Tumeacha kutetea bandari zetu sasa tunatetea mwekezaji muislam, waziri muislam na rais muislam!

Tumeacha kutetea bandari zetu sasa tunatetea mwekezaji muislam, waziri muislam na rais muislam!

Tatizo nchi hii akiongoza mvaa kobasi kuna watu roho zinawawasha ata awe mwema kiasi gani,Mwalimu Nyerere alilia kuhusu ubinafshaji wa mashirika ya Umma lakini tulibinafsisha. Miaka kadhaa nyuma tumesaini mikataba ya reli SGR na bwawa la Mwalimu Nyerere rufiji,Tuna mkataba wa mradi wa umeme pia maporomoko ya Rusumo(Tanzania,Burundi na Rwanda) walalamikaji wa sasa hawajawai kulalamika popote na wala awahoji.
Tupendane
Contractor unamlinganusha na mwekezaji? Sgr na hiyo miradi pale ni mkandarasi anajenga akimaliza anasepa mnaendesha wenyewe.
 
Makafir ni wale walio nyuma kielimu sheikh!
Wewe kafiri elimu yako imekufikisha wapi? Hao unaojifariji kua hawana elimu,wao wana natural resource ya Gas na Oil tu na wameitumia kubadilisha maisha yao na kua matajiri,

Au hujui maana ya Elimu ni nini?

Wewe una elimu na umeshindwa kuyatawala mazingira yaliyokuzunguka na kutumia vizuri resources ulizo nazo kubadili maisha yako,Acha kujifungia Kijijini kwenu tu,toka nje ukaione Dunia upate exposure kidogo.
 
Jeh

Jehanam wanakwenda wasiomwamini Mungu wa Kweli na wafanyao ushirika na majini.
Huko mnapouziwa mafuta ya upako ili muwe matajiri ghafla si ndio kila siku mnatoleana mapepo? Wewe umewahi kuliona hilo jini? Au ndio umekaririshwa na waliokushikia akili?
 
wacha ubaguzi.
mimi ni mkristu lakini nakubaliana na uwekezaji wa DPW naamini kuna wakristu na wasio na dini wengi wanakubali jitihada za Mhe. Rais na Serikali yake katika kukuza uchumi wa nchi.

lakini wapo baadhi wachache, wanao ingiza chuki ya kidini kwenye suala hili la uwekezaji, huo ni upuuzi na kamwe usipewe nafasi, Serikali isonge mbele isiwasikilize wapuuzi.
Kenya imeingia mikataba ya uwekezaji na nchi ya kiislamu ya IRANI lakini huwezi kusikia huu upuuzi, tuache ujinga.

Mama asibabaishwe wala kuyumbiswa na wanafiki....asonge mbele kwa masilahi ya Taifa letu.
Mbona nyie watu mna vichwa vigumu nani amewakataa DPW kinachokataliwa ni namna mkataba ulivyo.
Hii nchi una watu wa ajabu sana
 
Uzalendo ni kuchukua maaskofu na kwenda nao press conferences?
Uzalendo ni maaskofu kuacha makanisa na kwenda viwanjani kumtukana Rais?

Yaani uzalendo Tanzania wanao maaskofu tu?...
Wengineo wote hawana uzalendo??

Hao maaskofu wakati watu wanapigwa risasi uzalendo wao ulikuwa wapi??
Kipindi cha "Yohana" ndio kipindi pekee Maaskofu waliulizwa uraia wao mpaka kupelekea kuulizwa vyeti vya kuzaliwa vya bibi zao.
Ulikuwa unanyonya kiasi hayo hukuyashuhudia!!??
Kipindi cha "Yohana" ndiyo kipindi tulijua kuwa hawa viongozi wetu wa madhehebu ya Kikristo walivyo na PhD. za kweli kupitia "Waraka/Nyaraka" zao na maandiko yao mbalimbali katika kupinga nchi ilivyokuwa inaendeshwa.

Huyu "Yohana" kwa mujibu wa bandiko lako, atakuwa alikuwa ni mvaa kobazi, kwa mujibu wa bandiko lako.
 
naona kuna watu wanahoji mkataba kwa mihemko badala ya hoja, nadhani watanzania inabidi tuungane kukosoa madhaifu yaliyopo kwenye mkataba ili yarekebishwe, mana athari za mkataba sio za dini moja wala mtu mmoja bali zitatukumba wote pamoja na vizazi vyetu, dini zisituchanganye huu ni wakati muhimu wa kuungana bila kujali itikadi.

Inahuzunisha sana mtu anachangia kwa mihemuko ya dini balada ya hoja, nadhani hata wenzetu nchi nyingine watakuwa wanatushangaa kwamba hili jambo hatulichukulii kwa uzito bali ni kama tunapigania dini na viongozi wetu na pia viongozi wa dini wanahaki ya kuhoji mana nao ni watanzania kama sisi lakin wanatakiwa kuhoji kwa hoja na kama unawapinga nawe pinga kwa hoja lakin si kukimbilia kutukana na kuita watu majina mabaya mi sipendi watu wanavyoita wenzao kafir au wafuga majin si maneno mazuri, kwa sasa inabidi tuungane tuwe kwamoja kuomba serikali irekebishe mapungufu yaliyomo kwenye mkataba na tuache kujibu kwa mihemko.
 
