Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina upendeleo wa wazi kwa CCM na mgombea wake dhidi ya CHADEMA na Tundu Lissu

Kwa mujibu wa katiba ya nchi na kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, Tume ya Taifa ya uchaguzi ndiyo yenye mamlaka na dhamana ya kuendesha na kusimamia chaguzi za wabunge na rais nchini. Katika kutekeleza majukumu hayo kuna sheria kanuni na miongozo ya kufuata ikiwemo kuwa fair kwa vyama na wagombea wote bila upendeleo

Hata hivyo tume hii imeonyesha upendeleo mkubwa na wa dhahiri kwa CCM na mgombea wake dhidi ya Chama kikuu cha upinzani nchini na mgombea wake.

Hapa chini ni namna Tume ilivyofumba macho uvunjaji wa wazi wa maadili ya uchaguzi kwa kuinufaisha CCM

1. Mgombea wa CCM Magufuli mara kadhaa akiwa kanda ya Ziwa amekuwa akitumia kilugha
Magufuli amekuwa akiongea kilugha kinyume cha utaratibu wa kisheria na maadili ya uchaguzi, lakini Tume haijamuandikia barua ya onyo kuhusu jambo hili, lakini yenyewe iko mbiombio kukekemea wapinzani

2. Vyombo vya habari vya serikali vimekuwa na upendeleo kwa CCM na mgombea wake dhidi ya Upinzani na tume haijavionya
Sheria ya uchaguzi inataka vyombo vyote vya habari vya umma vitoe air time sawa kwa kila mgombea kipindi cha uchaguzi lakini vyombo hivyo vimekuwa na upendeleo wa kutisha kwa Magufuli dhidi ya wagombea wa upinzani akiwemo mheshimiwa Lissu, lakini tume ya Taifa ya uchaguzi haijavionya vyombo hivi kuwa vinakiuka kanuni na maadilibya uchaguzi

3. Rais Magufuli amewahi kutoa kauli kuwa Haiwezekani awape mishahara wakurugenzi wanaosimamia chaguzi huko kwenye halmashauri halafu watangaze Mpinzani kushinda, NEC haikuwahi kukemea hiyo kauli

Tume ya Taifa ya uchaguzi haijawahi kukemea kauli hiyo, hijawahi kumuandikia rais Magufuli barua yoyote ya kupinga kauli hiyo. Hata ksma aliitoa zamani, lakini chaguzi nyingi za marudio zimepita, na sasa tupo kwenye uchaguzi huu, kauli haijafutwa na NEC haijawahi kutaka ifutwe, kwa hiyo agizo haramu la kutotenda haki kutoka kwa rais bado lipo na NEC haijakemea chochote!

4. Mgombea wa CCM ndugu Magufuli ametoa kauli za kutisha wananchi wasifanye maamuzi huru kwenye uchaguzi huu kwamba wasipochagua wagombea wa CCM atawanyima maendeleo na NEC iko kimya tu

Hili ni kosa kubwa sana, NEC ilipaswa kumuonya rais Magufuli kuwa kutishia kuwanyima wananchi maendeleo, kuwabagua kwa namna yoyote ni kinyume cha sheria za nchi, siyo lengo la uchaguzi, ni kauli inayotishia amani, na kuleta vurugu kama vile uasi katika nchi maana maeneo yatakayobaguliwa makusudi kunyimwa maendeleo yanaweza kuanzisha uasi wa kujitenga ili yajiletee maendeleo. NEC haimuonyi Magufuli

5. NEC badala ya kusimamia uchaguzi na kuwa fair, na yenyewe inajiingiza katika kuipigia kampeni CCM kwa kuponda ilani za uchaguzi za vyama vingine

Juzi hapa Mkurugenzi wa NEC bwana Mahera alisikika wazi akiponda ilani ya vyama vingine kama ya Chadena kuhusu vitu mbalimbali ikiwemo sera yakebya madini. Siyo kazi ya tume kupigia kampeni chama fulani. Kwenye hili hatujaona bwana Mahera akichukuliwa hatua zozote juu ya Ukada na mapenzi yake ya dhahiri kwa CCM

