Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaanza kutoa matokeo ya rufaa za Udiwani na Ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020

Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaanza kutoa matokeo ya rufaa za Udiwani na Ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020

Joined
Feb 18, 2019
Posts
53
Reaction score
539

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kutoa matokeo ya rufaa za udiwani na ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 28 Oktoba 2020.

Leo tume imetoa matokeo ya rufaa 55 kama ifuatavyo:

1. Imekubali rufaa 15 na kuwarejesha wagombea katika kinyang'anyiro cha uchaguzi.

2. Imekataa rufaa 15 za wagombea ambao hawakuteuliwa.

3. Imekataa rufaa 25 za kupinga walioteuliwa.

IMG_20200908_150033.jpg


IMG_20200908_150030.jpg

----------

1599640087354.png

1599640108949.png

1599640132299.png

1599640146776.png

1599640169472.png
 
Wapuuzi sana ninyi, mnajifanya ni Tume huru wakati kila mtu anaona namna mnavyotekeleza majukumu yenu kwa kumfurahisha Magufuli. Nchi hii ikiingia kwenye machafuko lawama na laana zote zitakua juu yenu MILELE.
 
Hapo wagombea wote waliokata rufaa ni wapinzani, maana yake kwa vyovyote vile watakaoumia ni wapinzani, hata kama wapo watakaorejeshwa kugombea lakini kwa hao ambao hawatarejeshwa nalo bado litabaki pigo kwa upinzani.

Hivi kwanini hakuna mgombea wa CCM hata mmoja aliekatwa? au wao walienda kusomea wapi kujaza hizo fomu? Tume iwaache wagombea wote sanduku la kura ndio likaamue.
 
Tume tume, chonde chonde, Amani ya Taifa hili ipo mikononi mwenu. Watanzania hawa wameshachoka hawana tumaini jingine tena bali Uchaguzi huu kuwa HURU na HAKI ili watakayoyaamua basi yasimame na si vinginevyo.

Hao wasimamizi wa uchaguzi majimboni waliokata majina kwa sababu hizo basi nao wachukuliwe hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wenzao wenye akili kama zao.

Tunasubiri - bado tuna imani na nyie.
 
Back
Top Bottom