MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,775
- 71,893
Huu ni mwendelezo wa ule uzi niliouandika mwaka 2025 kuhusu tume ya Jaji Chande ambayo ilitumika kudogosha mauaji ya maelfu ya watanganyika. Kwa malengo ya kumbukumbu unaweza kufanya rejea hapa: Tume ya Uchunguzi yenye lengo la kudogosha mauaji ya watanganyika
========================================================================
Sasa CCM + TISS + TPDF + PT + MTANDAO mna uwanja mdogo sana tofauti ambavyo mnaweza kufikiria. Kipindi hiki, uwezo wenu wa ushawishi na nguvu unaishia Namanga kwa upande wa Kaskazini, unaishia Zanzibar kwa upande wa Mashariki, unaishia Kibondo kwa upande wa Magharibi, na unaishia Kyela kwa upande wa Kusini.
Mwarabu, Mchina na Mrusi, hawawezi kuwasiadia kukinga kifua dhidi ya watawala wenu wa kiasili (Mabeberu) ambao wametawala hii nchi kwa miaka zaidi ya 100 na wamekuwa wakiwalisha, kuwanywesha na kuwavisha kipindi chote cha uhuru wenu. Najua hili litawakera, lakini ukweli ndiyo huo. Hata baba yenu wa taifa alisomeshwa na mabeberu, na hata maraisi waliofuata baada yake baadhi yao ni rasilimali (Assets) za mabeberu.
Hivyo basi, kama masimulizi ya kale ya Kigiriki ya Homer yanavyosema kwamba, manowari ilikuwa inapita kwenye mfereji mwembamba (The Strait of Messina), na upande wa kushoto na kulia kulikuwa na majini ya baharini makubwa (Sea Monsters) yaoitwayo Scylla and Charybdis. Nahodha anavyopita kwenye huo mfereji alitakiwa awe na uamuzi mmoja tu, aidha apite kwa Scylla au apite kwa Charybdis, mambo ambayo yote mawili yalikuwa ni ya hatari.
Maadam President ameunda TUME YA UCHUNGUZI. Lengo lake anasema ni kuchunguza chanzo cha vurugu za kisiasa kwenye uchaguzi mkuu 2025. Ila wote tunafahamu kwamba chanzo kikuu ni KUOGOPA MKONO MREFU WA MABEBERU. Tume ya kwanza iliboronga vibaya kwasababu haikutoa njia ya jinsi ya kutoka kwenye korongo ambalo CCM mmeingiza nchi. Wengi tulitegemea TUME YA CHANDE ije na uchunguzi wake na itoe njia mbadala wa jinsi ya kujikwambua hapa tulipo ikiwemo TRANSITIONAL JUSTICE. Ila hola, mkadogosha muaji ya maelfu ya watanganyika mkitegemea yataisha tu.
Werevu walitegemea kwamba kama Raisi angekuwa na uwezo wa kung'amua mambo kwa kina, basi angechagua Scylla ambako siyo kubaya, kwamba awatoea kafara baadhi ya watu wakubwa ili dhoruba itulie. Watu wasulubiwe humu-humu ndani na mambo yaishe. Hata kama watanganyika watalalamika, lakini walau Yona atakuwa keshatoshwa baharini. Ila kiburi kimekuponza. Mabeberu huko duniani wamefahamu sehemu mbaya ya wakushika, na bahati mbaya watanzania wengi wanatoa ushirikiano kwa siri kwenye Mahakama ya uhalifu (ICC-The Hague, Bunge la Ulaya na Bunge la Marekani).
=======================================================================
IKO HIVI:
Kama nilivyosema kwenye uzi ulipita, ni kwamba ICC inafanya kazi kwa The Complementarity Principle. Itaingia kuishambulia serikali endapo tu, haitakuwa na uwezo wa kuendesha kesi za jinai, aidha kwa lengo la kuwalinda wahalifu au kutokuwa na uwezo wa kiutalaamu kuendesha kesi hizo (Unwilling or Unable).
Mwaka 2025, September, ICC ilitoa hukumu ya kipekee dhidi ya raia wa Central African Republic aitwaye Beina ambayo ilianza mwaka 2018. Huyu Beina alishitakiwa kwa kosa la kuua maelfu ya Waislamu nchini huko kwenye zile kampeni za mgambo wa Kikristo waitwao Anti-Balaka.
Beina aliachiwa na Mahakama ya ICC mwaka jana (2025), baada ya serikali ya Central African Republic (CAR) kuweka pingamizi kwamba Mahamaka ya ICC haina uwezo wa kuendeleza kesi yao dhidi ya Beina kwasababu tayari alishashitakiwa kwenye mahakama maalumu ya jinai nchini humo (Special Criminal Court).
Hivyo kigezo, siyo kuwa na tume peke yake, bali "Proof of Genuine Activity Against Perpetrators of Crime". Hivyo hata ukianzisha TUME YA UCHUNGUZI bila kuchukua hatua za ziada utakuwa unapiga mbizi kwenye lami.
Majuzi hapa Mzee wetu Prof. Issa G Shivji alipendekeza kitu kizuri kabisa ambacho nimekuwa nikikisema humu ndani kwa muda mrefu. Anzisha mahakama maalumu ya kushughulikia wahalifu wa 2025 (A Special Criminal Tribunal) ambayo itafanya kazi ya kushughulikia jinai za kimataifa (International Crimes) na siyo kuweka geresha kutumia mahakama za ndani na sheria za ndani kutoa adhabu.
=====================================================================
MKIENDELEA KUSHUPAZA SHINGO, maji yatazidi unga na hamtaweza kujilinda, Hivyo:
Mosi, nakushauri wewe kuwa MAMA MCHAWI, kubali kutoa kafara na kula nyama za watoto wako mwenyewe: Kamata kina Nkunda, Mombo, Kaji, Sirro, Muliro, Makonda, Bashungwa, Tax, na wahuni wako wengine ambao uliwatuma. Mbona Mzee Nyerere aliwahi kuwageuka wahuni wake aliokuwa anawatuma kukandamiza watanzania, kina Mzena, Bwimbo, Siyovelwa na Kisumo na kuwachinjia baharini kisa na nchi ikatulia.
Pili, au endelea kuwakumbatia kwa kutengeneza TUME YA UCHUNGUZI ambayo itaonesha wapinzani wako ndani ya CCM + TPDF + TISS kwamba wakishirikiana na mabeberu waliratibu vurugu za October 2025. Hili unaweza ukafanikiwa, lakini meli yako itazama kwasababu hakutakuwa na "Genuine Activity", na mtasulubishwa sana na hawa mabeberu kama ambavyo kwasasa mnaendelea kufanya mijadala isiyoisha na ICC.
It's Either Scylla or Charbdis a.k.a Being Caught in a rock and hard place
===============================================================
Kiufupi sisi ambao tunafahamu nini kinaendelea tunajua nchi iko pabaya mno.
Leo hii mimi hata unipe nafasi ya Uraisi siwezi kukubali kwasababu nafahamu fika kwamba kuna gharika kubwa ya Nuhu inakuja Tanzania. Hivyo kukaa nje ya mfumo ni kujitengenezea SAFINA SAFI KABISAAAA, ili yakianza tunaelea juu tu.

Sometimes when I think of what's coming, I envy the dead and feel sorry for the unborn...
ENIWEI, such is life......
SIJUI KAMA MTANIELEWA.....