6. Waziri Mkuu anazunguuka nchi nzima kufanya kampeni kwa kutumia rasilimali za serikali
Ukiachilia rasilimali fedha, kuna rasilimali muda. Waziri mkuu anatuibia sisi Watanzania muda wetu wa kufanya mambo ya nchi kwa kufanya mambo ya kampeni kwa mgombea wa urais wa CCM. Maadili yanakataza mawaziri kutumia rasilimali za nchi kufanya kampeni, sheria inawakataza kutoa hata matamko ya kisera na ahadi mbalimbali nyakati hizi za uchaguzi, Sasa kipindi hiki cha uchsguzi ambapo tulitegemea waziri mkuu autumie muda tunaomlipa mshahara kututumikia asimame kuendesha mambo ya serikali kipindi hiki cha uchaguzi, yeye yuko kiguru na njia mikoani, anatumia rasilimali muda, walinzi anaokuwa nao watahitaji per diem, anatumia madereva wa serikali kwenda kumfanyia Magufuli kampeni na kote huku pesa za umma zinatumika. NEC iko kimya, haijamuonya

6. CCM inatumia rasilimali za serikali, na umma, na hata za misaada ya wahisani kufanya kampeni kujinufaisha kisiasa.

Jana Karagwe, gari lililotolewa na wahisani, Donnor funded project, lenye namba DFP 5445 lilikuwa likizuunguuka huko Karagwe kutangaza ujio wa Waziri mkuu kwa ajili ya kampeni za kumnadi Magufuli. Hiki ni kinyume kabisa za sheria za uchaguzi, lakini NEC, haiwaonyi CCM juu ya suala la namna hii la kuvunja maadili na kanuni za uchaguzi.

Katika Mazingira hayo, Sisi wananchi tutaamini vipi kuwa Tume hii hii yenye upendeleo itaweza kusimamia uchaguzi huru ulio fair?.

Tume ineshayumba mpaka hivi sasa binafsi nina imani ndogo sana na tume hii!
Andiko la hovyo lililojaa upendeleo kwa CHADEMA na wagombea wake!
Halina msaada kwetu, tunapoelekea Uchaguzi Mkuu.
Uongo mwingi sana na hadithi za kutunga
Hakuna sehemu yoyote ambayo Mkurugenzi wa Tume hiyo ameipigia kampeni sera ya ccm ni HOJA YA UONGO!, Kusema Mahitaji ya watanzania ambavyo ni kweli tunayataka sio kuitangaza sera ya chama
Maji, Hospitali, Bababara, Maendeleo kwa ujumla ni HITAJI LA MSINGI LA WATANZANIA. sasa kama hii ndio sera ya ccm na CHADEMA wanalalamika, napata shida sana kuelewa maana yake,sera ya CHADEMA haina hayo mahitaji. Sasa mnatangaza nini huko mitaani? Ilani yenu ina nini?

Wakati unaandika haya (nafahamu wako watanzania wanaofahamu Mambo wamekurekebisha katika uzo huu) Ulifuatilia na kujisomea kuhusu taratibu wa Kampeni na Timu za kampeni? Majaliwa anavunjaje sheria hapo? Shida mkiona mmezidiwa mnalalamika kuonewa, kueni creative na nyie, hamjakatazwa!

Ulicho weka hapo ni upotoshaji na uongo tu, kama ilivyo kawaida yenu,kakae usome mambo kabla hujaleta hizi hekaya zenu!
 
Mimi Naweza kusema kuwa wewe huzijui Sheria vyema, unasoma upande mmoja tu. Labda niseme Sheria inasomwa Kama ambavyo inasonga ugali, katu huwezi songs ugali kwa mkono mmoja.

Lakini hivi umesahau kuwa ni Mbowe na Lissu ndio waliobifukuza hivyo vyombo vya umma? Hivi unajua kua sio kila vipindi ni vya bure katika vituo vya habari vya umma. Kuna vingine wanalipwa hasa hizo live.

Unalia na Lissu tu hatndewi Haki, vipi Lipumba, Rungwe, Membe, na wagombea wengine 10 waliobaki je wanapewa huduma hiyo.

Tume inamkemeaje wakala wa kampeni wa Mgombea fulani. Majaliwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Chama chake kimemteua kuwa wakala wa Mgombea wao kimnadi. Anatimiza majukwaa ya wagombea Ubunge na ratiba zao hayupo kwenye ratiba ya tume. Hata Lissu Kama Mnyika anaweza kufanya hivyo anaweza Mbona Zitto Kabwe alikuwa anazunguka Mikoani kuwanadi wagombea wa Chama chake na hamsemi Time imkemee? Abdull Nondo wa ACT alikuwa anazunguka Mikoani kunadi wagombea Mbona hamkusema kuhusu hilo? Toeni boriti jichoni kwenu kabla ya kibanzi kwa mwenzio.
Kauli ya Magufuli na Wakurugenzi aliitoa lini na wapi? Je mnaweza ipeleka Kamati ya Maadili?. USIKURUPUKE.

