Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina upendeleo wa wazi kwa CCM na mgombea wake dhidi ya CHADEMA na Tundu Lissu

Wewe una picha halisi za Karatu?
Yaani kushinda nyinyi ni ndoto ya mchana. Leo nimehakikisha kabisa kuwa mnaedit picha leo nilikuwepo Karatu hakukuwa na watu kama mnavyoonyesha picha.
 
Mbona ulisema Leo Ndio umeamini?
Kua picha zina fanyiwa editing
Pole Sana
Ndiyo nimeona picha zinazotembea hapa JF siyo za kweli nilikuwepo Karatu hakukuwa na watu wengi hivyo kama inavyoonyeshwa kwenye picha hizo.
 
Labda na ile ya jiwe kupiga magoti ni ya uongo
 
Maisha yetu yanatudai uaminifu,kuaminika.
Yàani ikiwa unasimamia maslahi ya watu,ufanye hivyo kwa uaminifu na watu wenyewe wakuamini.
Ikiwa mtu mwenye hadhi yake na akili zake akawa anafanya kazi kwenye taasisi kubwa na yenye dhamana ya kusimamia uchaguzi mkuu wa nchi na inakosa kuaminika na wananchi,bila shaka hana budi kuacha hiyo kazi.
Watu wetu ambao tunawaheshimu na kuwaona wasomi,hii leo wanafanya kazi katika tume ya uchaguzi inayokosa kuaminika na wananchi walio wengi,hivyo na wao viongozi wa tume wanakosa kuaminika na kwa kweli SI WAAMINIFU.
Tunadhani huko vyuoni waliokwenda kusoma basi watakuwa walienda kusomea UJINGA.
Tunaona sasa ni muda muafaka wa kuacha kuiongozea jamii yetu na kurudi kwenye kazi zao za siasa waliozoea ili waweze kujijengea uaminifu kwa wananchi.
 
Hiyo siyo uongo ni heshima ya wananjombe kumbe hujui na mila za wananjombe?
Heshima
Kaanza lini kua good boy?
Mimi najua sifa zake
Muuaji
Kiburi
Haambiliki
Mtekaji
Asiekua na huruma
Katili
Mdini
Mkabila
Mkanda
Mlipa visasi
Anasifa zote za farao
Baada ya uchaguzi utamuona
Wana Njombe watalipa goti Hilo
 
Mifumo na taasisi zetu ziko weak Sana kutusaidia kuwa na maendeleo na maisha yenye Haki

Kuna wakati huwa nasema kwa mifumo hii ni Kama tumaamua kutawaliwa na wachache
 
Asante kwa kuyaweka haya pamoja. Tume hii ya Mahera ni mbaya kuliko ZEC ya Jecha. Jecha aliweka makucha yake ndani mpaka uchaguzi ulipofanyika. Huyu Mahera bila aibu kabisa anapigia CCM kampeni. Hawezi kabisa kumtangaza TL mshindi. Wananchi tujitayarishe kulinda ushindi wetu kwa jasho na damu.
Kwa mujibu wa katiba ya nchi na kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, Tume ya Taifa ya uchaguzi ndiyo yenye mamlaka na dhamana ya kuendesha na kusimamia chaguzi za wabunge na rais nchini. Katika kutekeleza majukumu hayo kuna sheria kanuni na miongozo ya kufuata ikiwemo kuwa fair kwa vyama na wagombea wote bila upendeleo

Hata hivyo tume hii imeonyesha upendeleo mkubwa na wa dhahiri kwa CCM na mgombea wake dhidi ya Chama kikuu cha upinzani nchini na mgombea wake.

Hapa chini ni namna Tume ilivyofumba macho uvunjaji wa wazi wa maadili ya uchaguzi kwa kuinufaisha CCM

1. Mgombea wa CCM Magufuli mara kadhaa akiwa kanda ya Ziwa amekuwa akitumia kilugha
Magufuli amekuwa akiongea kilugha kinyume cha utaratibu wa kisheria na maadili ya uchaguzi, lakini Tume haijamuandikia barua ya onyo kuhusu jambo hili, lakini yenyewe iko mbiombio kukekemea wapinzani

2. Vyombo vya habari vya serikali vimekuwa na upendeleo kwa CCM na mgombea wake dhidi ya Upinzani na tume haijavionya
Sheria ya uchaguzi inataka vyombo vyote vya habari vya umma vitoe air time sawa kwa kila mgombea kipindi cha uchaguzi lakini vyombo hivyo vimekuwa na upendeleo wa kutisha kwa Magufuli dhidi ya wagombea wa upinzani akiwemo mheshimiwa Lissu, lakini tume ya Taifa ya uchaguzi haijavionya vyombo hivi kuwa vinakiuka kanuni na maadilibya uchaguzi

