Mkuu
Lord denning , kwanza asante kwa bandiko hili, pili kwa ruhusa yako, naomba kulitumia bandiko lako kama mbegu ya kuoteshea bandiko langu fulani, na kuzitumia hoja zako za humu kama shamba darasa la kuwafundisha watu humu kuhusu hii IGA.
Mimi na Lissu.
Kwanza nimesoma na TL Ilboru, nikiwa nimemtangulia, mimi nikiwa A level, TL akiwa O Level, mahali pekee tulipokuwa tunakutana na TL ni kwenye School Debate, TL ni mzuri sana kwenye debate, na pia upstairs is bright and brilliant!, nasisitiza TL ni mzuri, bright and brilliant, sheria anazijua but he is not the best!.
Nikiwa mwandishi wa habari, nimemripoti sana TL akiwa Leat. Hapa kati tukappteana, tukaja kukutana Atlanta nchini Marekani, yeye akiwa na yake, na mimi nikiwa na yangu.
Tuliporejea nchini, tukawa tuna interacts kwenye siasa yeye akiwa mbunge na kiongozi wa Chadema, mimi nikiwa mwandishi wa habari wa kujitegemea.
Kwenye hili la DPW, naamini TL anaujua ukweli ila anapotosha kwa makusudi for political mileage!.
Mtu ukiujua ukweli, halafu unapotosha kwa makusudi, hii maana yake ni kuwafanya wengine wote ni wajinga!.
Kwa vile yeye ndiye mwanasheria Mkuu wa Chadema, Chadema waamtegemea sana, wana mwamini sana, na matokeo yake mara kibao, amewaingiza chaka na kuja kuigharimu sana Chadema!.
Kusomea sheria, LL.B, Kuwa na Uwezo Mkubwa wa Kujieleza, na Kuwa Mwanasheria Mzuri, ni vitu viwili tofauti!.
TL ni msomi mzuri wa sheria, ni mzoefu mwenye long experience ya uzoefu wa muda mrefu, mwenye uwezo mkubwa wa kujieleza, he is very assertive kwa kutumia hoja za nguvu, (kulazimisha) badala ya kutumia nguvu za hoja!.
Naomba niwape baadhi ya mifano michache ya jinsi TL alivyo toa ushauri mbaya wa kisheria kwa kuishauri Chadema kwenye issues za kisheria, ushauri ambao umeigharimu sana Chadema, kwa kujua au kutojua!.
- Issue ya Bunge la Katiba - Serikali ilipoleta muswada wa sheria ya kuanzisha mchakato wa katiba mpya, Chadema kama the main opposition party, kiiliupinga mchakato huo, kwa maneno, TL kama mnadhimu mkuu wa opposition Bungeni, badala ya kuwasisha pingamizi kuuzuia muswada huo usisonge mbele, TL aliwasilisha go ahead yenye tamko tunapinga!, hivyo kuwaingiza chaka Chadema!. Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele! that was a mistake
- Chadema ina katiba yake, katiba hiyo ilikuwa na kipengele cha ukomo wa uongozi ni vipindi viwili vya miaka 5, jumla ni miaka 10!, lakini mwaka 2006 ni TL na watu fulani ambao naomba nisiwataje walikinyofoa hicho kipengele, kinyemela bila kufuata utaratibu rasmi wowote wa mabadiliko ya katiba!, Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA
- katiba hiyo ina utaratibu wa nidhamu, msimamizi mkuu wa kuhakikisha Chadema inaeshwa kwa mujibu katiba ni TL, lakini yeye ndiye mtu wa mstari wa mbele kutowatendea haki wanachama wao ile 2013, ni TL ndiye aliyesimamia dhulma hii Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!
- Waraka wa Mabadiliko - kuna wengi wanadhani siasa ni blah blah tuu!, lakini ukweli ni kweli kuna siasa za blah blah, uongo, fitna na majungu, na kuna siasa za ukweli ambazo sio blah blah, bali siasa za Sayansi ya siasa, Political Science, ule waraka wa mabadiliko ni waraka wenye hoja za ukweli za siasa za ukweli, but very unfortunately Chadema are too blind to see!, wakaita ni usaliti, na kuwatimua Zitto, Prof. Kitila na Mwigamba, hivyo kumpoteza think tank wa Chadema.
- TL ndiye aliyeshadadia sana kumtimua Zitto, TL kama mwanasheria anajua kabisa CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya NKM, lakini Chadema ilimtimua tuu. Nikawapa angalizo Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!" ni kweli karma iliwashughukia!.
- Chadema ilijinasibu kuupinga udikiteta kwa kufanya maandamano na mikutano ya hadhara, hoja ya udikiteta sio hoja ya kisiasa ni hoja ya kisheria, hivyo solutions ya udikiteta sio mikutano ya hadhara na maandamano Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele!
- Kuna vitu vinafanywa kisheria, kikanuni na kiutaratibu, moja ya vitu hivyo ni chaguzi mbalimbali , kwenye uchaguzi wa Wabunge wa EALA, Chadema kilishindwa kufuata taratibu, TL akawashauri Chadema waende mahakamani kupinga uchaguzi ule!, ni mimi ndiye niliye waokoa kwa bandiko hili CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue, Serious Issue ya Katiba ni UKUTA!.
- Issue ya kina Halima Mdee, ni kama issue ya Zitto, kwa mujibu wa katiba ya Chadema, CC ya Chadema haina mamlaka ya kumtimua Mdee, lakini CC ya Chadema, ikakaa kama a kangaroo court na kuwatimua, kwa sasa kesi iko mahakamani, japo huko mahakamani watashindwa, The Voices From Within: "Mahakamani Watashindwa Tena!" Sababu ni Mawakili! Jee Tanzania Tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?Jitokezeni Kusaidia! cha moto cha karma ya dhulma hii, Chadema watakipata!.
- Kiongozi fulani wa Chadema, kafanya jinai, akahifadhiwa mahali , kesi ikaunguruma, Mahakama ikathibitisha uwepo wa prima facie!. Wakajitokeza kina Askofu Makarios wetu, kumuombea msamaha, TL akawagomea!. Tukamshauri Mama asamehe tu hata bila kuombwa msamaha, Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?
- Mama akasamehe na kuanza vikao vya maridhiano, wakakubaliana kugawana nusu mkate, TL hataki maridhiano, anataka confrontations!, Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?
Hivyo kwenye hili la hii IGA, ni kweli IGA inamatatizo ya kisheria kama walivyo ainisha wanasheria na watu mbalimbali, nikiwemo mimi,
Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
IGA ni kama barua tuu ya posa, mahari ni HGA, kama mahari ni kumnunua binti, then bandari imeuzwa, lakini kama mahari ni consideration ya kumpata mke, hakuna hata milimita moja ya Bandari yetu iliyouzwa!. Tuyazungumze matatizo ya IGA bila upotoshaji na badala yake tufanye uendeshaji umma ili mwisho wa siku tupate HGA nzuri.
P