Hivi kumbe kuna vyama Ilani zao ni matusi, kuhimiza vurugu na kutishiana na si kumleta maendeleo kwa wapigakura wao. Hivi ni cha gani ambacho kikishinda, Miundominu ya Barabara, afaya, Elimu, umeme, mawasiliano hakitafanya? Mimi Kama Mwananchi nataka Sana Chama kitakacho hakikisha huduma bora za kijamii, mkulima nayafikia masoko kwa kua na Barbara nzuri, watoto wanasema vizuri na huduma za afya zinakuja Bora zaidi ya Sasa. JIPANGE NDUGU.
Hawezi kujua hayo, wao wanakariri mambo. Na ndio maana wanapigwa kila kukicha. Uwezo mdogo wa kufikiri
 
Andiko la hovyo lililojaa upendeleo kwa CHADEMA na wagombea wake!
Halina msaada kwetu, tunapoelekea Uchaguzi Mkuu.
Uongo mwingi sana na hadithi za kutunga
Hakuna sehemu yoyote ambayo Mkurugenzi wa Tume hiyo ameipigia kampeni sera ya ccm ni HOJA YA UONGO!, Kusema Mahitaji ya watanzania ambavyo ni kweli tunayataka sio kuitangaza sera ya chama
Maji, Hospitali, Bababara, Maendeleo kwa ujumla ni HITAJI LA MSINGI LA WATANZANIA. sasa kama hii ndio sera ya ccm na CHADEMA wanalalamika, napata shida sana kuelewa maana yake,sera ya CHADEMA haina hayo mahitaji. Sasa mnatangaza nini huko mitaani? Ilani yenu ina nini?

Wakati unaandika haya (nafahamu wako watanzania wanaofahamu Mambo wamekurekebisha katika uzo huu) Ulifuatilia na kujisomea kuhusu taratibu wa Kampeni na Timu za kampeni? Majaliwa anavunjaje sheria hapo? Shida mkiona mmezidiwa mnalalamika kuonewa, kueni creative na nyie, hamjakatazwa!

Ulicho weka hapo ni upotoshaji na uongo tu, kama ilivyo kawaida yenu,kakae usome mambo kabla hujaleta hizi hekaya zenu!

Hata kama vyama visipolalamika sisi wananchi tukiona uonevu tutalalamika maana na sisi tusio na vyama maalum ni wadau wa uchaguzi maana tunapiga kura.

Tukiona uonevu wowote dhidi ya mtu au chama chochote, na upendeleo kwa chama kingine tutasema tu.

Kitendo cha Magufuli kutisha wananchi kuwa hatowapelekea maendeleo wakichagua upinzani, tume ilipaswa kukemea matamshi hayo yanayoblackmail watu kwenye uchaguzi!
 
We waulize tume Kassim Majaliwa anazunguka nchi nzima kufanya kampeni kama nani? Na ratiba yake iko wapi na imetolewa na Mamlaka ipi? Wakikujibu niambie.
Jibu lao ni simple tu, watasema hakuna mgonbea au chama kilichopeleka malalamiko kwao kwa maandishi, japo kwa wengine hawatasubiri malalamiko kama mkurugenzi alivyofanya kwa LISSU.
 
Kwa mujibu wa katiba ya nchi na kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, Tume ya Taifa ya uchaguzi ndiyo yenye mamlaka na dhamana ya kuendesha na kusimamia chaguzi za wabunge na rais nchini. Katika kutekeleza majukumu hayo kuna sheria kanuni na miongozo ya kufuata ikiwemo kuwa fair kwa vyama na wagombea wote bila upendeleo

Hata hivyo tume hii imeonyesha upendeleo mkubwa na wa dhahiri kwa CCM na mgombea wake dhidi ya Chama kikuu cha upinzani nchini na mgombea wake.

