Tumeachana rasmi kwa kuwa mimi si Mchaga

Bahati Mbaya huwezi kueleza mabaya ya Mama yako aliyokuwa anamfanyie Mzee, na huwezi kuyaona au kutajua hadi utakapooa. Ndio maana aliamua kuondoka .
Mashangazi lazima walishangaa kazi unayofanya kwasababu unaonekana kabisa usoni kwamba huna akili sasa ukiwaeleza wanashangaa waliokuajiri waliwaza nini
 
😁😁😁😁😁 ilo neno "Chasaka" ni la kindezi sanaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚!!!
 
Mimi nimchaga pia...nataka kukupooza hayo machungu unayopitia
 
Umeambiwa ukweli ukapaa Tu.

We si unaonaga ni Raha kutukatana makabila ya watu ( kwa mihemuko na chuki zako Bila utafiti) lakin wew ukiambiwa ukweli unapinga kama vile wew msafi wa kila kitu.

Bro nyie ni wabaguzi,wabinafsi,wezi na wenye roho mbaya.
Wajomba zako watakuachia radhi wewe.
 
Dah pole sana dada. Huyo kijana hana akili sawa sawa. Yaani miaka mitano halafu mtu ndio anakuzima hivyo?!

Kama amedhakuonyesha hizo dalili basi umefanya maamuzi ya busara sana kuondoka.

But usije ukawazia vibaya kuwa jamii ya wachagga wapo hivyo, hizo ni tabia binafsi za mtu au familia yake. Mimi kuna rafiki yangu ni Mnyakyusa, alikutana na binti wa kichagga kwenye mwaka 2012 hivi.

Binti alikuwa amemaliza form 4. So akawa ana msapoti kuendelea na masomo kuanzia ngazi ya cheti. So binti alitoka cheti, diploma hadi degree akamaliza.

Alipomaliza jamaa amejiachia anajua mke wangu ndo huyu aanze mipango ya ndoa weeee, binti alimgeuka kama kitu gani sijui. Kisa tu familia yake walikwenda kumchunguza familia ya mshikaji na walipogundua maisha yao na kuwa ni wanyakyusa mmmmmmhmn walipita hivi fasta wakawa wanakwepa kutena kutoa ushirikiano na binti yao wakaoza kwa kabwana mdogo kengine kajitu ka huko huko moshi.


Nilipochunguza ndio nikaambiwa kuna baadhi ya familia za kichagga huwa wanaogopa sana jamii za wanyakyusa, wahaya nadhani na wasukuma..... Nadhani ni kwasababu wanahisi zina nguvu sana na zinaweza kuwa dominate. Especially mawifi wa kinyakyusa.......
So, mmmmmmmhmn kumbu kumesa...

Kuna neno huwa wanatumia kwa mwanaume wa jamii tofauti na yao, wanaita Chasaka kama sio kyasaka.....
 
Mnakaa miaka mitano ili mgundue nini huo ulikuwa uchumba sugu ni rahisi kufa
Kuna Maisha yanalazimu mtu avute muda mrefu katika mahusiano. Wanaweza kuwa walikutana akiwa sekondari then akaanza safari ya masomo ya chuo kikuu, ni zaidi ya miaka 5.....
 
Kuna Maisha yanalazimu mtu avute muda mrefu katika mahusiano. Wanaweza kuwa walikutana akiwa sekondari then akaanza safari ya masomo ya chuo kikuu, ni zaidi ya miaka 5.....
Dah ulivo mnafiki na huoni aibu ama kweli Kuna watu uso wa soni hamna
 
Dah ulivo mnafiki na huoni aibu ama kweli Kuna watu uso wa soni hamna
sasa unafiki wangu upo wapi?! Kwani umeambiwa kanuni ya mahusiano inatoa muongozo wa kuishi na mtu katika mahusiano kwa kipindi gani?!

Kila couple ina malengo ya tofauti. Kuna ambao wanamambo wanaweka sawa kwanza kabla ya kuingia ndoani, wengine wakikutana tu mambo yapo sawa so wanaingia katika ndoa straight ndani ya wiki mbili. Inategemea.
 
Hakuna mtu ambae si mbinafsi, Kama huyo dada si mbinafsi mbona hataki kuwa kwenye mahusiano hayo? Anayodai hataki kuwa nayo? Huo ndio ubinafsi namba moja.
Sasa Mkuu mtu ameshaambiwa kuwa anatakiwa Mchaga, kwa hiyo aendelee kudate na jamaa wakati hakuna hope huko mbeleni ili asiwe mbinafsi?
Mi ninamsifu hata kwa kuamua kuuface ukweli maana jamaa angemtumia kisha akafunga ndoa na Mchaga mwenzake kimya kimya.
 
Mimi mchaga na babangu ananikazia lazima nioe mchaga nikitaka kuoa.japo babangu ni muislamu pure alieshika dini



Ila mimi ni mchaga rebel sina kabisa mambo yao ya kichaga na nitaoa yoyote sitaki limit kwenye maisha yangu.
watakutenga tu ...lbda uwe na mipunga sana
 
Hapana ni mfano tu, warombo ni wanawake wazuri kwa hakika, wana roho ya utu, hofu ya Mungu na watafutaji pia sio watu wa kubweteka... hata mizigo wanayo si umeona mwenyewe!! Kila la Kheri mkuu.
Hapo kwenye mizigo hapana, strictly Machame tuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ila kwa rangi na ngozi laini ni hapo Marangu mangiπŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Sawa mzee tumekusikia, kila la heri kwenye kutawaza wazee hapo Denmark!
 
Mkuu vipi hawa wa Rombo ukoo wa shirima wanashida gani.?
Mchumba wangu ni wa huko na ukoo wake ni shirima , wanashida yoyote hawa.?
Shida ni hela zako tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ zisije zikakata ghafla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…