Tumalize ubishi wa miamba hii ya muziki nchini kati ya Chidumule, Bitchuka na hayati TX Moshi, nani alikuwa mtunzi na muimbaji mzuri?

Tumalize ubishi wa miamba hii ya muziki nchini kati ya Chidumule, Bitchuka na hayati TX Moshi, nani alikuwa mtunzi na muimbaji mzuri?

Swali langu ni hilo wakuu, japo kwa upande wangu nilimkubali na nitaendelea kumkubali sana mzee Hassan Rehani Bitchuka.

Wewe je unakubaliana na huyo huyo wa kwangu?

Au Cosmos Chidumule?

Au hayati Tx Moshi?
Tx Moshi usimfananishe na hivyo viroboti.
 
Swali langu ni hilo wakuu, japo kwa upande wangu nilimkubali na nitaendelea kumkubali sana mzee Hassan Rehani Bitchuka.

Wewe je unakubaliana na huyo huyo wa kwangu?

Au Cosmos Chidumule?

Au hayati Tx Moshi?
TX Moshi ni moto wa kuotea Mbali
 
Swali langu ni hilo wakuu, japo kwa upande wangu nilimkubali na nitaendelea kumkubali sana mzee Hassan Rehani Bitchuka.

Wewe je unakubaliana na huyo huyo wa kwangu?

Au Cosmos Chidumule?

Au hayati Tx Moshi?
Orodha hii ni fake, bila Hemed Chiriku Maneti, Max Bushoke!
 
HEmedi maneti huyo baba mkwe
Yeah, Hemed "Chiriku" Maneti na wimbo wake wa Maria Mary alikuwa baba lao!!
Nikisafiri kwenda Tanga, Arusha na Moshi mawazo yote kwako!
KWA KWELI SASA NIMENASA SINA UJANJA AAAAAH, SINA UJANJAAAAAA
KUPENDA SAWA NA AJALI HAINA KINGAAAA
NILIVYOMUHUSUDU MTOTO MARY, SIJAPATA KUPENDA TOKA NIZALIWEEEE NA WALA SITAPENDA MPAKA NIFE MPAKA NIFEEE MAMA MARY EEEEEH!
 
Bichuka ni kitu kingine ndgu,japo Moshi ndo alimalizia mwishooni
Nyie wote kumbe wa juzi juzi hapa! Kama hukuwahi kumsikia Hemed Chiriku Maneti huwezi kuelewa! Huyo ndiye alikuwa funga kazi ndiyo wakaja hao akina Mzee Kijicho (jina eti limenitoka), Tx Moshi William, Rehani Bitchuka, Seleman Kalala Mbwembwe, somebody Dede alikuwa Mlimani Park Orchestra, wale vijana wa Tancut Almas enzi zile! Mziki wa jazz ulikuwa wa maana sana siyo haya mauchafu ya sasa hivi!
 
Maneti kiboko yake marijani,narijaninayekiboko yake ni mbaraka mwinshehe,mbaraka naye kiboko yake salum abdalkah,unavyozidi kurudisha miaka nyuma ndio ubakutana na manguli zaidi
 
Moshi nadhani ni mtunzi mzuri.
Linapokuja suala la sauti nzuri na melodi ya maana Hakuna kama Bichuka Tanzania hii, hakika hakuna. Hebu kasikilize 1. Mfaume wanilizq, Talaka ya hasira, Talaka rejea, msikilize Bichuka humo.
Kuna kipande anaimba" madhara yake no makubwaa..... Madhara yake ni makubwa..... Wengine wananiita shangaziii....wengine wananiita mimi wifiiii.....
2. Baada ya Bichuka nadhani Eddie sheggi ndiye vocalist na melodist mzuri.
 
Hata kwenye utunzi, bado Moshi atakabiliwa na ushindani wa watunzi nguli kama Shabani Dede, Juma Mrisho "Ngulimba wa Ngulimba", Msafiri Haroub, mtaalam Benovila Antony, Zahir Zoro na wengine wengi.
Ramadhani Masanja "Banza Stone nadhani ndiyo mtunzi wa mwisho kwenye mziki wa dansi Tanzania. Baada ya wakongwe wengi kustaafu au kusinzia, na kifo Cha Banza hajaibuka mtunzi mwingine Tena wa maana
 
Tx Moshi alikuwa na Golden sound. Yule jamaa nampa maua yake ,he is best in my book.
 
Ramadhan MASANJA banza stone mwalimu wa walimu. Mwamba alienda na ubora wake utunzi na uimbaji alikuwa full package. Kasikilizeni ELIMU YA MJINGA NI MAJUNGU, AUNGURUMAPO SIMBA, KUMEKUCHA, MTU PESA.
 
Back
Top Bottom