Tume ya Haki Jinai kuanza kuzichunguza TAKUKURU, DCEA, Polisi, Magereza na Mahakama kesho

Hata hivyo Rais ameufanyia kazi Ushauri wa Tito Magoti
Wadau walishauri kuwa ingelichaguliwa tume yenye mchanganyiko ulio sawa, pamoja na hao waliochaguliwa sasa, wangelikuwemo pia na watu kama Mbowe ama Wakili Madeleka na wafungwa waliofungwa hadi kumaliza vifungo kwa kesi za kubambikiziwa.
 
Wa
Wachunguze na TRA
 
Utafute Uzi wa Tito magoti hapa upo.
Mkuu nimefuatilia na nimeusoma, ni madini matupu jamaa aliyatema.

Nikiri kuwa sikuwahi kuuona na kuusoma kabla.

Maudhui ya hiyo barua ya wazi yenye title " Barua ya wazi kwa Rais kuhusu haki jinai" imeeleza kwa kirefu sana na imegusa kila sehemu yenye "uozo"!

Nikiangalia na hotuba ya jana ambayo Rais aliitoa kwa hao wajumbe wa tume ya haki jinai, nina hakika ya 90% kuwa Rais aliisoma hiyo barua ya wazi iliyotumwa kwake na kuamua kuifanyia kazi.
 
Swali langu Ni moja tu.
Hiyo tume imeundwa na wazungu toka Denmark au Ni Hawa Hawa kina Mbonde ?
Naomba waanze na yule MTU wa takukuru aliyechukua rushwa ya dola 2500 sawa na madafu miloni sita halafu akapigwa faini ya milioni moja.
Hata kuku akiliangalia hili ataelewa tu kwamba Kuna ujinga ulifanyika.
 
Nashukuru sana. Nimeamini we ni Raia mwema sana na unajielewa. Hongera.
 
Inauma sana
 
Wadau walishauri kuwa ingelichaguliwa tume yenye mchanganyiko ulio sawa, pamoja na hao waliochaguliwa sasa, wangelikuwemo pia na watu kama Mbowe ama Wakili Madeleka na wafungwa waliofungwa hadi kumaliza vifungo kwa kesi za kubambikiziwa
Absolutely
 
tunachokiomba hii tume itende haki, waache tabia ya kulindana, penye uozo wauseme wazi kwa manufaa ya wananchi.

wafanye uchunhuzi wao kwa uhuru na kwa kujiamini, waache tabia ya kulindana
 
Hoja fikirishi🤔 Dhamira njema inashinda uovu ?
 
tunachokiomba hii tume itende haki, waache tabia ya kulindana, penye uozo wauseme wazi kwa manufaa ya wananchi.

wafanye uchunhuzi wao kwa uhuru na kwa kujiamini, waache tabia ya kulindana
Mimi ninavyoona, wakilindana kwa mambo ambayo yapo bayana nchi nzima watu wanayaelewa, kuanzi Rais mwenyewe aliyewateua mpaka kwa raia wa chini kabisa, basi ujue hakuna tena itakayokuja kuunda iaminike!

Kuanzia kwa mjumbe mmoja mmoja katika timu hiyo, watakuwa wamejipaka matope ya grisi yasiyosafishika.

Pia matokeo yaripoti ya tume hii ndiyo itaonesha kama kuna haja tena ya kuendelea kuunda tume zingine zinazopoteza tu rasilimali na zisizokuwa na manufaa kwa Taifa.

Ile rai ya Rais ya kurekebisha sheria mbovu mbovu kabla ya katiba mpya itakosa maana iwapo wajumbe hawa watachezea nafasi hii adhimu waliyopewa na mtu aliyelenga kuwaheshimisha katika jamii, kama alivyoheshimishwa Waryoba na tume yake.

Nasi raia tutampima Rais kwa kumwangalia usoni ni jinsi gani atakavyoipokea ripoti hiyo na namna atakavyoridhika ama kutoridhika nayo pamoja na namna atakavyoifanyia kazi.

Maana tume kama hizi zilishaundwa sana huko nyuma na tawala zilizopita, lakini hakuna historia inayoonesha kuwa ripoti zile kufanyiwa kazi na kuleta mabadiliko ya maana, hakuna.

Dhamira ya rais ni njema na anakubali kufanyia kazi mawazo ya watu, lakini je hawa wanaoteuliwa watafanya kwa uadilifu na hawatamuangusha?

Waswahili wanasema: "usiku wa deni haukawii kucha", mwezi May ni kesho tu tusubiri tuone!
 
 
Kuna Tume ngapia zilizoshawahi kutungwa na hakuna kitu. Siku moja atakuja Rais , ataunda Tume kuchunguza Tume zilizowahi kupita. Ndio siasa ilivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…