu ya Tanzania na Dubai hayaoneshi kiwango cha uwekezaji utakaofanywa na mgawanyo wa mapato, akitumia hiyo kama moja ya sababu ya kuyaponda makubaliano tuliyoingia na Dubai kuhusu masuala ya uwekezaji.

Lissu anasema haya huku nikiwa na uhakika kuwa anapotosha kwa sababu najua kwa hakika kuwa anajua IGA au BIT ikiwa imetoa nafasi ya kuwepo kwa HGA haiwezi kuzungumzia uwekezaji husika na mgawanyo wa mapato kwa kuwa HGA ndo mkataba wa uwekezaji mahsusi ambao ndiyo unaoonesha aina ya uwekezaji, kiwango cha uwekezaji na mgawanyo wa mapato.

Pili najua kuwa amesoma IGA yetu na Dubai na anajua imeeleza katika Ibara ya kwanza sehemu ya pili kuwa Kutakuwa na Mikataba Mahsusi ya Uwekezaji baina ya Tanzania na Dubai ambayo inaeleza haki na wajibu wa kila upande.
View attachment 2701848

Kwa kuwa najua Tundu Lissu yupo humu na nina uhakika atasoma huu uzi. Leo nataka atuambie humu.

Kuna IGA au BIT gani iliyowahi kuingiwa Duniani (POPOTE PALE) ambayo imetoa nafasi ya kuingiwa kwa HGA ( Mkataba mahsusi wa uwekezaji) alafu still ikaonyesha kiwango cha uwekezaji, aina ya uwekezaji na mgawanyo wa mapato?

Ninaweka ahadi apa! Endapo Tundu Lissu atajibu hili swali au mtu yeyote atajibu hili swali kwa ufasaha na kama nilivyouliza basi nitakuja na Verified ID humu.

Ifike kipindi sasa aache kuwadanganya watu kwa kuwa tu hawana uelewa wa mambo!

Tundu Lissu & Co nawasubiri humu.

Angalizo. Muje na Majibu sio longolongo.


Nawasubiri!!
1. Nionyeshe IGA au BIT yoyote ambayo inasainiwa na Kampuni badala ya state.
2. Nionyeshe IGA au BIT yoyote inayotaja miradi Phase 1, Phase 2 etc.
 
Sijawahi kupanda mahakamani!.

IGA ni posa tuu, posa ikiisha kubaliwa, unapangiwa mahari (HGA), ukiisha lipa mahari, ndipo unakabidhiwa mke. Mwenye dada hakosi shemeji, IGA ni posa tu. Je, tuendelee kupiga kelele kuzozania posa, au tutulie tupange Mahari ya maana kwenye HGA?

Duh...!.
P

Hoja yako inafikirisha ati IGA ni kama "posa" na HGA ndio "mahari". Je, posa huwa na masharti kama yaliyomo kwenye IGA? Mkuu Paskali, kama mwanasheria, unajua uzito wa neno shall lilotumika kwenye baadhi ya vifungu.
 
Nina maswali kadhaa kwako ndugu mleta hoja;

1. Ndugu Lord denning, hivi Tanzania mpaka sasa tumeingia makubaliano ya mashirikiano (IGA)na Dubai pekee au zipo IGA za mashirikiano na nchi zingine pia kama Canada, Kenya, Uganda, USA nk nk?

2. Kama ziko IGA zingine, unadhani ni kwanini hii inapingwa na kuleta mjadala mkali unaotugawa kama taifa? Unadhani ni kwa sababu Rais Samia Suluhu Hassan ni muislam au Mzanzibari na kwa sababu hizi anafanyiwa mtima nyongo tu?

3. Je, unaweza kuleta IGA kati ya Tanzania na nchi nyingine yoyote mfano USA au Canada ili tujaribu kulinganisha na hii ya Dubai tuone shida iko wapi?




LA MWISHO NA LA MUHIMU ZAIDI NI HILI👇👇👇

4. Hii IGA inayoleta mjadala is very confusing. It's confusing because haiko specific and straight kiasi cha kuwaacha watu in dilemma Kwa kujiuliza kuwa hivi haya ni makubaliano ya mashirikiano ya kiuchumi na kijamii (interGovernmental Agreements - IGA) kati ya nchi na nchi au ni mkataba wa kibiashara (business contract) kati ya TPA na DP WORLD?..

Nakuuliza swali hili kwa sababu hata nyie watetezi wa hii kitu mnapata shida kueleweka kwa sababu haileweki mnatetea IGA au mkataba wa kibiashara kati ya Tanzania na DP world au nchi ya Dubai kiasi cha kujichanganya mara kwa mara. Hata Bunge la Dr Tulia asiyeweza kutulia mpaka sasa halijui lilipitisha mkataba au makubaliano..!!

Hata hivyo, maandishi hayo yanaonesha moja Kwa moja kuwa huo ni mkataba wa kibiashara kwa sababu unataja eneo specific ambalo DP world watakakalo deal nalo yaani UWEKEZAJI KATIKA BANDARI ZETU ZOTE..

Na kama ndiyo hivi, basi huu ni mkataba wa kibiashara na hivyo basi hoja na maswali ya tunaoukataa mkataba huo kuwa hauko sawa ni lazima yajibiwe ndani ya mkataba (kisheria tunasema mkataba sharti ujisemee na kujitetea wenyewe). Wewe Lord denning na wenzako hamwezi kutetea mkataba kama wenyewe hauwezi kujitetea....!!

Maswali yetu ni mengi. Lakini makubwa ni kama vile; hivi mwekezaji anakuja (wekeza kiasi gani?), ukomo wa mkataba, wajibu wa mwekezaji ni upi, na sisi kama nchi wajibu na haki zetu ni zipi, nini matarajio ya manufaa (ajira, mapato nk) tukayopata sisi kama nchi nk nk..

Lakini maswali ni mengi zaidi Kwa viongozi wetu. Mfano kama hili ni jambo zuri ikawaje kufanya kama Siri hadi mkataba huu ulipovujishwa tu na serikali kukurupuka kujifanya kupekeka bungeni? Ni wapi na lini tenda ya kukaribishwa wawekezaji kwenye bandari zetu ilitangazwa? Kampuni gani ziliomba? Kwanini ni bandari za upande mmoja tu wa muungano - Tanganyika wakati bandari ni suala la muungano? Kwanini mwekezaji apewe bandari zote za bahari na maziwa yetu??? Kwanini??

Mwisho, unahangaika bure ndugu Lord denning. Hii kitu iko very clear kwamba kuna shida mahali. Na shida kubwa ni rushwa Kwa viongozi wetu tuliowapa dhamana kutuongoza kwenda Kanaani, lakini cha ajabu hawa watu wametuongoza kututumbukiza kwenye shimo la uchafu..

Kama hutaki kuelewa, basi let's go to war na mwisho wa siku itajulikana mshindi ni nani. Je, ni hawa wajiitao viongozi wetu au ni wananchi wenye nchi yao. And just to remind you, NGUVU YA UMMA - WANANCHI haijawahi kushindwa..!!
 
Back
Top Bottom