Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

Kitabu cha kwanza ni QUR'AN yenyewe, Wakati Mtume Muhammad alikufa, Quran ilikuwa imeandikwa kikamilifu. Haikuwa katika fomu ya kitabu, hata hivyo. Ilirekodiwa kwenye ngozi na vifaa tofauti tofauti, na nyingine ilikuwa imehifadhiwa kichwani na Masahaba wa Mtume.

Ali Ibn Abi Talib huyu ni swahaba wa Mtume na aliandika vitabu vingi ikiwemo Nahjul Balagha, Al-Saheefah Al-Alawiyah , Nahj al-hikma wa ul-balagha na vingine vingi.
 
Unajuaje Kama wanaouliza wote ni wakristo au ni kujistukia mkuu wakt unajua kabisa majina yenyewe hayaeleweki haya.
 
baada ya jibu hili nimesitisha nilichotaka kuuliza, nimepata ukakasi na ujuzi na uadilifu wa mtoa mada.....kuna kitu kinaniambia tofauti, the guy is here just to make fun of islam!!!
Hiyo ni hoja mkuu imeukusanya na mawazo yangu ndani yake. Kama una hoja weka hapa tuwe na bainisho la mawzo yako ndani ya maandiko kama sehem ya udadavuaji wako.. Simpo
 
Kuna ukweli wowote kuhusu Mtume kumuoa mke wa mwanaye, lingine kwanini yeye alioa wake zaidi ya 7 ila kwa Waislam wengine mwisho wanne kwann yeye wawe wengi
Alioa wake wengi baada ya kufariki kwa mke wake wa kwanza Bi Khadija, mtume alioa kwa sababu ya kijamii au kisiasa; vile alitaka kuwaheshimu wanawake wacha Mungu, au alitaka uaminifu wa makabila fulani ili Uislam uenee kati yao. Wake wote ambao Muhammad alioa hawakuwa bikra, wala hawakuwa vijana au wazuri. Sisi waisilamu wengi MUNGU ametutaka kuoa mwisho wa 4 nasio zaidi, bali nafasi hiyo alipewa mtume pekee kutokana na sababu nilizokupatia
 
Je ni kweli mtume alizaliwa akiwa ametahiriwa?

Je ni kweli mtume hakuwa na kimvuli hata alipotembea juwani?

Je Uislami unaamini Masia ndio atahukumu wazima na wafu siku ya mwisho.?
Ahsante ndugu.
Ndio ni ukweli Muhammad s.a.w alizaliwa bila ya govi (tayari alikuwa ameshatahiriwa) na alama au muhuri wa unabii alikuwa nao mabegani.

Ndio, ni kweli kivuli chake hakikuwahi kukanyaga ardhini, Inaaminika kwamba kila nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu alikuwa na alama yake kwenye sehemu fulani ya mwili wake. Muhammad hakuwa na kivuli ardhini, ilitafsiriwa kama ishara ya "nuru" yake. Pia Muhammad alikuwa akisikia sauti za watu ambao walikuwa wakiteswa katika makaburi yao.

Masia ukimaanisha nini ?
 
Jitahidi kupitia marejeo yako(vitabu).
Buraq alitumika kutoka Macca hadi Jerusalem (Israa). Kutoka Jerusalem hadi mbinguni ilitumika ngazi(mi-iraaj).
Ndio sababu ya kuitwa safari hiyo "israa na mi'iraaj)
Ni sahihi kabisa ndugu yangu, sema naandika kwa haraka sana. Shukran ulamaa
 
Manaswara hawatakua radhi nanyi hadi mfuate mila zao

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kuweka chanzo cha kihistoria kuwa Quran ilikuwa compiled Karne ya 7? Data zote nilizoziona ni kuwa ilikuwa compiled angalau miaka 200 baadaye. Kitu kinachomaanisha hakukuwa na shuhuda hata mmoja.

Huyu swahaba aliandika vitabu vyake karne ya ngapi?
 
Alikuwa na umri gani?

Hadija pia alikuwa na umri gani?

Je ni kweli alishapita na mke ya "jamaa flani" alipoenda kumtembelea na akakuta jamaa hayupo?
Aisha alikua na miaka 6 lakini aliamza kulala nae kama mke akiwa na miaka 9.
Hadija alikua na miaka 40 pindi anaolewa na mtume ambaye alikua na miaka 25 .
Kuhusu kupita na mke wa jamaa alipomtembelea sijui ingawa alimuoa mke wa zayd lakini baada ya kuachwa na zayd
 
Miaka 19 ndipo mtume alifariki akiwa na miaka 63
 
Kwasababu aliyo yaleta Muhammad s.a.w ni mfano wa yale yale yaliyoletwa na mitume wengine waliokuwa kabla yake.
Kijografia na kiteolojia kwann kunautofauti?
Namaanisha mitume yoote (mayahudi) iliyotangulia mafundisho yao hawakutofautiana, kwann yeye amekuja tofauti pamoja na kukubali au kuyabeba baadhi ya mafundisho ya kiyahudi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…