Hapa chini ni namna Tume ilivyofumba macho uvunjaji wa wazi wa maadili ya uchaguzi kwa kuinufaisha CCM

1. Mgombea wa CCM Magufuli mara kadhaa akiwa kanda ya Ziwa amekuwa akitumia kilugha
Magufuli amekuwa akiongea kilugha kinyume cha utaratibu wa kisheria na maadili ya uchaguzi, lakini Tume haijamuandikia barua ya onyo kuhusu jambo hili, lakini yenyewe iko mbiombio kukekemea wapinzani

2. Vyombo vya habari vya serikali vimekuwa na upendeleo kwa CCM na mgombea wake dhidi ya Upinzani na tume haijavionya
Sheria ya uchaguzi inataka vyombo vyote vya habari vya umma vitoe air time sawa kwa kila mgombea kipindi cha uchaguzi lakini vyombo hivyo vimekuwa na upendeleo wa kutisha kwa Magufuli dhidi ya wagombea wa upinzani akiwemo mheshimiwa Lissu, lakini tume ya Taifa ya uchaguzi haijavionya vyombo hivi kuwa vinakiuka kanuni na maadilibya uchaguzi

3. Rais Magufuli amewahi kutoa kauli kuwa Haiwezekani awape mishahara wakurugenzi wanaosimamia chaguzi huko kwenye halmashauri halafu watangaze Mpinzani kushinda, NEC haikuwahi kukemea hiyo kauli

Tume ya Taifa ya uchaguzi haijawahi kukemea kauli hiyo, hijawahi kumuandikia rais Magufuli barua yoyote ya kupinga kauli hiyo. Hata ksma aliitoa zamani, lakini chaguzi nyingi za marudio zimepita, na sasa tupo kwenye uchaguzi huu, kauli haijafutwa na NEC haijawahi kutaka ifutwe, kwa hiyo agizo haramu la kutotenda haki kutoka kwa rais bado lipo na NEC haijakemea chochote!

4. Mgombea wa CCM ndugu Magufuli ametoa kauli za kutisha wananchi wasifanye maamuzi huru kwenye uchaguzi huu kwamba wasipochagua wagombea wa CCM atawanyima maendeleo na NEC iko kimya tu

Hili ni kosa kubwa sana, NEC ilipaswa kumuonya rais Magufuli kuwa kutishia kuwanyima wananchi maendeleo, kuwabagua kwa namna yoyote ni kinyume cha sheria za nchi, siyo lengo la uchaguzi, ni kauli inayotishia amani, na kuleta vurugu kama vile uasi katika nchi maana maeneo yatakayobaguliwa makusudi kunyimwa maendeleo yanaweza kuanzisha uasi wa kujitenga ili yajiletee maendeleo. NEC haimuonyi Magufuli

5. NEC badala ya kusimamia uchaguzi na kuwa fair, na yenyewe inajiingiza katika kuipigia kampeni CCM kwa kuponda ilani za uchaguzi za vyama vingine

Juzi hapa Mkurugenzi wa NEC bwana Mahera alisikika wazi akiponda ilani ya vyama vingine kama ya Chadena kuhusu vitu mbalimbali ikiwemo sera yakebya madini. Siyo kazi ya tume kupigia kampeni chama fulani. Kwenye hili hatujaona bwana Mahera akichukuliwa hatua zozote juu ya Ukada na mapenzi yake ya dhahiri kwa CCM

6. Waziri Mkuu anazunguuka nchi nzima kufanya kampeni kwa kutumia rasilimali za serikali
Ukiachilia rasilimali fedha, kuna rasilimali muda. Waziri mkuu anatuibia sisi Watanzania muda wetu wa kufanya mambo ya nchi kwa kufanya mambo ya kampeni kwa mgombea wa urais wa CCM. Maadili yanakataza mawaziri kutumia rasilimali za nchi kufanya kampeni, sheria inawakataza kutoa hata matamko ya kisera na ahadi mbalimbali nyakati hizi za uchaguzi, Sasa kipindi hiki cha uchsguzi ambapo tulitegemea waziri mkuu autumie muda tunaomlipa mshahara kututumikia asimame kuendesha mambo ya serikali kipindi hiki cha uchaguzi, yeye yuko kiguru na njia mikoani, anatumia rasilimali muda, walinzi anaokuwa nao watahitaji per diem, anatumia madereva wa serikali kwenda kumfanyia Magufuli kampeni na kote huku pesa za umma zinatumika. NEC iko kimya, haijamuonya

6. CCM inatumia rasilimali za serikali, na umma, na hata za misaada ya wahisani kufanya kampeni kujinufaisha kisiasa.

Jana Karagwe, gari lililotolewa na wahisani, Donnor funded project, lenye namba DFP 5445 lilikuwa likizuunguuka huko Karagwe kutangaza ujio wa Waziri mkuu kwa ajili ya kampeni za kumnadi Magufuli. Hiki ni kinyume kabisa za sheria za uchaguzi, lakini NEC, haiwaonyi CCM juu ya suala la namna hii la kuvunja maadili na kanuni za uchaguzi.

