Tume ya Haki za Binadamu yatoa ripoti ya kifo cha Nusura Hassan Abdallah, chasema hakuna uhusiano na ajali ya Waziri Dkt. Festo Dugange

Sijawahi kuona umuhimu wa hizi Tume kwa kweli. Hii Tume ya Haki za Binafamu ni kupoteza raslimali za nchi kwa gharama zinazotumika kuwaweka kwenye ofisi.

Naibu Waziri Ndejembi hatuelewi ana manufaa gani na kumkingia kifua huyu Naibu mwenzie Dugange. Yaani element tu kuwa Watanzania siyo wapumbavu
 
Tulitegemea majibu km haya, hakuna kipyaa hapo.
 
Naomba tu kuuliza. Kwani hao waliofanya huo uchunguzi ni wadamu au malaika.
 
Ukweli utafahamika tu.. mna haaahaa..
🤔🤔🤭🤭🤔🤭🤭🤔
Damu ya mtu haiendi bure.
 
Jamaa anasafishwa kwa nguvu kubwa sana
 
Nimeisoma ripoti yote hii ya Tume na kifupi mimi nimependezewa na ushauri wa Tume kwa Jeshi la Polisi kwamba zifungwe kamera za kisasa na mifumo ya technologia ya kisasa barabarani ambapo itasaidia kudetect makosa na vyanzo mbalimbali vya ajali barabarani likiwemo hii la ajali ya Dr Festo Dugunge.Kama kamera zingekuwepo zimefungwa barabarani inamaana ushaidi wa picha na video wa ajali ile ungeonekana na ingejidhihirisha wazi kama huyo binti wa chuo alikuwa kwenye ajali ya gari ya Mheshimiwa au la na kuondoa sintofahamu yote na "uongo" ambao ulienezwa na kuenea kwa haraka kama moto katika jamii yote ambayo imekuwa ikipenda sana kusikia feki stories na uongo mwingi.Ni muda muafaka kwa jeshi letu la Polisi kuchukua hatua haraka sasa kwa kufunga hiyo mitambo.Wenzetu nchi nyingi za kiAfrika na duniani huko kama Rwanda,Kenya,Morocco, Dubai,Senegal Qatar Cameroon nk wamefunga hizi kamera ambazo zimekuwa msaada mkubwa wa kupunguza ajali za kizembe za barabarani lakini pia zimekuwa zikikamata makosa mengine ya kihalifu na kutumika kama ushaidi mahakamani katika kesi mbalimbali lakini pia kutokana na makosa ambayo yamekuwa yakifanywa na madereva wazembe "mashine" hizi zimekuwa zikiyanasa kwa wingi automatically na kuwa ni chanzo kikubwa cha mapato katika nchi hizi.Kuiga kizuri sio dhambi sisi kama Taifa tuige kwa wenzetu hawa.
 
Bonge la script
Tambala limechezwa
 
Hawakua na sababu ya kuandika maandishi mengi hivi, kwani yote hayo sisi tulishayajua hata kabla wao hawajawaza kuwa watatakiwa kuchunguza.

Ili kuokoa muda wangendika kichwa cha habari tu na ku share na vyombo vya habari
 
Aliyemuacha mkewe kwa kashfa hiyo ni Kaisari na siyo Mfalme Suleiman
 
Yule mwanamke aliyepata ajali na waziri yeye yukowapi maana waziri alipata majeraha kiasi cha kulazwa abiria wake yukowapi mtuambie alipo
 
Matapishi waliyapata wapu voz hakuna mtu ambaye huwa anatunza matapishi. Hii nchi bwana ila basi tu
 
Duu hiyo sumu ni ya kisasa na ya aina yake yaani imdhuru mtu mmoja tuu (mgeni) kati ya watatu waliokula au hao wenyeji kwao hiyo sumu ni chakula walichozoea nawaza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…