Kama hujawai kukutana na huo mgogoro huwezi kuelewa.Hicho unachokisema kupambana hapo patazuka ugomvi mkubwa ambao hukuutarajia.Hawachelewi kukimbilia polisi kua umemtishia maisha na kama unavyojua wanasikilizwaga ata kama anayoyaongea ni ujinga.mwisho wa siku wewe mwanaume ndio unaonekana mkorofi na unaingia gharama.ndo maana wanaume wengi wanaamuaga kukaa kimya nakuendelea na harakati zingine.Wanawake waone hivyo hivyo ndugu.
Niliambiwa na dada mmoja hivi!!
Si mkeo kaondoka na kwenda kupanga?
Nikamjibu ndio..
Akaniambia usimfuate we ishi maisha yako atarudi tu siku moja..
Nikamwambia pia nina muda wa yeye kurudi ukipita huo muda asitarajie tena.
Manzi akaniambia ukimfuata tu atakukatia RB na kukusingizia lolote baya.
Anaweza kusema hata kuwa ulitaka kumbakia binti yake..
Maana nilimkuta na mtoto wa kike wakati namuoa na mpaka anaondoka binti yake kafikisha miaka 17.
Akaniambia kaka yake aliwahi kushutumiwa hivyo na wifi yake tena kwa binti yake wa kumzaa kabisa je kwako ambae ni baba wa kambo utafanywa nini??
Nikabaki nalo moyoni..
Sasa ikaja siku nikamuita rafiki yake mke wangu waliokuwa wanaswampa pamoja
Nikamuonya kuhusu tabia yake ya kupenda kujipenyeza kwenye familia za watu na kuvunja ndoa aache atakuja kukutana na majanga..
Nikamwambia kwa aliyoyafanya sidhani kama nitamsamehe milele
Ila namuacha aende kwa kuwa sijapata cha kumfanya..
Akarusha mdomo sana na yuko ndqni kwangu na tuko wawili tu..
Shetani kwakuwa ni mshikaji wangu hakunituma vibaya siku hii aliniheshimu sana maana hata hasira nilikuwa nazitawala vyema.
Baadae akaenda wakayajenga na wife.
Sasa mimi nikiwa kijijini kwetu Mama akaniuliza hizi habari nikamueleza
Nikamuambia ngoja nimpigie simu na wewe usikie sauti kubwa.
Kwanza simu kupokelewa zikaanza shutuma oohoo umeanza kuwatishia marafiki zangu
Na maneno chungu nzima.
TUkajibizana pale mara akaniambia kwa taarifa yako nina RB yako usiwafuatilie marafiki zangu wala mimi.
NIkamuambia kama ni RB hata mimi naweza kukukatia fresh tu kama umefikia huko..
Akasema nimekukatia RB yaani unanifuatilia unataka kunibakia binti yangu??
Nikatabasamu kwa huzuni sana,, Mama alisikia akasema kajinga, Kashetani kabisa hako.
Nakupa miezi sita asiporudi tafuta mke mwingine oa.
Nikawaza miezi sita?
Mimi nishamaliza kupitia hiyo kauli tu,, Nilifanya kama alikufa tu na watoto nikampa ili siku nikioa niwashukie watoto wangu walipo kama Tai..
Ahsante Mungu naishi na mwingine, yeye amebaki kupiga simu tu na kusema wewe ishi na umtakae lakini kama Mungu alipanga uwe mume wangu utakuwa wangu tu.
Nasikitika tu rohoni mwangu..
Ile kauli itaishi ndani mwangu milele..
I wont find forgiveness for a such statement.
Yule dada nilipomueleza alisema, aliitarajia sana na shukurani ni kwamba sikumfuata pale alipohamia maana hiyo ndio silaha yao ya maangamizi wanayoitegemea kumuangushia mwanaume kwa madai ya huyu dada.