Katika Mazingira hayo, Sisi wananchi tutaamini vipi kuwa Tume hii hii yenye upendeleo itaweza kusimamia uchaguzi huru ulio fair?.

Tume ineshayumba mpaka hivi sasa binafsi nina imani ndogo sana na tume hii!

TV ya Taifa na Radio ya Taifa imekuwa na full coverage ya Kampeni za CCM, I do not believe kwamba hao wengine wamekataa coverage
Mgombea wa CCM tunajua ni incumbent candidate hivyo bado ana nguvu za kiti, lakini pia tuwe makini na waangalifu na kitu kinachoitwa "power overriding"
 
Hata kama vyama visipolalamika sisi wananchi tukiona uonevu tutalalamika maana na sisi tusio na vyama maalum ni wadau wa uchaguzi maana tunapiga kura.

Tukiona uonevu wowote dhidi ya mtu au chama chochote, na upendeleo kwa chama kingine tutasema tu.

Kitendo cha Magufuli kutisha wananchi kuwa hatowapelekea maendeleo wakichagua upinzani, tume ilipaswa kukemea matamshi hayo yanayoblackmail watu kwenye uchaguzi!
Sio kweli kwamba wewe huna chama maalumu, Chama Unacho na ndio ulichohangaika kukisemea hapa
UONGO UONGO MTAACHA LINI NYIE NDUGU ZETU?
KILA WAKATI NYIE NI WATU WA KULIA LIA TU NAKUTAKA SYMPATHY VOTES BADILIKENI, ACHENI SIASA ZA KUNUNULIKA
 
Eti watanzania wanahitaji kuona barabara, elimu, madini yao yasiibiwe, ni kichaa kufikiri hivyo, mie nahitaji uhuru haki na maendeleo ya watu, maendeleo ya vitu yawe matokeo, sina chakula unionyeshe ndege!
 
Mkurugenzi wa tume anaifundisha ATM namna ya kutoa hela.

Hivyo ni vitu basic kwa serikali yoyote duniani. Kujenga hayo madufe ni rahisi ila kazi ya tathmini ya uanze na kipi, wapi na kwa gharaa zipi ndiyo kazi ngumu inayohitaji sera makini na aina ya uongozi unaofikiri kabla ya kujijengea hovyohovyo. Na huu uchaguzi unahusu kutafuta uongozi utakaoweza kudeliver.

Msajili aache vyama vinadi sera zao tuzisikie wenyewe asiwafundishe na wala asiwafokee.

Siyo kazi ya tume kufundisha wananchi aina ya kiongozi anayewafaa, wao kazi yao ni kuratibu uchaguzi baasi mambo mengine ni siasa, na siasa siyo kazi yao!
 
TV ya Taifa na Radio ya Taifa imekuwa na full coverage ya Kampeni za CCM, I do not believe kwamba hao wengine wamekataa coverage
Mgombea wa CCM tunajua ni incumbent candidate hivyo bado ana nguvu za kiti, lakini pia tuwe makini na waangalifu na kitu kinachoitwa "power overriding"

Sheria ya uchaguzi haitambui kitu ulichokisema "power of incumbent". Sheria ya uchaguzi inataka fairness ya vyombo vya habari vya Taifa kwenye kutangaza kampeni za wagombea wote
 
Kwasababu umekaza akili, huwezi kujua kwanini wanafull coverage kwenya kampeni, Nyie si mliwafukuza?
Mlisahau kama kuna kampeni na inabidi mtunze fedha za matangazo, mkalamba pesa zote saivi hamna hata fedha za matangazo mnataka kuzua uongo kuwa kuna watu wanapendelewa, pelekeni fedha muone kama hamtarushwa hewani
 
Back
Top Bottom