PostGE2025 Tume ya Uchunguzi yenye lengo la kudogosha mauaji ya watanganyika

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Very insightful and informative thread kutoka kwa MALCOM mwenyewe.

Binafsi huwa kuna namna nakwazika sana na hawa wasomi wabobezi wa kibongo na jinsi wanavyotumia taaluma zao.

Umemuongelea huyo mwenyekiti ya hiyo TUME YA KUZIMU jaji Othman Chande kuwa ni mwanasheria nguli na mzoefu wa kudeal na hizo kesi kubwa kwenye mahakama za kimataifa...

...kwa hiyo kumbe ameteuliwa hapo lengo ikiwa ni kuhakikisha anatumia waledi waledi mkubwa alionao pamoja na uzoefu kuhakikisha anamuokoa Samiya na genge lake la akina Kikwete,Mkunda,Wambura ,Rostam wanapona na hawaingii hatiani kwa mauaji ya maelfu ya watu wasio na hatia waliofanya..

..Yaani ni kuwa huyo Jaji Othman Chande akiwa na akili zake timamu kabisa atatumia ujuzi wake wa kisheria kupindisha ukweli wa kile kilichotokea hili tu akoe kikundi cha watu wasiozidi 20 wasikutane na rungu la ICC, na kuacha maelfu ya familia za watu waliopoteza wapendwa wao wakiumia bila kuona haki ikitendeka?

Yaan watu wamefanya mauaji ya watu zaidi ya 11,000 tena kwenye mazingira ambayo wengi hawakuwa na hatia, haya baada ya hapo wakaenda kuzikwa kinyama sana, halafu anatokea msomi mmoja anaamua kuwatetea wahusika wa mauaji hayo ambao ni kikundi cha watu wachache sana, na kuwanyima haki wahanga na familia zao waendelea kuumia? Huku wahusika wakiendelea kufurahia maisha?..

..ndio maana wasomi wa kiafrika kuna muda huwa wanadharauliwa sana maana wanatumia usomi wao katika namna ya kumtumikia shetani.
 
The day has come....

1) Je, watasema ukweli ???

2) Je, watawasigina marehemu ???

3) Je, kuna baadhi watatolewa kafara ???

4) Watatueleza sisi nini leo hii ???
​


Afrika Mashariki hakuna kama Jaji Mohamed Chande Othman.

Jaji Mkuu wa zamani wa Tanzania, mwanachama wa timu iliyounda ICC, mjumbe wa Independent Expert Review ya ICC, mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Uhalifu wa Rwanda na Timori Mashariki, na mtaalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu.

Mpambe wa daraja la juu kabisa. Hakuna anayemfikia Afrika Mashariki yote.🔥
 
Kuna nguli mwingine alikuwa anaitwa Johnson Mbwambo..
 
Mshupaza shingo huvunjika!

Naona BEBERU anataka kukamata serikali nzima ya Malawi.

Ila hamuwezi kulaumu ilhali tumewashauri na kuwakemea miaka humu ndani.

Kiukweli, wengi tulishafahamu mchezo utaendaje lakini maafisa usalama uchwara hawana ufahamu...
​
 
Sijamjua huu Uzi uliojaa Nondo ilikuwaje ukanipita
 
Hapo Kenya wakina Kenyatta na Rutto waliachiwa huru lakini mawakili wao na watu wengine wa vyombo vya usalama walifunguliwa kesi ya Obstruction of Justice. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2015. Mwaka 2026 kudhani kwamba utaweza kufanya kama walivyofanya wakina Kenyatta ni kupaka rangi upepo.

Wiki hili limekuwa baya kwa serikali ya CCM, kuliko kipindi chake kingine chochote. Kwanza kabisa serikali haina uhalali (Has no legitimacy), imetengwa (A diplomatic pariah) na ina viongozi wasiokuwa na uwezo (Extremely incompetent leaderiship) tangu nchi hii ipate uhuru.

Jambo ambalo wengi tumeshindwa kulielewa ni kwamba Marekani anapambana na Tanzania kwa kutumia sheria zake bila kutumia ICC (International Criminal Court) kwasababu yeye mwenyewe siyo mwanachama, na akitumia Rome Statute ina maana atakuwa anaipa ICC uhalali ambao yeye mwenyewe, USA, ISRAEL, RUSSIA na UCHINA wamepinga kwamba mahakama haina.

Marekani akitumia maneno kama Crimes Against Humanity na Genocide, hata yeye atakosa uhalali kwasababu dunia itasema mbona yeye anafanya hivyo kule Gaza, Iran na Lebanon. Hivyo Marekani ametumia mlango wa nyuma (Back-Door) ambapo ameamua kutumia sheria zake za ndani (Domestic Law), hasahasa Human Rights, ambapo sheria za Marekani zinasema kwamba Marekani itashirikiana kidiplomasia na kiuchumi na nchi ambazo zinaheshimu haki za binadamu tu.

