Tume ya Haki Jinai kuanza kuzichunguza TAKUKURU, DCEA, Polisi, Magereza na Mahakama kesho

Hata hivyo Rais ameufanyia kazi Ushauri wa Tito Magoti
Wadau walishauri kuwa ingelichaguliwa tume yenye mchanganyiko ulio sawa, pamoja na hao waliochaguliwa sasa, wangelikuwemo pia na watu kama Mbowe ama Wakili Madeleka na wafungwa waliofungwa hadi kumaliza vifungo kwa kesi za kubambikiziwa.
 
Wa
Akizungumza leo Jumanne Januari 31, 2023 Ikulu Chamwino, Dodoma wakati akizindua tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai nchini, Rais Samia ameitaka tume hiyo kuichunguza ofisi hiyo juu ya utendaji kazi na uendeshaji ili kubaini kasoro zilizopo na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuiboresha iweze kutoa haki kwa wananchi.

Amesema mbali na ofisi hiyo ya mashtaka tume hiyo itakayoanza kazi Jumatano Februari 1, hadi Mei 30, 2023 itazifanyia tathmini taasisi za utoaji haki jinai nchini ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na kuibua manung’uniko kwa wananchi, ikiwamo Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Jeshi la Polisi, Magereza na Mahakama.

“Kutokana na ukubwa wa kazi tunawapa miezi minne kuanzia kesho hadi Mei 30 nendeni mkaangalie Ofisi ya Mashtaka kwenyewe kukoje na kuna kasoro zipi.

“Zamani ofisi hii kulikuwa na ngoma nzito inachezwa mpaka kukusanya fedha za plea bargaining nyingine zimeonekana na nyingine hazijaonekana ukifuatilia utaambiwa mara kuna akaunti China.

“Tutazame kuna nini haswa kilichoharibu hii taasisi, pia tuiangalie Takukuru kwa sababu kubadilisha tu mkuu wa taasisi haisaidii watamdanganya tu wafanye wanavyotaka.

“Jeshi la Magereza na kwenyewe tukalitazame, magereza zetu zikoje na zinatakiwa ziweje, mwendelezo wake na kama linafanya kazi ya msingi? Mamlaka ya Kuzuia Dawa za Kulevya nako kuna changamoto nyingi za kutegea watu dawa,” amesema Rais Samia.

Naye, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amempongeza Rais kwa kuanzisha tume hiyo ili Watanzania waweze kupata haki kwani kumekuwa na manung’uniko mengi ya wananchi juu ya mfumo wa utoaji haki jinai nchini.

MWANANCHI
Wachunguze na TRA
 
Utafute Uzi wa Tito magoti hapa upo.
Mkuu nimefuatilia na nimeusoma, ni madini matupu jamaa aliyatema.

Nikiri kuwa sikuwahi kuuona na kuusoma kabla.

Maudhui ya hiyo barua ya wazi yenye title " Barua ya wazi kwa Rais kuhusu haki jinai" imeeleza kwa kirefu sana na imegusa kila sehemu yenye "uozo"!

Nikiangalia na hotuba ya jana ambayo Rais aliitoa kwa hao wajumbe wa tume ya haki jinai, nina hakika ya 90% kuwa Rais aliisoma hiyo barua ya wazi iliyotumwa kwake na kuamua kuifanyia kazi.
 
Swali langu Ni moja tu.
Hiyo tume imeundwa na wazungu toka Denmark au Ni Hawa Hawa kina Mbonde ?
Naomba waanze na yule MTU wa takukuru aliyechukua rushwa ya dola 2500 sawa na madafu miloni sita halafu akapigwa faini ya milioni moja.
Hata kuku akiliangalia hili ataelewa tu kwamba Kuna ujinga ulifanyika.
 
Mkuu nimefuatilia na nimeusoma, ni madini matupu jamaa aliyatema.

Nikiri kuwa sikuwahi kuuona na kuusoma kabla.

Maudhui ya hiyo barua ya wazi yenye title " Barua ya wazi kwa Rais kuhusu haki jinai" imeeleza kwa kirefu sana na imegusa kila sehemu yenye "uozo"!

Nikiangalia na hotuba ya jana ambayo Rais aliitoa kwa hao wajumbe wa tume ya haki jinai, nina hakika ya 90% kuwa Rais aliisoma hiyo barua ya wazi iliyotumwa kwake na kuamua kuifanyia kazi.
Nashukuru sana. Nimeamini we ni Raia mwema sana na unajielewa. Hongera.
 
Akizungumza leo Jumanne Januari 31, 2023 Ikulu Chamwino, Dodoma wakati akizindua tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai nchini, Rais Samia ameitaka tume hiyo kuichunguza ofisi hiyo juu ya utendaji kazi na uendeshaji ili kubaini kasoro zilizopo na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuiboresha iweze kutoa haki kwa wananchi.

Amesema mbali na ofisi hiyo ya mashtaka tume hiyo itakayoanza kazi Jumatano Februari 1, hadi Mei 30, 2023 itazifanyia tathmini taasisi za utoaji haki jinai nchini ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na kuibua manung’uniko kwa wananchi, ikiwamo Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Jeshi la Polisi, Magereza na Mahakama.

“Kutokana na ukubwa wa kazi tunawapa miezi minne kuanzia kesho hadi Mei 30 nendeni mkaangalie Ofisi ya Mashtaka kwenyewe kukoje na kuna kasoro zipi.

