Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaanza kutoa matokeo ya rufaa za Udiwani na Ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020

Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaanza kutoa matokeo ya rufaa za Udiwani na Ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2020

Someni kiambatanisho

Hongera Sana Tume ya Uchaguzi Ya Taifa Kwa Kutenda Haki

i
FB_IMG_15995684810076334.jpg
FB_IMG_15995684849553547.jpg
 
Hapo wagombea wote waliokata rufaa ni wapinzani, maana yake kwa vyovyote vile watakaoumia ni wapinzani, hata kama wapo watakaorejeshwa kugombea lakini kwa hao ambao hawatarejeshwa nalo bado litabaki pigo kwa upinzani.

Hivi kwanini hakuna mgombea wa CCM hata mmoja aliekatwa? au wao walienda kusomea wapi kujaza hizo fomu? Tume iwaache wagombea wote sanduku la kura ndio likaamue.
CCM ilitawanya wataalamu wake nchi nzima kwenda kuwasaidia wagombea wake jinsi ya kujaza fomu kikamilifu!
 
CCM ilitawanya wataalamu wake nchi nzima kwenda kuwasaidia wagombea wake jinsi ya kujaza fomu kikamilifu!
Achana na hadithi za kusimuliwa, mimi sio mtaalamu wala nini lakini nilimsaidia mgombea wa Ccm hasiyejua kusoma wala kuandika kujaza form yake
 
Naiomba kule Zanzibar tume isiwarudishe wale wa ACT ni hatari
Ni hatari wakirudishwa au ni hatari wasipo rudishwa?

Wasipo rudishwa ni hatari maana watakua wanapora haki yao na haki ya wapiga kura mchana kweupe.

AMANI ni tunda la HAKI, km hakuna haki ni vigumu kuzungumzia Amani
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kutoa matokeo ya rufaa za udiwani na ubunge zilizokatwa na wagombea katika Uchaguzi mkuu wa 28 Oktoba 2020.

Leo tume imetoa matokeo ya rufaa 55 kama ifuatavyo:

1. Imekubali rufaa 15 na kuwarejesha wagombea katika kinyang'anyiro cha uchaguzi.

2. Imekataa rufaa 15 za wagombea ambao hawakuteuliwa.

3. Imekataa rufaa 25 za kupinga walioteuliwa.


Hapo bado la kutafuta tunalitafuta.

Suruhu hapa ilikuwa kuacha sanduku la kura kufanya kazi yake.

Ushindi wa mezani wa nini?
 
KWA UFUPI WAGOMBEA 40 KATI YA 50 WAMEKUWA APPROVED 10 WAMELIWA KICHWA NA KWA VYOVYOTE NI WA UPIZANI.

KWA KASI HII TUME ITATUMIA SIKU 13KUMALIZA RUFAA 557
 
Back
Top Bottom