3. Rais Magufuli amewahi kutoa kauli kuwa Haiwezekani awape mishahara wakurugenzi wanaosimamia chaguzi huko kwenye halmashauri halafu watangaze Mpinzani kushinda, NEC haikuwahi kukemea hiyo kauli

Tume ya Taifa ya uchaguzi haijawahi kukemea kauli hiyo, hijawahi kumuandikia rais Magufuli barua yoyote ya kupinga kauli hiyo. Hata ksma aliitoa zamani, lakini chaguzi nyingi za marudio zimepita, na sasa tupo kwenye uchaguzi huu, kauli haijafutwa na NEC haijawahi kutaka ifutwe, kwa hiyo agizo haramu la kutotenda haki kutoka kwa rais bado lipo na NEC haijakemea chochote!

4. Mgombea wa CCM ndugu Magufuli ametoa kauli za kutisha wananchi wasifanye maamuzi huru kwenye uchaguzi huu kwamba wasipochagua wagombea wa CCM atawanyima maendeleo na NEC iko kimya tu

Hili ni kosa kubwa sana, NEC ilipaswa kumuonya rais Magufuli kuwa kutishia kuwanyima wananchi maendeleo, kuwabagua kwa namna yoyote ni kinyume cha sheria za nchi, siyo lengo la uchaguzi, ni kauli inayotishia amani, na kuleta vurugu kama vile uasi katika nchi maana maeneo yatakayobaguliwa makusudi kunyimwa maendeleo yanaweza kuanzisha uasi wa kujitenga ili yajiletee maendeleo. NEC haimuonyi Magufuli

5. NEC badala ya kusimamia uchaguzi na kuwa fair, na yenyewe inajiingiza katika kuipigia kampeni CCM kwa kuponda ilani za uchaguzi za vyama vingine

Juzi hapa Mkurugenzi wa NEC bwana Mahera alisikika wazi akiponda ilani ya vyama vingine kama ya Chadena kuhusu vitu mbalimbali ikiwemo sera yakebya madini. Siyo kazi ya tume kupigia kampeni chama fulani. Kwenye hili hatujaona bwana Mahera akichukuliwa hatua zozote juu ya Ukada na mapenzi yake ya dhahiri kwa CCM

6. Waziri Mkuu anazunguuka nchi nzima kufanya kampeni kwa kutumia rasilimali za serikali
Ukiachilia rasilimali fedha, kuna rasilimali muda. Waziri mkuu anatuibia sisi Watanzania muda wetu wa kufanya mambo ya nchi kwa kufanya mambo ya kampeni kwa mgombea wa urais wa CCM. Maadili yanakataza mawaziri kutumia rasilimali za nchi kufanya kampeni, sheria inawakataza kutoa hata matamko ya kisera na ahadi mbalimbali nyakati hizi za uchaguzi, Sasa kipindi hiki cha uchsguzi ambapo tulitegemea waziri mkuu autumie muda tunaomlipa mshahara kututumikia asimame kuendesha mambo ya serikali kipindi hiki cha uchaguzi, yeye yuko kiguru na njia mikoani, anatumia rasilimali muda, walinzi anaokuwa nao watahitaji per diem, anatumia madereva wa serikali kwenda kumfanyia Magufuli kampeni na kote huku pesa za umma zinatumika. NEC iko kimya, haijamuonya

6. CCM inatumia rasilimali za serikali, na umma, na hata za misaada ya wahisani kufanya kampeni kujinufaisha kisiasa.

Jana Karagwe, gari lililotolewa na wahisani, Donnor funded project, lenye namba DFP 5445 lilikuwa likizuunguuka huko Karagwe kutangaza ujio wa Waziri mkuu kwa ajili ya kampeni za kumnadi Magufuli. Hiki ni kinyume kabisa za sheria za uchaguzi, lakini NEC, haiwaonyi CCM juu ya suala la namna hii la kuvunja maadili na kanuni za uchaguzi.

Katika Mazingira hayo, Sisi wananchi tutaamini vipi kuwa Tume hii hii yenye upendeleo itaweza kusimamia uchaguzi huru ulio fair?.

Tume ineshayumba mpaka hivi sasa binafsi nina imani ndogo sana na tume hii!
 
Mifumo na taasisi zetu ziko weak Sana kutusaidia kuwa na maendeleo na maisha yenye Haki

Kuna wakati huwa nasema kwa mifumo hii ni Kama tumaamua kutawaliwa na wachache

Tunahitaji overhaul ya mfumo mzima wa utawala nchini, huu mfumo tulionao ni mfumo wa enzi za chama kushika hatamu, haukidhi tena mahitaji ya wananchi!. Just imagine kada wa wazi wa CCM eti ndiye mkurugenzi wa NEC. Huu ni utani mbaya sana kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
 
Huna jipya. Tume, CCM na Serikali wameshatukanwa sana na mgombea wenu na nyie vibaraka wa mkoloni. Ila izi ngebe zenu mwisho 28 Oktoba 2020. Akili zitawakaa sawa tu.
 
