Tumalize ubishi wa miamba hii ya muziki nchini kati ya Chidumule, Bitchuka na hayati TX Moshi, nani alikuwa mtunzi na muimbaji mzuri?

Tumalize ubishi wa miamba hii ya muziki nchini kati ya Chidumule, Bitchuka na hayati TX Moshi, nani alikuwa mtunzi na muimbaji mzuri?

Swali langu ni hilo wakuu, japo kwa upande wangu nilimkubali na nitaendelea kumkubali sana mzee Hassan Rehani Bitchuka.

Wewe je unakubaliana na huyo huyo wa kwangu?

Au Cosmos Chidumule?

Au hayati Tx Moshi?
Ila cha kushangaza hawa kuonekana kutembea na ccm wala kufanya ujinga wa wasanii waleo
 
Swali langu ni hilo wakuu, japo kwa upande wangu nilimkubali na nitaendelea kumkubali sana mzee Hassan Rehani Bitchuka.

Wewe je unakubaliana na huyo huyo wa kwangu?

Au Cosmos Chidumule?

Au hayati Tx Moshi?
1. Chidumule
2. Rehan bitchuka
3. Tx
 
Kwa upande wangu, Shaban Ally Mhoja Kishiwa (TX Moshi William) ndio mtunzi bora wa mwisho mwisho wa muziki wa dansi.

Baada ya kifo chake, Msondo ngoma ikajifia kimyakimya!!

Anyway, jamaa alishawahi kuua huko Tanga na kukimbilia Dar
Moshi aliua?
 
Ndiyo! Muhidin Gurumo Mwalimu!
Hivi mnajua ni kwa nini Bitchuka aliitwa ''Stereo''? Sauti yake kwenye nyimbo yoyote ilikuwa ni unique. Alikuwa ananogesha nyimbo sana. Anyways, kushindanisha wanamuziki kwa sauti mara nyingi ni very challenging kwani kila mwimbaji an vionjo vyake. Ni kama vyakula. TX Moshi alikuwa ana ladha yake tofauti na Bitchuka au Gurumo. Ila mimi Bitchuka ndiyo nampenda zaidi.
 
Back
Top Bottom