PostGE2025 Tume ya Uchunguzi yenye lengo la kudogosha mauaji ya watanganyika

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Na je Uhuru na Ruto waliishia wapi baada ya kushtakiwa?? ICC is just a toothless paper tiger
SAMIA is not UHURU.

UHURU was not a head of state back in 2008, SAMIA is a head of state.

Facts of their case differ marginally, and it is astounding to see a person making an analogy of them.

BY THE WAY, after the ICC we clearly can see RUTTO's behavior adjusted, he is a cornered CAT.

Bila ya ICC, RUTTO na Polisi wangeua maelfu ya Gen-Z, lakini kwasababu waliadabishwa hawathubutu.

NB: Lengo la ICC siyo kukufunga tu, bali kurekebisha tabia yako. SAMIA akifika tu pale wengine watabadilika.
​
 
Ukisoma madini kama haya unabaki Kumwomba Mungu usikutane na Kichwa kinacho uchosha mwili kwa kudundika mziki wa watawala. Kaka Malcom Lumumba Historia hujirudia na hii hapa kwetu imewahi kutokea, ni Nchi gani ziliweza kufikia hali na mazingira kama tuliyonayo lakini yaliweza kupunguza athari za vifo na machafuko kwa Ujumla?
 
J

Je hii iliwezekana kwa Nkurunzinza?maana hatukusikia ICC wakiweka pressure ya kumkamata na kumshtaki mpka umauti ulipomkuta 2020... MALCOM LUMUMBA
Nkurunzinza anaitoa Burundi ICC shauri lilikuwa bado halijafunguliwa ila kulikuwa na minong'ono.

Angeendelea kuwepo mpaka leo nadhani angekuwa ashafunguliwa shauri na washatoa Indictment.

Omar Al Bashir alikuwa na nguvu kuliko Nkurunzinza na Samia lakini alikuwa anasakwa na ICC hadi akawa anaogopa kusafiri. Wewe unaamini kabisa kwamba wakiamua kumtafuta Samia hawa wazungu watashindwa ???
​
 
AFRIKA KUSINI YA MAKABURU.
Baada ya vita baridi (Cold War) kuisha 1991, Afrika Kusini kulikuwa na vuguvugu zito ambalo lingepelekea vita kubwa mno (Racial War) na umwagikaji mkubwa wa damu. Makaburu waliusoma mchezo mapema sana, na kina De Clarke wakaenda gerezani kumpigia magoti Mzee Nelson Mandela. Kama wangeendelea kukomaa basi machafuko makubwa yangetokea na mauaji yangekuwa ya kutisha mno. Ila walikubali kushindwa kimkakati na kufanikiwa kwa sehemu kubwa kuwahadaa wananachi kupitia The Truth Commission.

MOROCCO 2011 (ARAB SPRING)
Wakati machafuko yameanza Tunisia, Libya, Egypt na Syria, mfalme wa Morocco Idriss alitoka nje na kutoa hotuba kukubali mabadiliko. Mwaka huohuon walifanya mabadiliko ya katiba na uchaguzi wa wabunge. Morocco ikatulia tuli, na maandamano yakawa yameisha kihivyo yani. Serikali ya Morocco ina nguvu mno, tokea miaka na miaka. Majasusi wao na jeshi lao wanapewa mafunzo na mataifa kama Israel, Ufaransa na Marekani, hivyo siyo taifa la mzaha-mzaha. Mfalme Idriss alikuwa anaweza kuamua kuua tu maelfu ya watu wanaoandama kama ambavyo CCM+TISS+PT+TPDF walifanya, ila alitumia hekima ya hali ya juu mno.

Waliokomaa kama kina Mubarak, Ghaddafi na Assad kutumia silaha nzito yaliwakuta. Kiufupi hata uwe kiongozi mzuri vipi, ni lazima ujifunze kusoma alama za nyakati na kufahamu ni wakati upi unatakiwa kuondoka. Hata kama maandamano yanaratibiwa na watu wa nje, basi ni lazima kuna nyufa fulani ambazo adui amezikuta na akaamua kuzitumia. Ghaddafi tunampenda, lakini ukweli ni kwamba kuna mambo mengi utawala wake ulikosea sana kufanya nchini mle. Sasa hili somo JAKAYA ataenda kujifunza muda siyo mrefu..
​
 
Niliwahi kufikiria hii ndio itakuwa mbinu ya kutunusuru na Machafuko na kuigawa nchi vipande vipande, Makaburu wasingemfata Mandela Story ingekuwa nyengine, Kwa hali tuliyonayo siioni CCM ile inayoweza kuamka na kusema Nchi Kwanza, CCM yote imekuwa Corrupt kila mmoja anaangalia tumbo lake kuliko hatma ya vizazi vijavyo.
 
Muda utasema, wewe subiri uone....​
 
bahati mbaya sana Akili kama hizi huwezi kuzikuta zimewazunguka Viongozi wetu, Wazungukwa na Mamburula yanayotoa suluhu za kuua Mende kwa kutumia nyundo.
 
Samia hana pa kwenda zaidi ya kujificha Kizimkazi na Oman.
 
Naomba kufahamu,hawa mashehe wanaoibuka kila siku lengo lao hasa nini na nani anawatuma kufanya hivyo.

Pili je endapo tume iliyoundwa na samia itakuja na majibu yakuridhisha kwamaana ya kuwajibisha waliohusika na kuandaa mchakato wa katiba mpya.?
 
Hakika haya unayosemq nimeona series inaitwa A GENTLEMAN FROM MOSCOW
 
Asante sana MALCOM LUMUMBA , kwa kutupa kuweza kufahamu, ambayo hatukuwa tukifahamu. Mungu akubariki .
 
Yaan kwasaivi hiyo TUME ndo last hope yao, kwasabb wakibaki madarakani ni issue na wakijiuzuru pia ni issue labda tu ICC na WATANZANIA waamue kupotezea Damu za watanganyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…