Hii lialia yenu sio bure. Design mmeshaona kabisa kwamba hamtoboi, hamtoboiiiii in Bwegez voiz, yani hamtoboi, sasa njia na option pekee mliyobaki nayo ni kujenga chuki, kuchochea vurugu, ila juzi nimemcheck mgombea wenu kule Nyamongo mabomu ya machozi tu alipoteana na walinzi wake. Fanyeni kampeni kistaarabu fujo hamziwezi waoga wakubwa nyie.
 
Katiba mpya ni muhimu sana kikawaida mtu ukiwa na rasilimali nyingi unaweza kuzitumia hovyo hovyo kwahiyo lazima uchorewe mstari
 
Kwa mujibu wa katiba ya nchi na kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, Tume ya Taifa ya uchaguzi ndiyo yenye mamlaka na dhamana ya kuendesha na kusimamia chaguzi za wabunge na rais nchini. Katika kutekeleza majukumu hayo kuna sheria kanuni na miongozo ya kufuata ikiwemo kuwa fair kwa vyama na wagombea wote bila upendeleo

Hata hivyo tume hii imeonyesha upendeleo mkubwa na wa dhahiri kwa CCM na mgombea wake dhidi ya Chama kikuu cha upinzani nchini na mgombea wake.

Hapa chini ni namna Tume ilivyofumba macho uvunjaji wa wazi wa maadili ya uchaguzi kwa kuinufaisha CCM

1. Mgombea wa CCM Magufuli mara kadhaa akiwa kanda ya Ziwa amekuwa akitumia kilugha
Magufuli amekuwa akiongea kilugha kinyume cha utaratibu wa kisheria na maadili ya uchaguzi, lakini Tume haijamuandikia barua ya onyo kuhusu jambo hili, lakini yenyewe iko mbiombio kukekemea wapinzani

2. Vyombo vya habari vya serikali vimekuwa na upendeleo kwa CCM na mgombea wake dhidi ya Upinzani na tume haijavionya
Sheria ya uchaguzi inataka vyombo vyote vya habari vya umma vitoe air time sawa kwa kila mgombea kipindi cha uchaguzi lakini vyombo hivyo vimekuwa na upendeleo wa kutisha kwa Magufuli dhidi ya wagombea wa upinzani akiwemo mheshimiwa Lissu, lakini tume ya Taifa ya uchaguzi haijavionya vyombo hivi kuwa vinakiuka kanuni na maadilibya uchaguzi

3. Rais Magufuli amewahi kutoa kauli kuwa Haiwezekani awape mishahara wakurugenzi wanaosimamia chaguzi huko kwenye halmashauri halafu watangaze Mpinzani kushinda, NEC haikuwahi kukemea hiyo kauli

Tume ya Taifa ya uchaguzi haijawahi kukemea kauli hiyo, hijawahi kumuandikia rais Magufuli barua yoyote ya kupinga kauli hiyo. Hata ksma aliitoa zamani, lakini chaguzi nyingi za marudio zimepita, na sasa tupo kwenye uchaguzi huu, kauli haijafutwa na NEC haijawahi kutaka ifutwe, kwa hiyo agizo haramu la kutotenda haki kutoka kwa rais bado lipo na NEC haijakemea chochote!

4. Mgombea wa CCM ndugu Magufuli ametoa kauli za kutisha wananchi wasifanye maamuzi huru kwenye uchaguzi huu kwamba wasipochagua wagombea wa CCM atawanyima maendeleo na NEC iko kimya tu

Hili ni kosa kubwa sana, NEC ilipaswa kumuonya rais Magufuli kuwa kutishia kuwanyima wananchi maendeleo, kuwabagua kwa namna yoyote ni kinyume cha sheria za nchi, siyo lengo la uchaguzi, ni kauli inayotishia amani, na kuleta vurugu kama vile uasi katika nchi maana maeneo yatakayobaguliwa makusudi kunyimwa maendeleo yanaweza kuanzisha uasi wa kujitenga ili yajiletee maendeleo. NEC haimuonyi Magufuli

5. NEC badala ya kusimamia uchaguzi na kuwa fair, na yenyewe inajiingiza katika kuipigia kampeni CCM kwa kuponda ilani za uchaguzi za vyama vingine