Aheri uende ICC utapewa baadhi ya haki. Marekani kutumia sheria zake kuwahukumu watawala wa nchi nyingine ni jambo baya na hatari zaidi kwasababu, ni UBEBERU ambao hauna kichwa wala miguu na hauwezi kuwapa watawala wa nchi nyingine haki. Ni kama alivyofanywa Maduro na Noriaga, na sasa Castro. Kiufupi kama hii sheria ikipita ina maana hakuna mtu wa serikali ya Tanzania ataingia Marekani na kwenye nchi washirika wa Marekani. Fedha za kigeni zitafuatiliwa na hata mali binafsi za mafisadi kama Kikwete wenye majumba NewYork hali zao zitakuwa mbaya.

Hiyo TISS iliyofubaha, zile account zake za Ubelgiji na Uswisi ndiyo vile tena, kuzifikia litakuwa jambo gumu. Ukizingatia uwezo wetu kiusalama uko chini mno, ndiyo imekula kwetu. Uchina, Urusi, Iran, Pakistan na Korea Kaskazini ambao ndiyo washirika wakubwa wa CCM+TISS+JWTZ kwenye huu ulimwengu wa giza hawawezi kuwasaidia kwa kiwango kikubwa bila kuwapa kitu kikubwa.

Njia pekee ya kukwepana na hili ni Samia kukubali kuchutama yaishe. Marekani anazitaka mali za Tanzania, na hii ndiyo imekuwa njia pekee ya kuhakikisha anapora zote. Ninyi mnaweza kutetea serikali yenu ya CCM kwasababu zenu, lakini hata Wamarekani wasipopitisha hii sheria bado imekula kwenu, kwasababu CCM itawapa mali nyingi ili za watanganyika ili waponye shingo zao. Marekani yuko kwenye kihoro cha kuokoa uchumi wake na yuko radhi aue hata mamilioni.

Mpaka kufika mwaka 2030 Tanzania itakuwa haina utofauti wowote na Nigeria..
Hata wewe utakaa pembeni ukiwa umestaafu kwenye nchi ambayo haina mwelekeo huku ukijuta.
​
 
Tume imefanya kile tulichotarajia kama wanachama hai wa chama nanserikali!

Pongezi kwa tume ya chande!!

Sisi CCM tuna desturi yetu ya kuyamaliza mambo yetu ndani ya chama!!

Kilichopangwa kabla ya uchaguzi kufanyika ndicho kitakacho tokea!!

Kwa sasa naona operation PJLK inatekelezwa J na L Tayari bado P,L na K!!
 
Jukwaa la Wahariri nchini, sijui wamepata wasaa kusoma bandiko hili?
 
Tanzania ina mikataba mingi ya ya siri mizito ya ushirikiano wa kiuchumi, misaada, uwekezaji, usalama na diplomasia na mataifa mbalimbali. Hivyo mambo mengi huishia kwenye “concern”, “discussion” na “ushauri”, lakini si mabadiliko ya moja kwa moja kama watu wanavyotarajia. Tuna mikataba mingi ya sisi na wao ya kidiplomasia na ndo maana hata serikali ya Tanzania hata uipigie kelele kuhusu ushoga haitachukua action yoyote.

Msitegemee mabadiliko makubwa, Samia yuko hadi 2030
 
Hata ikijitoa, mambo yalianzia nchi ukiwa mwanachama!
 
De Jure Tanzania na Marekani wako sawa na wana makubaliano.

De Facto Tanzania hawezi kuwa sawa na taifa kubwa kama Marekani likiamua kuwaumiza.

Muingereza na Israel washirika wakubwa kabisa wa Marekani wenye makubaliano ya siri ya kidiplomasia na kiusalama, waliwahi kuingia kwenye 18 za Marekani,walijuta. Uingereza alipewa masharti ya kufanya mabadiliko au uchumi wake kuwekewa vikwazo na kufilisiwa kabisa akaufyata. Israeli aliambiwa aondoe vikosi vyake Misri la sivyo atashughulikiwa, akaufyata.

Kama MITI MIBICHI ilitendwa hivi, unadhani MTI MKAVU (Tanzania) atacheza na Marekani kweli endapo beberu kaamua kuwashughulikia ???

Halafu tulizungumza hapo mwanzo ukasema hakiwezi kutokea chochote: Mwaka huu siyo mrefu tutarudi kwenye huu uzi hapa.
​
 
Hizo ni wishes za walioikatia tamaa Tanzania. Wanasiasa huja na kuondoka lakini Tanzania itabaki milele na milele Ni vyema kutatua matatizo yetu wenyewe ndani kwa ndani kuliko kujianika kwa hao unaowafagilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…