Uzalendo ni kuchukua maaskofu na kwenda nao press conferences?
Uzalendo ni maaskofu kuacha makanisa na kwenda viwanjani kumtukana Rais?

Yaani uzalendo Tanzania wanao maaskofu tu?...
Wengineo wote hawana uzalendo??

Hao maaskofu wakati watu wanapigwa risasi uzalendo wao ulikuwa wapi??
pole sana
 
Watanzania hatujawahi.kuwa na akili. Acha yatukute ya kutukuta
Kwa mantiki hiyo Unamuita Raisi wetu kuwa hajawahi kuwa na Akili?

Tatizo lako wewe upo hapa kuendeleza propaganda, na ukipata mwanya tu huwa unatupia matusi yako humu.

Wacha Ugaidi wako Gaidi we
 
Basi bado hajapata somo! mfadhili mkuu wa ugaidi Duniani na Mmarekani na anafanya hivo kwa maslahi yake binafsi na si vinginevyo! Shemu kubwa ya mashariki ya kati inakumbwa na machafuko kwa interest za Marekani na ulaya.

Japo mimi ni Mkristu ila siwezi kulificha ili na ni upumbavu kuendelea kuamini kuwa DP World ataleta ugaidi, binafsi napinga terms and condistios za IGA ila sina tatizo na Kampuni ya DP World wala sina tatizo na Waarabu wala sina tatizo na United Arab Emirates.
Msome tena mleta mada kwenye komenti zake amesema DP World inatumika kueneza ugaidi na uislam.
 
Uzalendo ni kuchukua maaskofu na kwenda nao press conferences?
Uzalendo ni maaskofu kuacha makanisa na kwenda viwanjani kumtukana Rais?

Yaani uzalendo Tanzania wanao maaskofu tu?...
Wengineo wote hawana uzalendo??

Hao maaskofu wakati watu wanapigwa risasi uzalendo wao ulikuwa wapi??
Wacha Upotoshaji. Watu gani hao waliopigwa risasi halafu maaskofu hawakutia neno?
Wewe ni muongo
 
Another thread ingine ya uwongo na uzushi . ..from you ..
Wewe Jana umeanzisha thread unasema askofu Mwamakula kasema Dpworld watajenga msikiti...

Dpw world wamejenga msikiti UK walipopewa bandari?
German walijenga msikiti walipopewa bandari?..
China walijenga msikiti walipopewa bandari
South Africa walijenga msikiti walipopewa bandari?
Belgium walijenga msikiti walipopewa bandari?


Yaani Dpworld waendeshe bandari nchi 92 Duniani kote huko wasijjenge msikiti ila waje wajenge msikiti Mbeya??

Na kuna wajinga wanakuona unaongea vya maana?
Kuna mpotoshaji zaidi ya kwako wewe?
 
Uzalendo ni kuchukua maaskofu na kwenda nao press conferences?
Uzalendo ni maaskofu kuacha makanisa na kwenda viwanjani kumtukana Rais?

Yaani uzalendo Tanzania wanao maaskofu tu?...
Wengineo wote hawana uzalendo??

Hao maaskofu wakati watu wanapigwa risasi uzalendo wao ulikuwa wapi??
Maaskofu na mapadri unaowasema wameonyesha vipengere, vifungu na sehemu mbovu kwenye mikataba hiyo. Je wasisikilizwe ?!. Hao ma sheikh wameonyesha nini cha tofauti zaidi ya kutetea imani, ambayo si sehemu ya mgogoro huu.

Unapolinganisha vitu hivi lazima uwe smart. Hakuna anayepinga Dp world bali tatizo ni mkataba. Siku hizi unafeli wapi ?!
 
Ni rahisi sana kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini zao na CCM wanalifahamu vizuri jambo hili.

Hata kama kuna jambo baya sana kwa maslahi ya nchi yetu ukitaka likubalike basi wewe lipake rangi ya dini flani utaona mara moja watazuka watu na kulitetea kwa nguvu zao zote kwasababu tu jambo hilo lina rangi ya dini yao!

Suala la mkataba wa bandari limeonesha kuwa watanzania hawana misingi ya kusimamia isipokuwa mafungamano na dini zao.

Ni ajabu kubwa kwamba watu wapo tayari kuuza nchi yao kwa kuaminishwa kwamba hili ni jambo la kidini! CCM wanajua fika jambo hilo na wanalitumia sasa kama walivyolitumia kwenye chaguzi zilizopita dhidi ya CHADEMA na CUF.

Suala la bandari lilianza kujadiliwa vizuri kwa uzalendo lakini watu flani walipogungua linagusa dini yao sasa wamebadili hoja zao na bandari imekuwa suala la kidini.

Sakata la bandari sasa limekuwa suala la Uislamu; mwekezaji muislam, waziri mwislam na rais mwislam!
Ukiona hivyo basi ujue kuna upungufu flani Kwa hao wanao egemea dini
 
Back
Top Bottom