Juzi hapa Mkurugenzi wa NEC bwana Mahera alisikika wazi akiponda ilani ya vyama vingine kama ya Chadena kuhusu vitu mbalimbali ikiwemo sera yakebya madini. Siyo kazi ya tume kupigia kampeni chama fulani. Kwenye hili hatujaona bwana Mahera akichukuliwa hatua zozote juu ya Ukada na mapenzi yake ya dhahiri kwa CCM

6. Waziri Mkuu anazunguuka nchi nzima kufanya kampeni kwa kutumia rasilimali za serikali
Ukiachilia rasilimali fedha, kuna rasilimali muda. Waziri mkuu anatuibia sisi Watanzania muda wetu wa kufanya mambo ya nchi kwa kufanya mambo ya kampeni kwa mgombea wa urais wa CCM. Maadili yanakataza mawaziri kutumia rasilimali za nchi kufanya kampeni, sheria inawakataza kutoa hata matamko ya kisera na ahadi mbalimbali nyakati hizi za uchaguzi, Sasa kipindi hiki cha uchsguzi ambapo tulitegemea waziri mkuu autumie muda tunaomlipa mshahara kututumikia asimame kuendesha mambo ya serikali kipindi hiki cha uchaguzi, yeye yuko kiguru na njia mikoani, anatumia rasilimali muda, walinzi anaokuwa nao watahitaji per diem, anatumia madereva wa serikali kwenda kumfanyia Magufuli kampeni na kote huku pesa za umma zinatumika. NEC iko kimya, haijamuonya

6. CCM inatumia rasilimali za serikali, na umma, na hata za misaada ya wahisani kufanya kampeni kujinufaisha kisiasa.

Jana Karagwe, gari lililotolewa na wahisani, Donnor funded project, lenye namba DFP 5445 lilikuwa likizuunguuka huko Karagwe kutangaza ujio wa Waziri mkuu kwa ajili ya kampeni za kumnadi Magufuli. Hiki ni kinyume kabisa za sheria za uchaguzi, lakini NEC, haiwaonyi CCM juu ya suala la namna hii la kuvunja maadili na kanuni za uchaguzi.

Katika Mazingira hayo, Sisi wananchi tutaamini vipi kuwa Tume hii hii yenye upendeleo itaweza kusimamia uchaguzi huru ulio fair?.

Tume ineshayumba mpaka hivi sasa binafsi nina imani ndogo sana na tume hii!
Mimi Naweza kusema kuwa wewe huzijui Sheria vyema, unasoma upande mmoja tu. Labda niseme Sheria inasomwa Kama ambavyo inasonga ugali, katu huwezi songs ugali kwa mkono mmoja.

Lakini hivi umesahau kuwa ni Mbowe na Lissu ndio waliobifukuza hivyo vyombo vya umma? Hivi unajua kua sio kila vipindi ni vya bure katika vituo vya habari vya umma. Kuna vingine wanalipwa hasa hizo live.

Unalia na Lissu tu hatndewi Haki, vipi Lipumba, Rungwe, Membe, na wagombea wengine 10 waliobaki je wanapewa huduma hiyo.

Tume inamkemeaje wakala wa kampeni wa Mgombea fulani. Majaliwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Chama chake kimemteua kuwa wakala wa Mgombea wao kimnadi. Anatimiza majukwaa ya wagombea Ubunge na ratiba zao hayupo kwenye ratiba ya tume. Hata Lissu Kama Mnyika anaweza kufanya hivyo anaweza Mbona Zitto Kabwe alikuwa anazunguka Mikoani kuwanadi wagombea wa Chama chake na hamsemi Time imkemee? Abdull Nondo wa ACT alikuwa anazunguka Mikoani kunadi wagombea Mbona hamkusema kuhusu hilo? Toeni boriti jichoni kwenu kabla ya kibanzi kwa mwenzio.
Kauli ya Magufuli na Wakurugenzi aliitoa lini na wapi? Je mnaweza ipeleka Kamati ya Maadili?. USIKURUPUKE.

Hivi kumbe kuna vyama Ilani zao ni matusi, kuhimiza vurugu na kutishiana na si kumleta maendeleo kwa wapigakura wao. Hivi ni cha gani ambacho kikishinda, Miundominu ya Barabara, afaya, Elimu, umeme, mawasiliano hakitafanya? Mimi Kama Mwananchi nataka Sana Chama kitakacho hakikisha huduma bora za kijamii, mkulima nayafikia masoko kwa kua na Barbara nzuri, watoto wanasema vizuri na huduma za afya zinakuja Bora zaidi ya Sasa. JIPANGE NDUGU.
 
Pombe kesho piga magoti
Kesho ataanza kuomba msamaha
Kwa muda mrefu watanzania tulikua tunasema
We can't breathe
Lakini Sasa jiwe ndo linasema
I can't breathe
 
Back
Top Bottom