“Zamani ofisi hii kulikuwa na ngoma nzito inachezwa mpaka kukusanya fedha za plea bargaining nyingine zimeonekana na nyingine hazijaonekana ukifuatilia utaambiwa mara kuna akaunti China.

“Tutazame kuna nini haswa kilichoharibu hii taasisi, pia tuiangalie Takukuru kwa sababu kubadilisha tu mkuu wa taasisi haisaidii watamdanganya tu wafanye wanavyotaka.

“Jeshi la Magereza na kwenyewe tukalitazame, magereza zetu zikoje na zinatakiwa ziweje, mwendelezo wake na kama linafanya kazi ya msingi? Mamlaka ya Kuzuia Dawa za Kulevya nako kuna changamoto nyingi za kutegea watu dawa,” amesema Rais Samia.

Naye, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amempongeza Rais kwa kuanzisha tume hiyo ili Watanzania waweze kupata haki kwani kumekuwa na manung’uniko mengi ya wananchi juu ya mfumo wa utoaji haki jinai nchini.

MWANANCHI
Inauma sana
 
Wadau walishauri kuwa ingelichaguliwa tume yenye mchanganyiko ulio sawa, pamoja na hao waliochaguliwa sasa, wangelikuwemo pia na watu kama Mbowe ama Wakili Madeleka na wafungwa waliofungwa hadi kumaliza vifungo kwa kesi za kubambikiziwa
Absolutely
 
tunachokiomba hii tume itende haki, waache tabia ya kulindana, penye uozo wauseme wazi kwa manufaa ya wananchi.

wafanye uchunhuzi wao kwa uhuru na kwa kujiamini, waache tabia ya kulindana
 
Mapolisi, Jaji mkuu, Katibu mkuu, Mkurugenzi mkuu wa Takukuru na nani sijui shasahau, lakini wote hao walikuwa ni viongozi waandamizi wa taasisi hizo, kwa sasa ni wastaafu.

Utaratibu huu tayari ulikwishakukosolewa mapema kwamba, hao wote hawawezi kutenda ya maana kwa sababu mfumo huu wa hovyo wa haki jinai ndiyo walioukuta na ukawanufaisha.

Na hakuna hata mmoja wao katika historia ya maisha yake ambaye alikwishapata misukosuko ya kisheria na kutiwa ndani na akaonja joto ya jiwe kwa uharamia wa haki jinai.

Hivyo sasa, haidhaniwi kuwa tume hiyo wataweza kuleta mapendekezo ya maana na yenye tija.

Wadau walishauri kuwa ingelichaguliwa tume yenye mchanganyiko ulio sawa, pamoja na hao waliochaguliwa sasa, wangelikuwemo pia na watu kama Mbowe ama Wakili Madeleka na wafungwa waliofungwa hadi kumaliza vifungo kwa kesi za kubambikiziwa.

Hapo wangeweza kufukua vizuri makaburi bila kuacha mabaki ya mifupa.

Sasa ngoja tusubiri tuone tume hiyo kama itakidhi matakwa ya aliye wateua pamoja na wananchi kwa ujumla.

Ninaona dhamira njema ya kutoka moyoni ya Rais wetu Samia, lakini sina imani sana na viongozi wengi waliobebwa na mfumo huu mbovu wa ukandamizaji na uonevu wa haki jinai kwa watu.
Hoja fikirishi🤔 Dhamira njema inashinda uovu ?
 
tunachokiomba hii tume itende haki, waache tabia ya kulindana, penye uozo wauseme wazi kwa manufaa ya wananchi.

wafanye uchunhuzi wao kwa uhuru na kwa kujiamini, waache tabia ya kulindana
Mimi ninavyoona, wakilindana kwa mambo ambayo yapo bayana nchi nzima watu wanayaelewa, kuanzi Rais mwenyewe aliyewateua mpaka kwa raia wa chini kabisa, basi ujue hakuna tena itakayokuja kuunda iaminike!

Kuanzia kwa mjumbe mmoja mmoja katika timu hiyo, watakuwa wamejipaka matope ya grisi yasiyosafishika.

Pia matokeo yaripoti ya tume hii ndiyo itaonesha kama kuna haja tena ya kuendelea kuunda tume zingine zinazopoteza tu rasilimali na zisizokuwa na manufaa kwa Taifa.

Ile rai ya Rais ya kurekebisha sheria mbovu mbovu kabla ya katiba mpya itakosa maana iwapo wajumbe hawa watachezea nafasi hii adhimu waliyopewa na mtu aliyelenga kuwaheshimisha katika jamii, kama alivyoheshimishwa Waryoba na tume yake.

Nasi raia tutampima Rais kwa kumwangalia usoni ni jinsi gani atakavyoipokea ripoti hiyo na namna atakavyoridhika ama kutoridhika nayo pamoja na namna atakavyoifanyia kazi.

Maana tume kama hizi zilishaundwa sana huko nyuma na tawala zilizopita, lakini hakuna historia inayoonesha kuwa ripoti zile kufanyiwa kazi na kuleta mabadiliko ya maana, hakuna.

Dhamira ya rais ni njema na anakubali kufanyia kazi mawazo ya watu, lakini je hawa wanaoteuliwa watafanya kwa uadilifu na hawatamuangusha?

Waswahili wanasema: "usiku wa deni haukawii kucha", mwezi May ni kesho tu tusubiri tuone!
 
Kuna Tume ngapia zilizoshawahi kutungwa na hakuna kitu. Siku moja atakuja Rais , ataunda Tume kuchunguza Tume zilizowahi kupita. Ndio siasa ilivyo.
 
Back
Top Bottom