Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina upendeleo wa wazi kwa CCM na mgombea wake dhidi ya CHADEMA na Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina upendeleo wa wazi kwa CCM na mgombea wake dhidi ya CHADEMA na Tundu Lissu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Kwa mujibu wa katiba ya nchi na kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, Tume ya Taifa ya uchaguzi ndiyo yenye mamlaka na dhamana ya kuendesha na kusimamia chaguzi za wabunge na rais nchini. Katika kutekeleza majukumu hayo kuna sheria kanuni na miongozo ya kufuata ikiwemo kuwa fair kwa vyama na wagombea wote bila upendeleo

Hata hivyo tume hii imeonyesha upendeleo mkubwa na wa dhahiri kwa CCM na mgombea wake dhidi ya Chama kikuu cha upinzani nchini na mgombea wake.

Hapa chini ni namna Tume ilivyofumba macho uvunjaji wa wazi wa maadili ya uchaguzi kwa kuinufaisha CCM

1. Mgombea wa CCM Magufuli mara kadhaa akiwa kanda ya Ziwa amekuwa akitumia kilugha
Magufuli amekuwa akiongea kilugha kinyume cha utaratibu wa kisheria na maadili ya uchaguzi, lakini Tume haijamuandikia barua ya onyo kuhusu jambo hili, lakini yenyewe iko mbiombio kukekemea wapinzani

2. Vyombo vya habari vya serikali vimekuwa na upendeleo kwa CCM na mgombea wake dhidi ya Upinzani na tume haijavionya
Sheria ya uchaguzi inataka vyombo vyote vya habari vya umma vitoe air time sawa kwa kila mgombea kipindi cha uchaguzi lakini vyombo hivyo vimekuwa na upendeleo wa kutisha kwa Magufuli dhidi ya wagombea wa upinzani akiwemo mheshimiwa Lissu, lakini tume ya Taifa ya uchaguzi haijavionya vyombo hivi kuwa vinakiuka kanuni na maadilibya uchaguzi

3. Rais Magufuli amewahi kutoa kauli kuwa Haiwezekani awape mishahara wakurugenzi wanaosimamia chaguzi huko kwenye halmashauri halafu watangaze Mpinzani kushinda, NEC haikuwahi kukemea hiyo kauli

Tume ya Taifa ya uchaguzi haijawahi kukemea kauli hiyo, hijawahi kumuandikia rais Magufuli barua yoyote ya kupinga kauli hiyo. Hata ksma aliitoa zamani, lakini chaguzi nyingi za marudio zimepita, na sasa tupo kwenye uchaguzi huu, kauli haijafutwa na NEC haijawahi kutaka ifutwe, kwa hiyo agizo haramu la kutotenda haki kutoka kwa rais bado lipo na NEC haijakemea chochote!

4. Mgombea wa CCM ndugu Magufuli ametoa kauli za kutisha wananchi wasifanye maamuzi huru kwenye uchaguzi huu kwamba wasipochagua wagombea wa CCM atawanyima maendeleo na NEC iko kimya tu

Hili ni kosa kubwa sana, NEC ilipaswa kumuonya rais Magufuli kuwa kutishia kuwanyima wananchi maendeleo, kuwabagua kwa namna yoyote ni kinyume cha sheria za nchi, siyo lengo la uchaguzi, ni kauli inayotishia amani, na kuleta vurugu kama vile uasi katika nchi maana maeneo yatakayobaguliwa makusudi kunyimwa maendeleo yanaweza kuanzisha uasi wa kujitenga ili yajiletee maendeleo. NEC haimuonyi Magufuli

5. NEC badala ya kusimamia uchaguzi na kuwa fair, na yenyewe inajiingiza katika kuipigia kampeni CCM kwa kuponda ilani za uchaguzi za vyama vingine

Juzi hapa Mkurugenzi wa NEC bwana Mahera alisikika wazi akiponda ilani ya vyama vingine kama ya Chadena kuhusu vitu mbalimbali ikiwemo sera yakebya madini. Siyo kazi ya tume kupigia kampeni chama fulani. Kwenye hili hatujaona bwana Mahera akichukuliwa hatua zozote juu ya Ukada na mapenzi yake ya dhahiri kwa CCM

6. Waziri Mkuu anazunguuka nchi nzima kufanya kampeni kwa kutumia rasilimali za serikali
Ukiachilia rasilimali fedha, kuna rasilimali muda. Waziri mkuu anatuibia sisi Watanzania muda wetu wa kufanya mambo ya nchi kwa kufanya mambo ya kampeni kwa mgombea wa urais wa CCM. Maadili yanakataza mawaziri kutumia rasilimali za nchi kufanya kampeni, sheria inawakataza kutoa hata matamko ya kisera na ahadi mbalimbali nyakati hizi za uchaguzi, Sasa kipindi hiki cha uchsguzi ambapo tulitegemea waziri mkuu autumie muda tunaomlipa mshahara kututumikia asimame kuendesha mambo ya serikali kipindi hiki cha uchaguzi, yeye yuko kiguru na njia mikoani, anatumia rasilimali muda, walinzi anaokuwa nao watahitaji per diem, anatumia madereva wa serikali kwenda kumfanyia Magufuli kampeni na kote huku pesa za umma zinatumika. NEC iko kimya, haijamuonya

6. CCM inatumia rasilimali za serikali, na umma, na hata za misaada ya wahisani kufanya kampeni kujinufaisha kisiasa.

Jana Karagwe, gari lililotolewa na wahisani, Donnor funded project, lenye namba DFP 5445 lilikuwa likizuunguuka huko Karagwe kutangaza ujio wa Waziri mkuu kwa ajili ya kampeni za kumnadi Magufuli. Hiki ni kinyume kabisa za sheria za uchaguzi, lakini NEC, haiwaonyi CCM juu ya suala la namna hii la kuvunja maadili na kanuni za uchaguzi.

Katika Mazingira hayo, Sisi wananchi tutaamini vipi kuwa Tume hii hii yenye upendeleo itaweza kusimamia uchaguzi huru ulio fair?.

Tume ineshayumba mpaka hivi sasa binafsi nina imani ndogo sana na tume hii!
 
Ukweli mtupu, aibu kwa muhuni anayejiita mzalendo mwenye hofu ya mungu.

Ila mwaka huu CCM wamepata somo kubwa, upinzan haukufa, uliamua kukaa kimya tu, hivyo CCM wajifunze kuheshimu wenye mawazo tofauti,
Hii nchi ni ya watanzania wote.
 
Walitamani kumuomba Lissu kwa gharama yeyote kama walivyofanya kwa wabunge na madiwani ila imeshindikana mpaka jamaa aliongea jukwaani sio utani ule..hii aibu wanaipata kweli maana aliamini watu wamemuelewa na mandege yake sasa hawezi kuyaongelea tena kwa wananchi wanaotaabika wanataka kumuona mkombozi wao Lissu...
 
Mimi sio mwana siasa lakini lakini simpendi kabisa rais magufuli
Kweli kweli no mbaguzi Sana
Katili Sana
Kiburi Sana
Muuaji mkuu
Hana huruma
Chuki binafs
Mtu wa visasi
Hapendi ushuru
Dharau
Kebehi
Dhulma
Kujikweza
Majivuno
Mkabila
Ndini
Mkanda
Kwa kweli ni mtu ambae anasifa nyingi za unyama na za kidikteta
Sidhani kama anasifa moja ya kiutu
Lakini atashinda uchaguzi kwa kishindo cha kufanya watanzania ni kufanya subira miaka mi5 panapo majaliwa itaisha
 
EjBrymVXkAc7QnL.jpeg

Tazama mikono na limdomo
 
Kama umemuangalia juzi Mahera akizungumza na Waandishi wa Habari body language yake inaonyesha wazi kuwa tayari wameshaandaa matokeo na mshindi wanae anasubiri tu kumtangaza.

Sina hata chembe ya imani na Tume ile.
 
Niombe wahusika wote katika kila hatua ya usimamizi wa UCHAGUZI, jitahidini kadri ya upeo wenu kuto onyesha UPENDELEO wa namna yeyote ile kwa wagombea wa ngazi zote.

Kuonyesha UPENDELEO kwa upande fulani kunapelekea kuamsha HASIRA miongoni mwa jamii ya waathirika wa UPENDELEO huo.

Tanzania ya sasa imebadilika sana. Waoga wanazidi kupungua, na wajasiri wanaongezeka kidogo kidogo. Pia kuna mtu aliyeponyoka HATARI KUBWA ambaye kila siku anajiongezea wafuasi wa ujasiri wake.

Tendo lolote la kupendelea CHAMA fulani au mgombea fulani kutapelekea jamii mpya ya wajasiri kufanya maamuzi ya kijasiri ambayo hatuwezi KUTABIRI MATOKEO YAKE KWA sasa.

NEC mnayo nafasi sasa kutenda haki. Kutoonyesha UPENDELEO wa wazi. Mnayo nafasi ya kuwapa democracy watanzania.

Kila la kheri NEC.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Ukweli mtupu, aibu kwa muhuni anayejiita mzalendo mwenye hofu ya mungu.


Ila mwaka huu ccm wamepata somo kubwa, upinzan haukufa, uliamua kukaa kimya tu, hvyo ccm wajifunze kuheshimu wenye mawazo tofauti,
Hii nchi ni ya watanzania wote.

Tume imetia aibu sana kwa jinsi inavyoonyesha upendeleo wa dhahiri kwa CCM
 
Kama umemuangalia juzi Mahera akizungumza na Waandishi wa Habari body language yake inaonyesha wazi kuwa tayari wameshaandaa matokeo na mshindi wanae anasubiri tu kumtangaza.

Sina hata chembe ya imani na Tume ile.

Mahera ametukosea sana Watanzania kwa kuipigia CCM kampeni za wazi pale alipoponda sera za vyama vingine hata kama kwa mtizamo wake anaona ni mbaya
 
Back
Top Bottom